Waandishi 6 wakamatwa baada ya kuvuja kwa video inayomuonyesha rais akitokwa na haja ndogo hadharani

Mnamo Desemba, video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ilionekana ikimuonyesha Bw Kiir akijikojolea huku wimbo wa taifa ukipigwa kwenye hafla.

Moja kwa moja

  1. Sudan Kusini: Waandishi 6 wakamatwa kutokana na kuvuja kwa video inayomuonyesha rais akitokwa na haja ndogo hadharani

    sALVA kiir

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Waandishi sita wa habari nchini Sudan Kusini wamekamatwa kutokana na kusambaa kwa picha za video zinazomuonyesha Rais Salva Kiir akitokwa na haja ndogo, mashirika ya kutetea haki za vyombo vya habari yanasema.

    Mnamo Desemba, video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ilionekana ikimuonyesha Bw Kiir akijikojolea huku wimbo wa taifa ukipigwa kwenye hafla.

    Wafanyakazi sita kutoka shirika la utangazaji la serikali walikamatwa wiki hii. Kamati ya Kulinda Wanahabari (CPJ) sasa inataka waachiliwe.

    Patrick Oyet, rais wa Muungano wa Waandishi wa Habari wa Sudan Kusini, aliambia Reuters kwamba waandishi hao "wanashukiwa kufahamu video hiyo ilivujaje".

    Shirika la Utangazaji la Sudan Kusini (SSBC) linasema video hiyo hiyo haikuonyeshwa kwenye kituo hicho.

    Waziri wa Habari wa Sudan Kusini Michael Makuei aliiambia Sauti ya Amerika kwamba watu wanapaswa kusubiri kujua kwa nini wanahabari hao walikamatwa.

    Mashirika ya kutetea haki za binadamu mara kwa mara yametaka mamlaka za Sudan Kusini kuacha kuwanyanyasa na kuwatishia waandishi wa habari.

    Bw Kiir alikua rais wa kwanza wa Sudan Kusini - nchi mpya zaidi barani Afrika - mnamo 2011. Lakini nchi hiyo imekumbwa na mizozo mingi tangu wakati huo, ikivumilia migogoro ya kikatili, machafuko ya kisiasa, majanga ya asili na njaa.

  2. Filippo Bernardini: Akiri kutumia kipaji cha kuigiza watu mashuhuri kuiba

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mtu mmoja, mwenye kipaji cha kuigiza sauti za watu maarufu raia wa Italia amekiri kuiba zaidi ya miswada 1,000 ya vitabu ambavyo haviijachapishwa, mingi ikiwa imeandaliwa na waandishi mashuhuri.

    Filippo Bernardini alikuwa akiwaiga watu mashuhuri kwenye tasnia ya uchapishaji ili kuwahadaa watu ili wakabidhi kazi zao kwake.

    Kwa ufupi alikuwa akijifanya kama mhariri, ama mchapishaji, ama muandaaji kutoka kampuni fulani ambayo inaaminika, kwa sauti yake na matendo yake wengi walifikiri ni mtu sahihi na kutoa kazi zao kwako, kumbe alikuwa akiiwaiga

    Alitumia ujuzi wake wa ndani wa tasnia, akiwa ameajiriwa na kampuni kubwa ya uchapishaji Simon & Schuster huko London.

    Bernardini, 30, amekutwa na hatia ya kufanya matendo hayo ya kulaghai huko New York, lakini nia yake haijawahi kuwa wazi.

    Baada ya kupata miswada hiyo, haikuvuja kwenye mtandao, wala hakudai madai yoyote ya fidia.

    Kuhukumiwa kwa Bernardini, ambaye alikamatwa na FBI Januari mwaka jana, inaonekana kuelezea fumbo ambalo limesumbua ulimwengu wa fasihi kwa miaka, huku Margaret Atwood, Ian McEwan na Sally Rooney wakiwa miongoni mwa waandishi wanaolengwa.

    Waendesha mashtaka walisema alisajili zaidi ya akaunti 160 bandia vya mtandao kuanzia 2016, kutekeleza azma yake.

  3. Mtoto wa miaka 6 ampiga risasi mwalimu wake baada ya kugombana nae darasani

    USA

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mtoto mdogo wa kiume mwenye umri wa miaka sita anashikiliwa na polisi baada ya kumpiga risasi mwalimu wake huko Virginia nchini Marekani, maafisa wanasema.

    Tukio hilo limetokea katika Shule ya Msingi ya Richneck katika jiji la Newport News, Mkuu wa Polisi wa eneo hilo Steve Drew alisema.

    Haijulikani ni jinsi gani mtoto huyo aliipata bunduki hiyo, lakini Bw Drew alisema kuwa tukio hilo halikuwa "la bahati mbaya".Mwalimu huyo - ambaye hakutajwa jina na anasemekana kuwa na umri wa miaka 30 - amepata majeraha makubwa ya kutishia maisha yake.Alipelekwa katika hospitali ya eneo hilo na anafuatiliwa kwa karibu na madaktari.

    Tukio hilo lilitokea katika chumba cha darasa la kwanza (chenye wanafunzi wa umri wa miaka sita hadi saba) baada ya kutokea ugomvi kati ya wawili hao.

    Lakini Bw Drew alisisitiza kwamba ufyatuaji risasi huo umekuwa tukio la pekee na akasisitiza kwamba maafisa "hawakuwa na taarifa kwamba kuna mtu alikuwa akizunguka maeneo ya shule akiwa na bunduki".Maafisa walisema wakati shule hiyo - ambayo ina wanafunzi wapatao 550 - ilikuwa na vifaa vya kugundua chuma ikiwemo silaha, wanafunzi walikaguliwa bila mpangilio na sio kila mtoto alikaguliwa.

    Polisi walikataa kutaja silaha iliyotumika katika tukio hilo, lakini walisema kijana huyo alitumia bunduki.

    Afisa anayesimamia Shule katika eneo hilo, Dkt George Parker alisema maafisa "watakuwa wakichunguza tukio lolote ambalo linaweza kuwa limesababisha tukio hili"."Hii ni mbaya, jambo kama hili halipaswi kutokea kamwe," Dk Parker aliongeza.

    "Tunataka kuhakikisha hakuna kitu kama hiki kinatokea tena."Alisema shule hiyo itafungwa Jumatatu, na kuahidi kuwa wanafunzi na wazazi watapewa msaada ili kuwasaidia kukabiliana na tukio hilo lililosababisha taharuki.

  4. Watu 29 wauawa wakati wa kumkamata mtoto wa El Chapo, kinara wa dawa za kulevya duniani

    Elchapo son

    Chanzo cha picha, Reuters

    Takriban watu 29 wameuawa wakati wa operesheni ya umwagaji damu ya kumkamata mtoto wa mfalme wa Mexico "El Chapo", mamlaka ya Mexico ilisema.

    Ovidio Guzmán-López, 32, anayedaiwa kuwa kiongozi wa genge la zamani la babake,linalojishughulisha na dawa za kukevya alikamatwa huko Culiacán na kusafirishwa hadi Mexico City siku ya Alhamisi.

    Lakini wakati na baada ya kukamatwa kwake, askari 10 na washukiwa 19 waliuawa.

    Wanachama wa genge lake wenye hasira waliweka vizuizi barabarani, wakachoma moto makumi ya magari na kushambulia ndege katika uwanja wa ndege wa eneo hilo.

    Wanajeshi wengine 35 walijeruhiwa na watu 21 wenye silaha walikamatwa, Waziri wa Ulinzi Luis Cresencio Sandoval alisema Ijumaa.

    El chapo son

    Chanzo cha picha, US STATE DEPARTMENT

    Bw Guzmán-López - anayeitwajina la utani "Panya" - alipakizwa kwenye helikopta na kusafirishwa hadi mji mkuu kabla ya kupelekwa katika gereza la shirikisho lenye ulinzi mkali.

    Anatumiwa kwa kuongoza kundi la baba yake maarufu la Sinaloa – mojawapo ya magenge makubwa zaidi ya ulanguzi wa dawa za kulevya duniani.

    Baba yake, Joaquín "El Chapo" Guzmán, anatumikia kifungo cha maisha jela nchini Marekani baada ya kupatikana na hatia mwaka wa 2019 ya ulanguzi wa dawa za kulevya na utakatishaji fedha.

  5. Hatimaye Marekani yapata Spika baada ya kura kurudiwa mara 15 kwa siku 4

    USA

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Kevin McCarthy amechaguliwa kuwa Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani huku kukiwa na majibizano makali ambayo karibu yashuhudiwe wawakilishi wa chama chake cha Republican washikane mashati.

    Bw McCarthy hatimaye ameshinda nafasi hiyo baada ya duru 15 za upigaji kura, licha ya chama chake kuwa na kura nyingi katika bunge.

    Ushindi wake umekuja baada ya kampeni kali ya shinikizo iliyofanywa na kushuhudiwa mubashara huku mmmoja wa waasi wa chama Matt Gaetz aliyekuwa hamuungi mkono mwanasiasa huyo alihimizwa kumpigia kura Bw McCarthy.

    USA

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Congressman wa Florida alikuwa miongoni mwa watu sita ambao walijiuzulu Ijumaa.

    Hapo awali, huku kukiwa na majibizano makali, Bw Gaetz alikuwa karibu apigwe na Mwakilishi Mike Rogers - mfuasi wa Bw McCarthy. Mbunge huyo wa Alabama alilazimika kuzuiwa na wenzake alipokuwa akimfokea na kumnyooshea kidole Bw Gaetz.

    Nchini Marekani Spika wa bunge hilo huweka ajenda za Bunge na husimamia shughuli za kutunga sheria. Nafasi hiyo ni ya pili kwa ukubwa nchini Marekani kama ilivyo kwa makamu wa rais baada ya Rais wa Marekani.