Urusi na Ukraine: Mashambulio ya makombora ya masafa ya Urusi yapiga Odessa na chuguev

Mashambulio ya makombora ya masafa ya Urusi katika mji wa Chuguev uliopo katika jimbo la Kharkiv limeharibu shule, majengo na makazi kadhaa ya watu, limesema shirika la habari la Ukraine la UNIAN

Moja kwa moja

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo, tukutane tena hapo kesho majaaliwa

  2. Rwanda: Adhabu ya kifungo cha miaka 22 jela yapendekezwa kwa waandishi wa habari

    Waandishi

    Chanzo cha picha, CHRONICLES

    Maelezo ya picha, Kutoka kushoto: Nshimiyimana Jean Baptiste, Niyonsenga Shadrack na Mutuyimana Jean Damascène

    Mwendesha mashitaka nchini Rwanda amependekeza kuwa waandishi wa habari watatu wa kituo cha televisheni cha Iwacu TV, inayotangaza kupitia mtandao wa You tube wafungwe kifungo cha miaka 22 na miezi mitano jela 5.

    Mutuyimana Jean Damascène, Nshimiyimana Jean Baptiste na Niyonsenga Shadrack wanashitakiwa baregwa makosa matati, ikiwemo kusababisha ghasia na hofu miongoni mwa umma.

    Makosa hayo ambayo yanaripotiwa na waendesha mashitaka kuwa ni ya chuki, yameripotiwa kutekelezwa kupitia taarifa ambazo walikuwa wakizitoa kupitia televisheni ya Iwacu ambayo walikuwa wakiifanyia kazi

    Wote wanakana mashitaka dhidi yao, wakisema walitenda kulingana na kazi zao za kiuandishi.

    Miongoni mwa mashitaka yanayowakumba ni pamoja na kutumia pichaambayo ni kinyume na uhalisia wake ambapo walitumia picha inayomuonesha Rais kagame wa Rwanda, Yoweri Museveni wa Uganda na mpinzani wa Rwanda Kayumba Nyamwasa wa chama cha upinzani RNC wakiwa pamoja.

    Waendesha mashitaka wanasema picha hiyo sio halisi kwani hawaelezei ni wapi waliwapiga picha wanaume hao watatu pamoja.

    Uamuzi wa kesi hiyo unatarajiwa kutolewa tarehe 15 Septemba mwaka huu.

  3. Kalidou Koulibaly ajiunga na Chelsea

    Koulibaly palicheza mechi 27 kwa ajili ya Napoli msimu uliopita na kufunga mabao matatu, na kusaidia ufungwaji wa magoli matatu

    Chelsea imesaini mkataba wamiaka minne na kiungo wa kati-nyuma Kalidou Koulibaly ambaye anatoka upande wa Serie A- klabu ya Napoli.

    Mchezaji huyu wa kimataifa wa Senegal mwenye umri wa miaka 31alijiunga na Napoli akitokea klabu ya Genk katika mwaka 2014 na amecheza michezo 317 katika Ligi ya Italia.

    Awaliwasiri katika Stamford Bridge kufuatia kuondoka kwa walinziAntonio Rudiger aliyeelekea Real Madrid na Andreas Christensen katika Barcelona, wote kwa uhamisho huru.

    "Ninafuraha kuwa hapa katika timu ya Chelsea," alisema Koulibaly.

    "Ni timu kubwa duniani na ndoto yangu imekuwa kila mara kucheza katika Primia Ligi.Chelsea ilikuja ya kwanza kunitafuta katika mwaka 2016 lakini hatukuweza kufanikiwa. Sasa walikuja kwangu na nikakubali kwasababu kusema kweli nilitaka sana kuja katika Primia Ligi kucheza nao.

    "Nilipozungumza na rafiki zangu wema Edou [Mendy] na Jorginho walilifanya chaguo langu kuwa rahisi zaidi.’’, alingeza Koulibaly.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  4. Tiwa Savage apata shahada ya udaktari

    University of Kent/Twitter

    Chanzo cha picha, University of Kent/Twitter

    Msanii wa muziki wa Afrobeats wa Nigeria , Tiwa Savage, amepewa shahada ya heshima ya udaktari kutoka Chuo kikuu alichosomea awalicha Kent nchini Uingereza.

    "Tiwa alisoma biashara katika Chuo kikuu cha Kent kabla ya kuanza kazi ya muziki- jambo ambalo linawakumbusha wahitimu wetu leo kufikia kiwa ngo cha kuwa nyota!. "Chuo kikuu kiliandika kwneye ujumbe wake wa na kulikana nao ‘’wanajivuna sana’’.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Tiwa- alianza kazi yake ya muziki akiimba kama muimbaji kwa ajili ya wasanii wengine.

    Alikuwa mwanamke wa kwanza kushinda tuzo ya mwanamiziki bora mwanamke wa Kiafrika katika Tuzo za MTV Europe za muziki wa ulaya mwaka 2018.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mwanamuziki wa Nigeria Tiwa Savage 'akwama' hotelini Kenya baada ya kutumbuiza hafla ya Redsan
    • Burna Boy na Tiwa Savage waapa kutofanya shoo zao Afrika Kusini
  5. Urusi na Ukraine: Mtoto wa miaka minne Liza aliuliwa katika shambulio la Urusi katika Vinnytsia

    IRINA DMITRIEVA

    Chanzo cha picha, IRINA DMITRIEVA

    Maelezo ya picha, Kiti cha cha kusukumwa cha Liza kikiwa nje ya jengo lililoporomoka la Jubilee tarehe 14 Julai.

    Kwenye nyasi mbele yalililokuwa jengo la jubilee lililoporomoka kimebaki kiti cha rangi ya waridi kilicholala kando kilichojaa damu.

    Kilikuwa mali ya mtoto mdogo wa kike anayeitwa Liza aliyekuwa na umri wa miaka minne

    Liza alikuwa miongoni mwa watoto watatu wadogo waliouawa Alhamisi wakati makombora ya Urusi yalipopiga katika kituo cha Vinnytsia.

    Mama yake Iryna Dmytriyeva, alijeruhiwa vibaya katika shambulio hilo.

    Watu ishirini na watatu wanafahamika kupoteza maisha yao na wengie wanane bado hawajulikani walipo. Makumi kadhaa wengine wamelazwa hospitalini.

    Muda mfupi kabla ya shambulio hilo, Iryna alikuwa ametuma kwenye mtandao video. Ni siku nzuri ya jua na Liza alikuwa anatabasamu, akisukuma kiti chake cha rangi ya waridi mbele yake, huku wakiongeakuhusu kwenda kumuangalia daktari wake wa wake wa maozezi ya kuongeza.

    IRINA DMITRIEVA

    Chanzo cha picha, IRINA DMITRIEVA

    Uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine: Mengi zaidi

    • MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  6. Urusi na Ukraine: Milipuko na moto mkubwa vinaripotiwa katika jimbo la Odessa

    Suspilne Odessa

    Chanzo cha picha, Suspilne Odessa

    Katika Odesa kuna moshi mkubwa unaopaa angani, kulingana na vyombo vya habari, roketi mbili zilipiga mji huo mapema leo asubuhi.

    Mashambulio katika Odessa yamethibitishwa na msemaji wautawa wa jeshi jimboi humo, Sergei Bratchuk, na mwakaili wa operesheni za kijeshi za "Kusini"

    Waokoaji wako katika eneo la tukio la moto. Hakuna taarifa rasmi kuhusu majeruhi kwa sasa.

    "Kulikuwa na mashambulio katika ghala la biashara na viwanda, kulikuwa na moto mkubwa. Namshukuru Mungu hakuna majeruhi. Na kuna kitu muhimu hapa nilishotaka kusema asubuhi hii: walinzi wa ghala walifuata kanuni za mienendo wakati wa uvamizi wa anga, na hililimeyaokoa maisha yao," alisema Bratchuk.

    Uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine: Mengi zaidi

    • MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  7. Urusi na Ukraine: Mashambulio ya makombora ya masafa ya Urusi yapiga Odessa na chuguev

    Mashambulio ya makombora ya masafa ya Urusi katika mji wa Chuguev uliopo katika jimbo la Kharkiv limeharibu shule, majengo na makazi kadhaa ya watu, limesema shirika la habari la Ukraine la UNIAN

    Watu watatu wameripotiwa kufariki na wengine wengi kujeruhiwa na kwa sasa wamelazwa hospitali, limeandika shirika hilo likinukuu mtawala wa jimbo hilo Oleg Sinegubov.

    Athari za shambulio la Chuguev

    Takriban watu watatu wameuawa katika Chuguev ambako Urusi imepiga kombora Jumamosi asubuhi kwa picha:

    State Emergency Service of Ukraine/Reuters

    Chanzo cha picha, State Emergency Service of Ukraine/Reuters

    Wakati huo huo Urusi idadi ya watu waliokufa kutokana na shambulio la Warusi la roketi katika mji wa wa Vinnitsa imepanda na kufikia hadi watu 24 leo asubuhi. Mtu mmoja aliyekuwa amelazwa kutokana na shambulio hilo amefariki kutokana na majeraha ya kuungua, amsema mtawala wa jimbo, Sergei Borzov.

    Jumla ya watu waliofariki hadi sasa ni 24, huku wengine 68 waliojeruhiwa wakiendelea kuuguza majeraha, wakiwemo watoto wanne.

    Uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine: Mengi zaidi

    • MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  8. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mabashara ya leo tarehe 16.07.2022