Jenin: Waombolezaji wajaza mitaa ya Jenin huku Israeli ikisitisha mashambulio
Mazishi ya watu waliouawa Jenin yamekuwa yakifanyika leo asubuhi
Moja kwa moja
Mahakama Kuu Kenya yaongeza maagizo yanayozuia Utekelezaji wa Sheria ya Fedha ya 2023

Chanzo cha picha, Thinkstock
Maelezo ya picha, Mahakamani Mahakama Kuu imeongeza muda wa maagizo ya kusitisha utekelezaji wa Sheria ya Fedha ya 2023 ambayo iliongeza bei mpya ya mafuta nchini Kenya.
Katika uamuzi uliotolewa Jumatano jioni, Jaji Mugure Thande aliongeza maagizo hayo kwa siku tano zaidi hadi Jumatatu, Julai 10, 2023, wakati ombi lililowasilishwa na Seneta Okiyah Omtata litakaposikizwa.
Okiya Omtatah alipinga utekelezwaji wa Sheria ya Fedha kwa misingi kwamba bunge la Seneti halikuhusika katika kupitisha sheria hiyo tata.
Wakati huo huo, Omtatah pia amewasilisha ombi la kutaka Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli (EPRA) ishtakiwe kwa kudharau agizo la mahakama baada ya kutekeleza bei mpya ya mafuta licha ya utekelezaji wa Sheria hiyo kusitishwa na mahakama.
Ombi la EPRA kudharau agizo la mahakama litatajwa na kuamuliwa wiki ijayo.
Omtatah amepewa saa 48 kuwapatia agizo hilo jipya watetezi
Serikali ya Uganda kudhibiti vipimo vya DNA

Chanzo cha picha, Getty Images
Serikali ya Uganda imechukua hatua ya kudhibiti upimaji wa chembe za urithi (DNA) ikisema kwamba inajua hatari iliyopo kwa jamii ikiwa sekta hiyo itaachwa bila kudhibitwa.
Waziri wa Habari na mwongozo wa Taifa Dr. Chris Baryomunsi aliambia bunge kuwa serikali inachukua hatua mara moja kulinda maslahi ya umma huku kukiwa taarifa za familia kusambaratika.
Katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita, Uganda imekuwa ikikabiliana na taarifa za kutatanisha ambapo wanaume wengi wanawasilisha maombi ya kutalakiana na wake zao, huku wengine wakiendelea na kutaka kubadilisha hata stakabadhi za watoto katika sajili ya data ya kitaifa baada ya vipimo vya DNA kuonyesha kwamba wao sio baba halali wa watoto ambao wamekuwa wakiwachukulia kuwa wao.
Carlo Ancelotti kuwa kocha wa Brazil 2024, asema rais Ednaldo Rodrigues

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Carlo Ancelotti ameshinda Ligi ya Mabingwa mara nne kama meneja na mara mbili akiwa na Real Madrid Mkufunzi wa Real Madrid Carlo Ancelotti atachukua mikoba ya kuinoa Brazil msimu ujao, asema rais wa Shirikisho la Soka la Brazil Ednaldo Rodrigues.
Washindi hao mara tano wa Kombe la Dunia wana uhakika Muitaliano huyo atakuwa tayari kwa Copa America mnamo Juni 2024.
Rodrigues alisema Fernando Diniz atasimamia Selecao hadi wakati huo, pamoja na jukumu lake kama bosi wa Fluminense.
"Atakuja na kufanya mabadiliko huko Brazil kwa Ancelotti," Rodrigues alisema.
"Mpango wake wa mchezo unakaribia kufanana na ule wa kocha atakayechukua mikoba ya Copa America, Ancelotti.
"Hatumwiti kocha wa muda wa timu ya taifa."
Brazil imekuwa bila kocha mkuu wa kudumu tangu Kombe la Dunia, Tite alipojiuzulu kufuatia kushindwa kwao robo fainali na Croatia, huku kocha wa vijana chini ya umri wa miaka 20, Ramon Menezes akisimamia mechi za kirafiki za hivi majuzi.
Ancelotti, ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao wa joto, atakuwa meneja wa kwanza wa kigeni kuifundisha Brazil tangu 1965.
Hakujawa na taarifa rasmi kutoka kwa Ancelotti au Real Madrid kwamba ataondoka katika klabu hiyo mwaka ujao.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 64 alianza kipindi chake cha pili Bernabeu mnamo 2021, baada ya kuondoka Everton, na ameshinda Ligi ya Mabingwa, La Liga, Copa del Rey na Kombe la Dunia miongoni mwa msururu wa mafanikio tangu arejee.
Ushindi wa fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Liverpool mwaka 2022 ulikuwa ushindi wa nne kwa Ancelotti wa Ulaya kama meneja, na wa pili akiwa na Real Madrid, baada ya kushinda shindano hilo mara mbili akiwa na AC Milan.
Soma zaidi:
Aimable Karasira apewa muda wa kutoa ripoti yake kuhusu ugonjwa wake wa akili

Ripoti ya kitabibu kuhusu afya ya akili ya Aimable Karasira inasema ugonjwa wake haujamnyima uwezo wa kufikiri.
Hii inapelekea yeye kuendelea kusimama kizimbani kwa kesi yake.
Yeye na mawakili wake wanasema ana ugonjwa wa mfadhaiko uliotokana na mauaji ya kimbari wakidai hakuna budi kwanza kutibiwa kabla ya kesi yake kuendelea.
Karasira anatuhumiwa kwa makosa ya kukana mauaji ya kimbari na kuyahalalisha.
Upande wa mashtaka uliongeza makosa ya hongo na kutoweka wazi chanzo cha utajiri wake.
Hata hivyo anakanusha mashtaka yote dhidi yake.
Leo mahakamani, Karasira alisema hakupewa nafasi ya kuwasilisha maoni yake kuhusu ripoti ya matibabu iliyofanywa na madaktari 3 na kwamba alinyanyaswa na gereza anamozuiliwa.
Karasira alisema kuwa yeye ndiye anapaswa kuamua nini kinakwenda kwenye hitimisho lake la ripoti ya madaktari, akisema hii ni kutokana na kwamba kuna mambo ambayo hakubaliani na mawakili wake ingawa aliwachagua mwenyewe hasa kuhusu chanzo cha mfadhaiko wake.
Alisema, “Watu wangu waliuawa na wanajeshi wa RPF, mawakili wangu nao kuna maoni yangu ambayo wanaogopa, mfano nikisema hivyo hawawezi kuniunga mkono, hawaamini kwamba tunaweza kuweka kauli hiyo kwenye ripoti.
Anaongeza: "Kigumu zaidi ni kwamba ninatuhumiwa kwa mauaji ya kimbari na kwa upande mwingine nina 'kiwewe' cha mauaji ya kimbari."
Kenya yachelewesha ufunguzi wa mpaka wake na Somalia kutokana na wasiwasi wa usalama

Serikali ya Kenya imeahirisha mpango wa kufungua tena vituo vya mpaka kati ya Kenya na Somalia, kulingana na Waziri wa mambo ya ndani na utawala wa kitaifa.
Kindiki alisisitiza kuwa kucheleweshwa kufungua tena vituo vya mpaka ni muhimu ili kukabiliana na ongezeko la hivi karibuni la mashambulizi ya kigaidi na uhalifu wa kuvuka mpaka ambao umekumba eneo hilo katika miezi ya hivi karibuni.
Serikali inalenga kutoa ulinzi zaidi kwa raia wake huku ikihakikisha uzingatiaji wa majukumu ya kimataifa.
"Serikali itachelewesha mpango wa kufungua tena vituo vya mpaka wa Kenya na Somalia hadi tutakaposhughulikia kwa ukamilifu msururu wa hivi majuzi wa mashambulizi ya kigaidi na uhalifu wa kuvuka mipaka" alisema Kindiki.
Amekiri kuwa, wakati idadi kubwa ya wakimbizi ni watu wanaotii sheria wanaotafuta hifadhi, idadi ndogo wametumia hali yao ya ukimbizi kujihusisha na vitendo vya uhalifu vikiwemo vitendo vya kigaidi.
Ili kushughulikia maswala haya, Kenya ilitekeleza Sheria ya Wakimbizi iliyopitiwa tena na kuboreshwa mwaka wa 2022, ikipatanisha sera za nchi na mikataba ya kimataifa.
Serikali imejitolea kutekeleza majukumu yake chini ya mikataba hii.
Habari za hivi punde, Jenin: Risasi 'zafyatuliwa hewani' kwenye misafara ya mazishi
Kama ambavyo tumekuwa tukiripoti, maelfu ya watu wamejiunga na maandamano ya mazishi huko Jenin asubuhi ya leo kwa Wapalestina waliouawa.
Miili hiyo ilipobebwa kwenye mitaa iliyojaa uchafu, BBC iliona wanamgambo wakifyatua risasi hewani.
Umati wa watu pia ulisikika wakiimba huku msafara huo ukipitia Jenin.
Soma zaidi:
Walifunua nguzo kutoka katika sinagogi na ubao wa mawe unaoonyesha baadhi ya Amri Kumi

Chanzo cha picha, Alamy
Maelezo ya picha, Hitler aliamuru kuharibiwa kwa sinagogi kuu la jiji hilo mnamo Juni 1938 Miaka themanini na mitano baada ya Adolf Hitler kuamuru kuharibiwa kwa sinagogi kuu la Munich, wafanyikazi wa ujenzi wamepata vifusi kutoka kwa jengo hilo kwenye mto wa karibu.
Walifunua nguzo kutoka katika sinagogi na ubao wa mawe unaoonyesha baadhi ya Amri Kumi.
Jumuiya ya Wayahudi na watu wa eneo hilo wamefurahishwa na ugunduzi huo.
"Hatukuwahi kufikiria kwamba tungepata chochote kutoka kwayo," alisema Bernhard Purin, mkuu wa jumba la makumbusho la Kiyahudi la Munich.
Hakukuwa na dalili ya jengo hilo tangu lilipobomolewa Juni 1938, baada ya Hitler kudai kuondolewa kwake kama jengo "linalotisha".
Miezi mitano baadaye, Wayahudi, masinagogi na biashara zinazoendeshwa na Wayahudi walishambuliwa kote Ujerumani ya Wanazi katika mauaji ya Novemba yanayojulikana sana kama Kristallnacht.
"Jana niliona [mabaki] kwa mara ya kwanza na ilikuwa moja ya wakati wa kusisimua zaidi katika miaka 30 ya kufanya kazi katika makumbusho ya Wayahudi, hasa kuona bamba la Amri Kumi ambalo halijaonekana tangu 1938," Bw Purin aliambia BBC.
Vifusi kutoka kwa jengo hilo la kihistoria inadhaniwa kuwa vilizama ndani ya Mto Isar tangu lilipotumika kujenga upya ukuta wa ajabu miaka 11 baada ya Vita vya Pili vya Dunia.
Soma zaidi:
Mji wa Ethiopia chini ya amri ya kutotoka nje huko Amhara baada ya tukio la kufyatuliwa risasi

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Wanamgambo wa Amhara, waliopigwa picha hapa 2021 huko Shewa Robit, wameambiwa wajiunge na polisi au jeshi. Mji wa Ethiopia chini ya amri ya kutotoka nje huko Amhara baada ya tukio la upigaji risasi
Picha: Wanamgambo wa Amhara, waliopigwa picha hapa 2021 huko Shewa Robit, wameambiwa wajiunge na polisi au jeshi.
Mauaji ya mkuu wa usalama katika mji mmoja katika eneo la Amhara nchini Ethiopia yamesababisha marufuku ya kutotoka nje usiku na kuongezeka kwa hali ya wasiwasi.
Tangu Aprili hali ya usalama katika eneo la Amhara imekuwa ikizorota kufuatia uamuzi wa kuvunja kundi la wanamgambo wa eneo hilo.
Kila jimbo la nchi hiyo limekuwa na vikosi vyake maalum, lakini serikali imehamia kuwaweka chini ya jeshi na polisi.
Maandamano mabaya dhidi ya serikali yalizuka kujibu huko Amhara.
Amri ya kutotoka nje iliwekwa katika mji wa Shewa Robit baada ya Abdu Hussein, mkuu wa idara ya usalama ya eneo hilo, kupigwa risasi na watu wasiojulikana siku ya Jumanne.
Ni mauaji ya tatu kama haya ndani ya siku nyingi huko Amhara.
Mkuu wa polisi na mkuu wa usalama katika wilaya nyingine alikuwa ameuawa kwa kupigwa risasi.
Mamlaka katika Shewa Robit, ambayo ni karibu kilomita 200 (maili 124) kaskazini-mashariki mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Addis Ababa, imepiga marufuku watu na magari kusafirishwa baada ya saa 18:00 za ndani.
Vikosi maalum vya Amhara vilisaidia jeshi la Ethiopia kupambana na wapiganaji wa Tigray ambao walianzisha uasi mnamo 2020 dhidi ya serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed.
Mzozo huo ulimalizika Novemba mwaka jana kwa kutiwa saini mkataba wa amani.
Vikosi vya Somalia vinachukua maeneo yaliyoachwa na wanajeshi wa AU

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Vikosi vya AU vimekuwa vikiisaidia serikali ya Somalia kupambana na waasi Vikosi vya Somalia vimechukua majukumu ya usalama katika sekta tano kati ya sita ambapo wanajeshi wa Umoja wa Afrika (AU) wametumwa.
Wizara ya ulinzi ilisema ilithamini "jinsi walivyojitolea" kwa miaka mingi na ujumbe wa AU na nchi ambazo zimechangia wanajeshi - Burundi, Djibouti, Ethiopia, Kenya na Uganda.
Kauli hiyo ilikuja baada ya mpango wa kuondoka kwa wanajeshi 2,000 wa AU - wanaotarajiwa kuwa waliondoka kufikia tarehe 30 Juni.
Kambi nyingi za kijeshi zilizokabidhiwa hadi sasa ziko katika eneo la Lower Shabelle na ziliendeshwa na kikosi cha Burundi cha ujumbe huo.
Wanajeshi wengine 3,000 wa AU wanatarajiwa kuondoka mwishoni mwa Septemba - huku kikosi kizima kikitarajiwa kuwa nje ya Somalia mwishoni mwa 2024.
AU imekuwa ikisaidia serikali ya Somalia kupambana na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la al-Shabab tangu mwaka 2007.
Soma zaidi:
Onana ana nia ya kutaka kujiunga na Manchester United

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Onana Kwa kuwa sasa Manchester United wamemsajili Mount, umakini wao unageukia idara ya makipa.
Haya yanajiri baada ya habari kuwa David de Gea amekuwa mchezaji huru baada ya kutotolewa uamuzi wowote iwapo atasalia Old Trafford.
Mtandao wa 90 min sasa unaripoti kwamba mchezaji wa Inter Milan Andre Onana, 27, amekataa nia yakuelekea Saudi Arabia na badala yake anatalka kujiunga na United.
Soma zaidi:
Mason Mount hatimaye ajiunga na Man United

Chanzo cha picha, Manchester United
Maelezo ya picha, Mason Mount Mason Mount alisema mpango wa Erik ten Hag wa Manchester United ulimshawishi kuondoka katika klabu yake ya utotoni ya Chelsea.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 ndiye mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Ten Hag msimu huu wa joto katika mkataba wa uhamisho wenye thamani ya pauni milioni 55, pamoja na nyongeza zinazowezekana za pauni milioni 5.
Mount amesaini mkataba wa miaka mitano na chaguo la mwaka zaidi.
"Baada ya kukutana na meneja, na kujadili mipango yake, sikuweza kufurahishwa zaidi na misimu iliyo mbele," alisema mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Mount.
Pia unaweza kusoma:
Madhya Pradesh: Mwanaume wa India akamatwa kwa kumkojolea mfanyakazi wa kabila la tabaka la chini

Chanzo cha picha, Getty Images
Polisi katika jimbo la kati la India la Madhya Pradesh wamemkamata mwanamume mmoja kwa kumkojolea mfanyakazi wa jamii inayokandamizwa hadharani.
Pravesh Shukla ameshtakiwa chini ya Sheria ya Jamii na Kabila Zilizoratibiwa (Kuzuia Ukatili) - sheria inayokusudiwa kulinda jamii zilizokandamizwa kihistoria.
Alikamatwa baada ya video inayomuonyesha akimkojolea mwanaume huyo kusambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii.
Tukio hilo limezua taharuki nchini.
Bw Shukla hajazungumza lolote kuhusu tukio hilo.
Baadhi ya wanasiasa wa chama kikuu cha upinzani Congress wamedai kwamba anahusishwa na chama tawala cha Bhartiya Janata Party (BJP) - ambacho pia kiko mamlakani huko Madhya Pradesh.
Hata hivyo, BJP imekanusha madai hayo.
Polisi pia walikataa kuzungumzia madai hayo, wakisema kwamba "ukweli wa kesi hiyo unahitaji kuchunguzwa kwanza".
Licha ya sheria zilizokusudiwa kuwalinda watu wa kabila, ubaguzi dhidi yao na watu wengine wa tabaka la chini nchini India - wanaofikiriwa kuwa karibu milioni 200 - bado ni uhalisia unaotokea kila siku.
Ni baadhi ya raia waliokandamizwa sana nchini humo kwa sababu ya tabaka la Wahindu lisilosamehe ambalo linawalaani hadi wale wa chini kabisa katika tabaka.
Soma zaidi:
Utafiti wa kinyesi cha tembo nchini Kenya unaonyesha wanakula lishe tofauti

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Watafiti walichanganua DNA ya mmea iliyopatikana kwenye kinyesi cha tembo nchini Kenya Wanasayansi nchini Marekani wanasema wamegundua kwamba tembo hula milo ya aina mbalimbali, huku kila mmoja wao akichagua kati ya mamia ya mimea ili kukidhi mahitaji na matamanio yao.
Katika utafiti huo , watafiti katika Chuo Kikuu cha Brown walichanganua vinasaba (DNA) vya mimea iliyopatikana kwenye kinyesi cha ndovu nchini Kenya.
Waligundua kwamba mlo wa tembo mmoja, wa nyasi, majani, matunda na mizizi, ulikuwa tofauti zaidi kuliko ilivyojulikana hapo awali - hata kati ya familia zilizokula pamoja.
Walisema hili lilionekana dhahiri zaidi miongoni mwa tembo wa kike ambao walikuwa wajawazito au wanaowalisha watoto wao.
Wanasayansi wanatumai maarifa haya ya lishe yatasaidia katika uhifadhi wa tembo wa mwituni.
Kanisa lililogawanyika la Uingereza kujadili kubariki ndoa ya wapenzi wa jinsi moja

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby amekuwa akisisitizia umuhimu wa kubariki ndoa za wapenzi wa jinsi moja makanisani Baraza linaloongoza la Kanisa la Anglikana la Uingereza litajadili jinsi makasisi wanavyoweza kutoa baraka kwa wapenzi wa jinsia moja litakapokusanyika katika jiji la York kwa mkutano wa siku tano siku ya Ijumaa.
Kusanyiko la maaskofu, makasisi na waumini - liitwalo Sinodi Kuu - pia linatazamiwa kujadili siku ya Jumamosi jinsi ya kuwalinda makasisi ambao wanaweza kuchagua kutoombea miungano ya wapenzi wa jinsia moja.
Kanisa la England( CoE), ambalo haliruhusu ndoa za jinsia moja katika makanisa yake 16,000, mnamo Januari lilitoa mapendekezo ya kuwaruhusu wapenzi wa jinsia moja kuwa na ibada ya maombi baadaya ndoa ya kiserikali, na liliomba msamaha kwa wapenzi wa jinsia mona ( LGBTQI+) kwa kukataliwa na uhasama ambao wamekabiliana nao. Sinodi ilipiga kura kuunga mkono mipango hiyo mwezi Februari.
Hilo lilisababisha kundi la kihafidhina la viongozi wa kanisa la kianglikana kutoka duniani kote kutangaza kuwa hawana imani tena na Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby, wakisema kuwa amesaliti kusimikwa kwake rasmi kama Askofu Mkuu wa Kanisa hilo.
Hata hivyo nchini Uingereza, kuna shinikizo la kwenda mbali zaidi, huku baadhi ya maaskofu wakijitokeza hadharani kuunga mkono ndoa za jinsia moja zifungwe makanisani.
Mgawanyiko umekuwa mkubwa kwa miongo kadhaa kuhusu jinsi taasisi ya karne nyingi - kanisa mama kwa Waanglikana milioni 85 duniani kote katika nchi 165 - linahusika na mapenzi ya jinsi moja na miungano ya watu wa jinsi moja. Mapenzi ya jinsi moja ni mwiko barani Afrika na ni haramu katika nchi zaidi ya 30 huko.
Welby, ambaye ni kiongozi wa kiroho wa ushirika mpana wa Kianglikana, alitoa wito kwa maaskofu mwaka jana "kuzidi katika upendo kwa wote". Lakini aliunga mkono uhalali wa azimio lililopitishwa mwaka 1998 ambalo lilikataa "mazoea ya mapenzi ya jinsi moja kuwa hayapatani na Maandiko".
Askofu Sarah Mullally aliwaambia waandishi wa habari mwezi uliopita: "Hiki hakijakuwa kipindi rahisi kwa watu katika mila mbalimbali na tunajua kwamba labda imekuwa ngumu zaidi tangu Februari kuliko ilivyokuwa hapo awali."
Alikariri kwamba mapendekezo hayatabadilisha fundisho kwamba ndoa ni kati ya mwanamume na mwanamke, na kwamba kutakuwa na ulinzi kwa wale ambao "kwa misingi ya dhamira yao" wanachagua kutobariki wapenzi wa jinsia moja.
Wanaharakati wa mapenzi ya jinsi moja , watu wa jinsi mbili na waliobadili jinsia (LGBT) kwa muda mrefu wamekuwa wakipigania haki sawa ya Wakristo wenzao ambao wanaooana na jinsi tofauti.
Ndoa ya wapenzi wa jinsi moja imekuwa halali nchini Uingereza kwa muongo mmoja.
Sudan Kusini : Rais Salva Kiir aahidi kugombea uchaguzi wa kwanza nchini humo

Chanzo cha picha, AFP
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, Jumanne ameahindi kwamba uchaguzi uliocheleweshwa uliopangwa kufanyika mwaka ujao utaendelea kama ilivyopangwa na kwamba atawania urais.
Kiir, ambaye ni kamanda mkuu wa wapiganaji wa msituni, amekuwa rais pekee wa taifa hilo tangu alipoliongoza kupata uhuru wake kutoka kwa Sudan mwaka 2011.
Kipindi cha mpito kilikusudiwa kuhitimishwa na uchaguzi mnamo Februari 2023, lakini serikali hadi sasa imeshindwa kufikia vifungu muhimu vya makubaliano, ikiwa ni pamoja na kuandaa katiba.
"Ninakaribisha uidhinishaji wa kugombea urais mwaka 2024," Kiir aliwaambia wafuasi wa chama chake tawala cha Sudan People's Liberation Movement, akilielezea kama "tukio la kihistoria."

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Hasimu wa Kiir Riek Machar(kulia) anatarajiwa kugombea urais katika uchaguzi ujao Hakuna mgombea mwingine ambaye ametangaza kugombea, lakini adui wa kihistoria Riek Machar anatarajiwa kugombea.
Mwezi Agosti, viongozi hao wawili waliongeza serikali yao ya mpito kwa miaka miwili zaidi ya muda uliokubaliwa, wakitaja haja ya kushughulikia changamoto zilizokwamisha utekelezaji wa makubaliano ya amani.
Unga unaoshukiwa kuwa wa Cocaine uliopatikana katika Ikulu ya Marekani wazua wasi wasi

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Huduma za ujasusi zilisema unga huo mweupe - unaodhaniwa kuwa kokeni - ulipatikana katika eneo la kazi la White House. Kitu cheupe kilichosababisha uhamishaji wa dharura wa wafanyakazi katika Ikulu ya White House Jumapili usiku kilithibitishwa kuwa na cocaine.
Kitu hicho cheupe kilipatikana katika eneo la kazi wakati wa ukaguzi wa kawaida, Huduma za Siri za Marekani zilisema.
Rais Joe Biden na familia yake walikuwa mbali katika makazi ya Camp David wakati Cocaine hiyo hiyo ilipopatikana.
Jumba la White House lilifungwa kama tahadhari mwendo wa mbili na dakika 45 kwa saa za Marekani (01:45 BST) siku ya Jumapili baada ya maafisa wa huduma za ujasusi kupata unga mweupe "ndani ya eneo la kazi" la West Wing, msemaji wa Huduma za ujasusi Anthony Guglielmi aliambia BBC katika taarifa.
Bw Guglielmi alisema idara ya zima moto iliitwa haraka na kubaini kuwa mzigo huo "sio hatari".
Alisema furushi hilo limetumwa kwa uchunguzi wa ziada na kwamba uchunguzi unaendelea, ikiwa ni pamoja na kubaini ni vipi mihadarati hiyo iliingia Ikulu.
Mabadiliko ya hali ya hewa: Siku ya joto zaidi duniani kuwahi kurekodiwa

Chanzo cha picha, STR
Maelezo ya picha, Watu wanapata shida nchini Uchina kutokana na wimbi la joto linaloendelea Wastani wa hali ya joto duniani ulifikia kiwango cha juu zaidi mnamo Jumatatu tarehe 3 Julai, na kuzidi nyuzi joto 17 kwa mara ya kwanza.
Watafiti wa Marekani walisema rekodi hiyo mpya ilikuwa ya juu zaidi katika rekodi yoyote muhimu iliyowahi kurekodiwa kuanzia mwisho wa karne ya 19.
Wanasayansi wanaamini kuwa mchanganyiko wa tukio la hali ya hewa la asili linalojulikana kama El Niño na utoaji unaoendelea wa wanadamu wa hewaya kaboni dioksidi ndio unaosababisha joto.
Mwezi uliopita pia umethibitishwa kuwa ndio mwezi Juni wenye joto zaidi duniani kuwahi kurekodiwa.
Wanasayansi katika Vituo vya Kitaifa vya Utabiri wa Mazingira wa Marekani walisema kuwa wastani wa joto duniani umefikia 17.01C tarehe 3 Julai, na kuvunja rekodi ya awali ya 16.92C ambayo ilikuwakatika kiwango hicho tangu Agosti 2016.
Tangu kuanza kwa mwaka huu, watafiti wamekuwa na wasiwasi juu ya kuongezeka kwa hali ya joto ardhini na baharini.
Rekodi joto la msimu wa vuli nchini Uhispania na nchi nyingi za Asia kuwa na mawimbi ya joto baharini katika sehemu ambazo kwa kawaida hayaonekani, kama vile Bahari ya kaskazini.
Wiki hii China iliendelea kukumbwa na wimbi la joto la kudumu na halijoto katika baadhi ya maeneo ya juu ya 35C, wakati Amerika Kusini pia ikiripotiwa kuwa na hali mbaya ya joto.
Kiwango cha juu zaidi cha Jumatatu ndicho cha joto zaidi tangu rekodi za ufuatiliaji wa satelaiti zilipoanza mwaka wa 1979.
Majambazi wenye silaha wampiga mwandishi wa habari wa Urusi na wakili

Chanzo cha picha, SERGEI BABINETS/CREW AGAINST TORTURE
Maelezo ya picha, Yelena Milashina na wakili Alexander Nomov walipelekwa hospitali kwa kutibiwa ya majeraha waliyopata Mwanahabari mashuhuri Yelena Milashina amepigwa vibaya na watu waliofunika nyuso zao muda mfupi baada ya kuwasili jamhuri ya Urusi ya Chechnya.
Alielezea kulazimishwa kutoka kwenye gari, kugongwa na mabomba ya plastiki na kunyolewa kichwa na kumwagiwa rangi ya kijani karibu na uwanja wa ndege.
Bi Milashina amepokea vitisho vya kuuawa siku za nyuma kutoka kwa kiongozi mashuhuri wa Chechnya, Ramzan Kadyrov.
Alikuwa akisafiri na wakili Alexander Nemov, ambaye pia alijeruhiwa.
Walikuwa ndio mwanzo wametua kwenye uwanja wa ndege wa Grozny ili kuhudhuria uamuzi wa mahakama wa mama wa wakosoaji watatu wa Kadyrov waliokimbilia uhamishoni. Lakini hawakuweza kusikiliza kesi hiyo, ambapo Zarema Musayeva alihukumiwa kifungo cha miaka mitano na nusu jela kwa mashtaka yaliyodaiwa kuwa ya kisiasa.
Chechnya imekuwa ikiendeshwa na Ramzan Kadyrov tangu 2007. Mshirika mkubwa wa Vladimir Putin na kiongozi wa vita vya Ukraine, amekuwa akishutumiwa kwa kuamuru mauaji ya kiholela, utekaji nyara na mateso nyumbani.
Mwandishi wa habari na wakili huyo walieleza jinsi gari lao lilivyovamiwa na kundi la watu wasiopungua 10 waliojifunika nyuso zao kwenye magari matatu mwendo mfupi kutoka uwanja wa ndege. Baadaye walisema wanaamini watu hao walikuwa wakiwasubiri ndani ya uwanja wa ndege.
CTE: Ugonjwa wa ubongo wagunduliwa kwa mwanariadha wa kike kwa mara ya kwanza

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Heather Anderson akicheza mpira wa miguu wa Sheria za Australia mnamo 2017 Wanasayansi wa Australia wanasema wamefanya uchunguzi wa kwanza duniani wa ugonjwa sugu wa kiwewe cha ubongo (CTE) kwa mwanariadha mtaalamu wa kike.
Uchunguzi juu ya ugonjwa wa kupungua kwa ubongo, unaohusishwa na michezo ya mawasiliano, kawaida hufanyika kwa wanariadha wa kiume.
Utambuzi huo ulifanywa kwenye ubongo wa Heather Anderson, mwanasoka wa Australian Rules ambaye alijiua mwaka jana akiwa na umri wa miaka 28.
Wanasayansi wanasema kesi hiyo inaweza kuwa "ncha ya barafu" kwa wanawake katika michezo.
CTE husababisha ongezeko la hatari ya ugonjwa wa akili na pia imehusishwa na shida ya akili, lakini inaweza tu kutambuliwa baada ya kifo. Wanasayansi wanaamini kuwa ilisababishwa na kugonga kichwa mara kwa mara na mtikisiko, na- utafiti wa taasisi 13 za kitaaluma mwaka jana kupata "ushahidi wa uhakika".
Utafiti kuhusu hali hiyo umekuwa ukiongezeka katika miaka ya hivi karibuni - huku zaidi ya kesi 300 zikitambuliwa katika soka la Marekani pekee.
Nchini Australia, wanasoka mashuhuri wa kiume wa Sheria za Australia Danny Frawley, Shane Tuck na Polly Farmer waligunduliwa kuwa na CTE, kama ilivyokuwa kwa mchezaji wa zamani wa ligi ya raga Paul Green.
Lakini utafiti wa CTE katika nyota wa michezo wa kike umekuwa mdogo.
