Taylor Swift na Travis Kelce wafunga ndoa jijini New York

Chanzo cha picha, Kevin Mazur/Getty Images
Baada ya miezi kadhaa Taylor Swift na Travis Kelce hatimaye wamefunga ndoa katika ukumbi wa Madison Square Garden jijini New York, Marekani
Taarifa hizo Habari hizo zilithibitishwa Ijumaa jioni na msemaji wa Swift,huku skrini kubwa nje ya ukumbi huo zikionyesha ujumbe: "JUST&T MARRIED!"
Swift, ambaye ni nyota mkubwa zaidi wa muziki wa pop duniani, na Kelce, bingwa mara tatu wa Super Bowl, walivishana pete ya uchumba Agosti mwaka iliyopita, na tangu wakati huo mashabiki wamekuwa wakijiuliza ndoa itafungwa lini, wapi na vipi tukio hilo lingefanyika.
Hafla hiyo ya siku mbili ilisababisha mojawapo ya maeneo yenye shughuli nyingi zaidi jijini New York kufungwa, huku orodha ya wageni ikijumuisha msururu wa mastaa wakubwa kama vile Selena Gomez, Camila Cabello, Hugh Grant, Gracie Abrams, Ellie Goulding, Graham Norton na Dakota Johnson.
Hakuna picha rasmi zilizotolewa kutoka ndani ya ukumbi huo, na wengi kati ya waliohudhuria—wanaokadiriwa kufikia 1,000—waliingia bila kupigwa picha, ingawa baadhi yao walionekana wakati wakiingia na kutoka.























