Mzozo wa Sudan: Watu 87 wapatikana katika kaburi la halaiki Darfur - UN
Mapigano makali kati ya RSF na wanajeshi wa Sudan yamekuwa yakiendelea tangu mwezi Aprili.
Moja kwa moja
Vifo vya waandamanaji Kenya vimeongezeka hadi 13 - shirika la kutetea haki za binadamu
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Anthony Irungu
- Nafasi, BBC News, Nairobi

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Maandamano hayo yalichochewa na mipango ya serikali ya kuongeza ushuru Idadi ya waliofariki nchini Kenya siku ya Jumatano katika maandamano kuhusu gharama ya juu ya maisha imeongezeka kutoka sita hadi 13, kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu nchini humo.
Tume ya Haki za Kibinadamu ya Kenya (KHRC) inasema watu 10 waliuawa na polisi, akiwemo mtoto mdogo, huku watu watatu wakifariki katika ghasia za kijamii zilizosababishwa na maandamano magharibi mwa nchi.
KHRC inachunguza ripoti kwamba polisi walishindwa kuingilia kati mapigano kati ya jamii, Davis Malombe, anayeongoza tume hiyo, alisema.
Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki anasema watu 312 akiwemo mbunge wa upinzani walikamatwa wakati wa maandamano na watafunguliwa mashtaka.
"Maafisa wa usalama wameagizwa kutekeleza sheria kwa uthabiti na kuwashughulikia wahalifu wote, wakiwemo wahujumu uchumi, waporaji na waharibifu wa mali ya umma na ya kibinafsi," waziri alisema katika taarifa yake.
Aidha ameeleza nia ya serikali ya kuwakamata viongozi wa upinzani Raila Odinga na Martha Karua walioitisha maandamano hayo.
Lakini upinzani bado umekaidi, huku mwanachama mkuu wa muungano huo, Edwin Sifuna, akiambia runinga ya Citizen ya Kenya siku ya Alhamisi, kwamba maandamano yataendelea wiki ijayo Jumatatu, Jumanne na Jumatano.
Soma zaidi:
Kenya: Gavana wa zamani Wycliffe Oparanya amekamatwa - Raila Odinga

Chanzo cha picha, TWITTER
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga anasema aliyekuwa Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya amekamatwa.
Akihutubia wanahabari Alhamisi Alasiri, Odinga alithibitisha kuwa Oparanya alikamatwa kuhusiana na maandamano ya kupinga serikali yaliyoongozwa na upinzani siku ya Jumatano.
Oparanya alikuwa miongoni mwa viongozi wa upinzani waliokuwa wakiongoza maandamano dhidi ya serikali Magharibi mwa Kenya.
Huku hayo yakijiri upinzani umetangaza kuwa maandamano yake dhidi ya serikali yataendelea tena kote nchini kote Jumatano wiki ijayo.
Katika mkutano na wanahabari Alhamisi alasiri, Muungano wa Upinzani wa Azimio la Umoja One Kenya Kenya ukariri azma yake ya kuishinikiza serikali kupunguza gharama ya maisha.
Bw Odinga alisema maandamano hayo yatafanyika iwapo serikali itatoa kibali au la.
''Tuko tayari kukamatwa na kupelekwa mahakamani''. alisema Odinga.
Maelezo zaidi:
- Maandamano Kenya:Mateso yatakuwa jambo la kawaida iwapo Ruto ataruhusiwa kutekeleza Sheria ya Fedha-Raila
- Takriban watu sita wameuawa katika maandamano nchini Kenya
- Kwanini maandamano ya Kenya yanaweza kuleta msiba Tanzania na Uganda?
Mzaliwa wa Nigeria nyota wa MMA amfunza Zuckerburg kumenyana na Musk

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Israel Adesanya ni bingwa wa Ultimate Fighting Championship (UFC) uzito wa kati Mzaliwa wa Nigeria bingwa wa Dunia wa mixed martial arts (MMA) Israel Adesanya ameweka picha kwenye Twitter akimfundisha bilionea wa teknolojia wa Marekani Mark Zuckerberg.
Hatua hiyo inawadia kabla ya mechi inayowezekana kutokea kati ya bosi wa Meta, anayemiliki Facebook na Instagram, na mpinzani wake Elon Musk - mjasiriamali mzaliwa wa Afrika Kusini ambaye sasa anaongoza Twitter.
"Sote tuna Waafrika Kusini wa kukabiliana nao," Adesanya alitania siku ya Alhamisi, akiwa na picha nne za wawili hao wakifanya mazoezi pamoja.
Bondia huyo mwenye umri wa miaka 33, ambaye alihamia New Zealand akiwa mtoto, ameratibiwa kumenyana na Dricus du Plessis wa Afrika Kusini katika pambano la Ultimate Fighting Championship (UFC) uzito wa kati mnamo Septemba.
Adesanya alisafiri hadi kwenye makazi ya Bw Zuckerberg kaskazini mwa California siku ya Jumamosi kuanza mazoezi yao, kulingana na ripoti za vyombo vya habari.
Bw Zuckerberg, 39, na Musk, 52, walikubali pambano lao kwenye mitandao ya kijamii mwezi uliopita.
Tarehe ya pambano hilo bado haijathibitishwa lakini wawili hao kwa sasa wako kwenye pambano lingine huku Meta ikizindua mbadala wa Twitter wiki iliyopita.
Mtandao wa Threads hadi sasa umesajili zaidi ya watu milioni 70.
Pia unaweza kusoma:
Kampuni ya India yabadilisha 90% ya wafanyikazi wake wa huduma kwa wateja na Akili Bandia

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni moja nchini India amekosolewa vikali baada ya kubadilisha asilimia 90 ya wafanyakazi wake wa huduma kwa wateja na kutumia chatbot ya akili bandia (AI).
Suumit Shah, mwanzilishi wa Dukaan, alisema kwenye Twitter kwamba chatbot iliboresha sana majibu ya awali kwa wateja na wakati wa kutatua maswali yao.
Tweet hiyo ilizua hasira kutoka kwa watumiaji wengi wa mtandao. Ilikuja wakati ambapo kuna wasiwasi kwamba AI inaweza kuwafanya watu wengi kupoteza kazi, hasa katika sekta ya huduma.
Alidai kuwa kuachisha kazi wafanyakazi ni uamuzi "mgumu" lakini ni "lazima" kufanya hivyo.
"Kwa kuzingatia hali ya uchumi, wanaoanza biashara wanatanguliza faida kuliko kujaribu kubuni 'ajira,' na sisi pia tunafanya hivyo," aliandika.
Shah aliongeza kuwa usaidizi wa wateja umekuwa tatizo kwa kampuni kwa muda mrefu na alikuwa akitafuta suluhisho.
Pia aliandika kuhusu jinsi walivyounda jukwaa la roboti na AI kwa muda mfupi ili wateja wote wa Dukaan waweze kuwa na msaidizi wa haraka. Alihakikisha kuwa bot inajibu kila aina ya maswali haraka na kwa usahihi.
"Katika umri wa kuridhika papo hapo, kuanzisha biashara sio tatizo tena," aliandika, na kuongeza: "Kwa wazo sahihi, timu sahihi, mtu yeyote anaweza kugeuza ndoto zao za ujasiriamali kuwa ukweli."
Shah pia alisema kuwa kampuni hiyo inaajiri kwa nyadhifa nyingi lakini, watumiaji wengi walikosoa machapisho yake na kumshutumu kwa kuvuruga maisha ya wafanyikazi wake ka njia "ya kikatili".
Maelezo zaidi:
- Kwanini kuna hofu juu ya teknolojia ya akili bandia?
- Akili Bandia: Ni kazi gani zinaweza kuwa hatarini zaidi?
- Wanafunzi sasa wageukia Akili Bandia kujifunza lugha mbali mbali
Mzozo wa Sudan: Watu 87 wapatikana katika kaburi la halaiki Darfur - UN

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Maelfu wameuawa katika miezi mitatu ya mapigano nchini Sudan Miili ya watu wasiopungua 87 wanaodaiwa kuuawa na Rapid Support Forces (RSF) nchini Sudan imepatikana katika kaburi la halaiki, kulingana na UN.
Shirika hilo lilisema watu wa Masalit ni miongoni mwa waliozikwa kwenye kaburi lisilo na kina kirefu nje kidogo ya El-Geneina.
Mapigano makali kati ya RSF na wanajeshi wa Sudan yamekuwa yakiendelea tangu mwezi Aprili.
Lakini RSF na wanamgambo washirika wao wamekanusha kuhusika katika mapigano ya hivi majuzi huko Darfur Magharibi.
Maelfu wamefariki dunia na mamilioni wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na mapigano kati ya jeshi la kawaida la Sudan linaloongozwa na Abdel Fattah al-Burhan na RSF inayoongozwa na naibu wa zamani wa al-Burhan, Mohamed Hamdan Daglo.
Umoja wa Mataifa umesema takriban miili 37 ilizikwa katika eneo la Darfur Magharibi tarehe 20 Juni, na mingine 50 katika eneo hilo hilo siku iliyofuata.
Miongoni mwa waliozikwa ni wanawake na watoto.
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Volker Türk alisema "amechukizwa na jinsi wafu, pamoja na familia zao na jamii, walivyotendewa" bila huruma tena kwa dharau.
Alitoa wito wa uchunguzi wa vifo vyao na kusema kwamba RSF inalazimika kuwachukulia waliokufa kwa "utu".
Mapema wiki hii, RSF ilikataa madai kutoka kwa Human Rights Watch kwamba waliwaua watu 28 wa jamii ya Masalit na kujeruhi makumi ya raia kabla ya kuharibu mji wa Misteri mwezi Mei.
Pia unaweza kusoma:
Daktari wa Kenya: Nilitibu watoto waliopigwa mabomu ya kutoa machozi bure

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Daktari wa Kenya: Nilitibu watoto waliopigwa mabomu ya kutoa machozi bila mapilo Daktari wa Kenya ameambia BBC kwamba hospitali yake imewatibu watoto 53 bila malipo baada ya gesi ya kutoa machozi kurushwa darasani mwao na polisi wakati wa maandamano siku ya Jumatano.
"Kama mzazi, niliitikia kwa matumaini na kwa hofu, jambo ambalo lilinilazimu kuchukua hatua bila kuomba pesa," Dkt Aron Shikuku, kutoka hospitali ya kibinafsi ya Eagle Nursing Home katika mji mkuu, Nairobi, aliambia kipindi cha Newsday cha BBC.
Huduma ya afya nchini Kenya inaweza kuwa ya gharama kubwa huku asilimia 19 pekee ya watu wakipata aina yoyote ya bima ya matibabu - kulingana na takwimu za hivi punde za 2018.
Hospitali za umma nchini kwa kawaida hazina wahudumu wa kutosha na hazina vifaa vya kutosha huku gharama ya kupata matibabu katika hospitali ya kibinafsi mara nyingi inaweza kusababisha kulemaza kwa shughuli kutokana na deni la matibabu.
Dk Shikuku alisema watoto hao waliruhusiwa Kwenda nyumbani baada ya kutibiwa kwa mshtuko na matatizo ya kupumua kutokana na gesi ya kutoa machozi.
Alisema walikuwa wakifuatiliwa walipokuwa wakitulia katika shule yao, iliyoko Kangemi, eneo la makazi duni kaskazini-magharibi mwa jiji.
Kulikuwa na maandamano kote nchini yaliyoitishwa na upinzani juu ya kupanda kwa gharama ya maisha, lakini yaligeuka kuwa mauti.
Watu sita waliuawa, mamlaka ilisema.
Unaweza pia kusoma
Tazama: Jinsi Korea Kaskazini ilivyofanya jaribio lake la kombora
Vyombo vya habari vya serikali ya Korea Kaskazini vimetangaza video inayoonesha jaribio la hivi punde la kombora la balestiki lililorushwa na nchi hiyo Jumatano asubuhi.
Kombora hilo liliruka kwa zaidi ya saa moja kabla ya kutua chini ya maji ya Japan.
Jaribio hilo la Pyongyang linajiri baada ya kutishia kulipiza kisasi dhidi ya kile ilichosema ni uvamizi wa hivi majuzi wa ndege za kijasusi za Marekani katika eneo lake.
Jaribio hilo limelaaniwa na Japan, Korea Kusini na Marekani.
Jenerali wa Urusi afutwa kazi baada ya kulikosoa jeshi

Chanzo cha picha, ANDREI GURULYOV
Jenerali wa ngazi ya juu wa Urusi anasema ameondolewa kwenye wadhifa wake nchini Ukraine baada ya kuwaambia wakuu wa kijeshi ukweli kuhusu hali mbaya iliyopo kwenye mstari wa mbele.
Meja Jenerali Ivan Popov alikuwa kamanda wa Jeshi la 58, ambalo limekuwa likipigana katika eneo la kusini la Zaporizhzhia.
Katika ujumbe wa sauti, Meja Jenerali Popov alisema aliuliza maswali juu ya kiwango cha juu cha majeruhi na ukosefu wa msaada wa silaha.
"Ilikuwa ni lazimani niseme ilivyo ama ninyamaze na kukaa kuwa mwoga," alisema.
"Sikuwa na haki ya kusema uwongo kwa jina lako, kwa jina la wenzangu waliokufa mikononi, kwa hivyo nilielezea shida zote zilizopo."
Ujumbe huo wa sauti ulitumwa kwa telegram na Mbunge wa Urusi Andrei Gurulyov, ambaye ni kamanda wa zamani wa kijeshi na mtoa maoni wa mara kwa mara kwenye TV ya serikali. Haijulikani ni lini ujumbe huo ulirekodiwa.
Miongoni mwa masuala ambayo Meja Jenerali Popov alisema aliangazia kwa wakubwa wake ni ukosefu wa mifumo ifaayo ya betri za kaunta kusaidia kuzima mashambulio ya Vifaru vya Ukraine, pamoja na ukosefu wa ujasusi wa kijeshi.
Kamanda huyo anasema kuachishwa kwake kazi kulitakiwa na makamanda wakuu - ambao aliwashutumu kwa uhaini - na kuidhinishwa na waziri wa ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu.
Azimio kufanya maandamano ya kupinga serikali kwa siku 3 wiki Ijayo - Sifuna

Chanzo cha picha, Raila Odinga facebook
Maelezo ya picha, Raila Odinga juu ya gari Katibu mkuu wa chama cha upinzani cha ODM nchini Kenya ambaye pia ni Seneta wa jiji la Nairobi Edwin Sifuna ameitisha maandamano ya siku tatu kuanzia wiki ijayo, akiapa kuzidisha maandamano dhidi ya serikali hadi matakwa yao yatakapotekelezwa.
Kulingana na Sifuna, maandamano hayo ya siku tatu kila wiki yatafanyika kuanzia Jumatatu hadi Jumatano na yatakamilika tu wakati Rais William Ruto atakapokubali kupitia upya Sheria ya Fedha ya 2023 yenye utata.
"Kuanzia wiki ijayo, siku tatu mfululizo za maandamano, Jumatatu, Jumanne, Jumatano hadi William Ruto atakapoelewa kuwa watu wanateseka na kubatilisha sheria hii jinsi alivyoiweka juu yao," alisema.
Akizungumza katika kipindi cha runinga ya Citizen mapema leo Alhamisi , alisema kwamba serikali inafaa kusikiliza matakwa ya Wakenya wengi kabla ya kuchukua suala hilo mikononi mwao.
"Ni afadhali wakati huu ambapo watu kama Sifuna, Raila, Osotsi (Seneta wa Vihiga), wanaongoza maandamano haya. Siku Wakenya watakaposhughulikia suala hili wenyewe hakutakuwa na mtu wa kuwaita kwenye meza," alisema.
Pia aliikemea serikali kwa kutangaza awali kuwa itawakamata viongozi wa Azimio wakidai kwamba hawatarudi nyuma katika vita vya dhidi ya serikali na wako tayari kukamatwa kwa sababu hiyo .
"Hakuna mtu atakayetutishia. Hakuna kitu ambacho hawa watu (Kenya Kwanza) hawajasema. Hakuna wanachoweza kututisha nacho. Ikiwa ni kukamatwa tuko tayari," alibainisha Sifuna.
Rais wa Iran azishtumu nchi za Magharibi kwa kuunga mapenzi ya jinsia moja

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Rais wa Iran Raisi Rais wa Iran Ebrahim Raisi amelaani mitazamo ya nchi za Magharibi juu ya kuunga mkono mapenzi ya jinsia moja wakati wa ziara yake nchini Uganda ambayo imeweka sheria kali dhidi ya LGBTQ kwa mujibu wa mtandao wa NTV Uganda.
Raisi akiwa nchini humo kuimarisha uhusiano na Afrika katika ziara yake ya kwanza ya kiongozi wa Iran barani humo katika kipindi cha miaka 11, alizishtumu nchi hizo za magharibi katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mazungumzo na rais wa Uganda Yoweri Museveni.
"Magharibi siku hizi zinajaribu kukuza wazo la mapenzi ya jinsia moja wanajaribu kukomesha kizazi cha wanadamu," Raisi alitangaza.
Museveni alitia saini mswada huo kuwa sheria mnamo Mei 29, na kuvutia hasira miongoni mwa mashirika ya kutetea haki za binadamu, Umoja wa Mataifa na wanaharakati wa LGBTQ pamoja na mataifa yenye nguvu kutoka Magharibi.
Sheria hiyo mpya inafanya "mapenzi ya jinsia moja yaliokithiri" kuwa kosa la kifo huku adhabu kwa mahusiano ya watu wa jinsia moja yenye maelewano yakiwa adhabuya hadi kifungo cha maisha jela.
Wanaume wageni 'ruksa' kusuka nywele ukiwa Zanzibar

Chanzo cha picha, Getty Images
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema sheria inayokataza wanaume kusuka visiwani Zanzibar haiwagusi wageni kutoka mataifa mengine, bali vijana wa Zanzibar
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Tabia Maulid Mwita ikiwa ni siku moja baada ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Sensa ya Elimu na Utamaduni visiwani humo, Dr Omary Adam kueleza kuwa ni marufuku kwa wanaume kusuka visiwani Zanzibar.
Dr. Adam alikuwa akirejea Sheria namba saba ya mwaka 2015 kifungu cha saba kinachozungumzia kulinda mila, silka na tamaduni za kizanzibar.
Akitoa ufafanuzi wa kauli hiyo, Waziri Mwita amesema: 'Tukisema tuachie (wanaume kusuka) haya ndio mambo ambayo yanayoleta vitu vingi vya hatari hasa kwa vijana wetu, lakini tuendelee ku-stick (kusimamia) kwamba Zanzibar suala la wanaume kusuka kiutamaduni, silka zetu na mila zetu kwa kweli halikubali'.
Hata hivyo Mwita ameongeza kuwa Zanzibar ambayo ni sehemu ya Tanzania ina heshimu na kutambua masuala ya kidiplomasia na utamaduni wa watu wengine
'Pindi wanapokuja wageni ambao wamesuka basi sisi hatuwezi kuwa-force (kuwazuia) kwamba wao wasisuke kwa sababu huko kwao utaratibu umeruhusu, wana uhuru wao pia kwa sababu tayari wameshaelekeza imani zao kwenye huko, na Zanzibar wapo hawajawahi kuguswa', alisema.
Siku mbili zilizopita kwenye mitandao ya kijamii kumekua na mjadala mkubwa unaoendelea nchini Tanzania kuhusu kauli ya Katibu wa Baraza la Sanaa visiwani humo kupiga marufuku wanaume kusuka katika visiwa hivyo vyenye kupokea wageni wengi kutoka mataifa mbalimbali.
Ikielezwa ili kupata kibali cha kuruhusiwa kusuka kutoka Baraza la Sanaa, wanaume wanapaswa kulipia shilingi milioni 1, kauli ambao Waziri Mwita amesema Baraza hilo halina Mamlaka ya kutoa kibali cha kusuka nywele na ni kinyume na maadili.
Misri kuandaa kikao cha kuisaidia Sudan
Misri inatarajiwa kuandaa leo mkutano wa kilele kujadili namna ya kuisaidia Sudan kujikwamua kutoka kwa mzozo uliozuka kati ya jeshi la nchi hiyo na kikosi cha wanamgambo wa Rapid Support Forces RSF.
Mapigano yamekuwa yakiendelea Sudan kwa zaidi ya miezi mitatu na kusababisha mzozo mkubwa kibinadamu nchini humo ambapo zaidi ya watu elfu wameuawa na mamilioni kuachwa bila ya makazi.
Pande zote mbili zinazohasimiana zinatuma wajumbe katika mkutano huo wa Misri.
Juhudi nyingi za usulushi zimefanywa bila ya mafanikio. Hapo jana, Rais wa Misri Abdel Fattah al Sisi na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed walikutana mjini Cairo kuujadili mzozo huo wa Sudan.
Vita vya Ukraine: Jenerali mwandamizi anayehusishwa na Wagner Sergei Surovikin ambaye 'amepumzika'

Chanzo cha picha, EPA
Kamanda wa zamani wa Urusi ambaye hajawahi kuonekana tangu ya uasi uliotekelezwa na kundi la Wagner mwezi Juni anapumzika , kulingana na mbunge mmoja mwandamizi katika bunge la taifa hilo.
Andrei Kartapolov, mwenyekiti wa kamati ya ulinzi , alisema kwamba jenerali Sergei Surovikin alaikuwa hapatikani , na kuzua wasiwasi kuhusu kule aliko.
Ripoti ambazo hazijathibitishwa zinasema kwamba jenerali Surovikin amezuiliwa kwa mahojiano kuhusu kuhusika kwake katika uasi huo.
Amedaiwa kuwa na uhusiano wa karibu na mkuu wa Wagner Yevgeny Prigozhin.
Mamluki wa Wagner walijaribu jaribio la uasi tarehe 23 na 24 mwezi Juni walipotishia kuelekea Moscow.
Uasi huo ulisitishwa baada ya rais wa Belarus Alexander Lukashenko kuingia makubaliano na Prigozhin.
Wapiganaji wa Wagner wametakiwa kujiunga na jeshi la Urusi , waende nyumbani au waende kuhudumia Belarus.
Siku ya jumatano , wizara ya ulinzi ilisema kwamba kundi hilo lilikuwa likikamilisha mpango wa kutoa silaha na vifaa vyengine vya kijeshi , ikiwemo ni Pamoja na vifaru 2000, vifaa vya kurushia roketi, bunduki za kukabiliana na ndege na silaha nyneginezo.
Jenerali Surovikin mara ya mwisho alionekana hadharani katika kanda ya video wakati wa uasi akiwataka wanajeshi wa Wagner kusitisha vitendo vyao.
Ripoti za vyombo vya habari baadaye zilisema alikuwa amekamatwa , lakini hakujakuwa na uthibitisho rasmi ama tamko kuhusu aliko.
Jenerali huyo alikuwa akisimamia Vikosi vya Urusi nchini Ukraine mwezi Oktoba lakini akandolewa miezi mitatu
Lijipatia sifa kwa ukatili wakat iwa operesheni nchini Syria ambapo alijulikana kuwa jenerali Armageddon
Huko Ukraine alisimamia mashambulio mabaya dhidi ya miundombinu ya nishati, na kuwaacha mamilioni ya raia bila umeme au maji wakati wa msimu wa baridi.
Nafasi yake ilichukuliwa Januari na Mkuu wa Wafanyakazi Jenerali Valery Gerasimov, na kuwa naibu wake.
Nato yaionyesha Ukraine haiwezi kupata kila kitu inachohitaji

Chanzo cha picha, EPA
Volodymyr Zelensky anaweza kuwa au asiwe shabiki wa Rolling Stones - lakini baada ya mkutano huu wa kilele wa Nato, pengine anafahamu wimbo wao unaoitwa You Can't Always Get What You Want.
Rais wa Ukraine alifika Vilnius, Lithuania, akiwa na matarajio makubwa.
Alikuwa akitafuta hakikisho kwamba nchi yake ingejiunga na Nato baada ya vita na Urusi kumalizika.
Alitaka uanachama wa muungano wa kijeshi wenye nguvu zaidi duniani uwe mwanga wa matumaini kwa watu wake, mgawanyiko wa mwisho wa amani ambao ungehakikisha kwamba wanajeshi wa Urusi hawatateka tena nchi ya Ukraine.
Badala yake, Bw Zelensky aliambiwa tu kwamba Ukraine ingealikwa kuwa mwanachama "wakati washirika watakapokubali na masharti kutekelezwa". Hadi sasa, hivyo hakuna hakikisho.
Haishangazi rais wa Ukraine aligonga paa, alikasirika na kusema ni "upuuzi" kwa viongozi wa Nato kutotoa hata ratiba. Masharti, alisema, yalikuwa "hayaeleweki".
Na alikasirishwa na wazo kwamba kwa namna fulani uanachama wa Ukraine wa Nato ungekuwa njia ya mazungumzo ya baada ya vita na Urusi.
Lakini mara tu Rais Zelensky alipokutana na viongozi wa Nato ana kwa ana, vumbi la kidiplomasia lilitanda. Walimuhakikishia wao wenyewe siku ya Jumatano kwamba mambo yalikuwa yamebadilika, na kwamba Ukraine ingejiunga na Nato.

