Wanajeshi walinda amani wa Tanzania wajeruhiwa katika mapigano na M23 DRC
Jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo, FARDC, limetangaza kuwa wanajeshi Tanzania wanaohudumu katika kikosi cha walinda amani cha Umoja wa Mataifa MONUSCO wamejeruhiwa wakati wapiganaji wa M23 waliposhambulia ngome yao iliyopo Rutshuru.
Moja kwa moja
Habari za hivi punde, Waingereza wawili na Mmorocco waliokamatwa na jeshi la Urusi wahukumiwa kifo
Chanzo cha picha, Telegram
Maelezo ya picha, Aiden Aslin (kushoto) na Shaun Pinner (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na raia wa Morocco Saaudun Brahim.
Waingereza
wawili na mwanamume mmoja wa Morocco waliokamatwa na vikosi vya Urusi nchini
Ukraine wamehukumiwa kifo, shirika la habari linalomilikiwa na Urusi RIA Novosti
linaripoti.
Aiden Aslin,
28, kutoka Nottinghamshire, Shaun Pinner, 48, kutoka Bedfordshire, na mtu wa
tatu, raia wa Morocco Saaudun Brahim, walifikishwa katika mahakama ya Jamhuri
ya Watu wa Donetsk, ambayo inashikiliwa na waasi wanaoiunga mkono Urusi.
Mahakama hiyo
haitambuliki kimataifa.
Wanaripotiwa
kushtakiwa kwa kuwa mamluki.
Lakini
familia za wanaume wa Uingereza wanasema walikuwa katika jeshi la Ukraine.
Wanaume wote
wa Uingereza wanahudumia wanajeshi wa Ukraine na Uingereza imeweka wazi kuwa ni
wafungwa wa vita wanaostahili kinga na hawapaswi kufunguliwa mashtaka kwa
kushiriki katika mapigano.
Telegram RIA
News ilisema: ‘’Mahakama Kuu ya DPR ilitoa hukumu ya kwanza kwa mamluki-
Mwingereza Aiden Aslin na Sean Pinner na Mmorocco Saadun Brahim walihukumiwa
kifo, mwandishi wa RIA Novosti anaripoti kutoka chumba cha mahakama.’’
Morocco yaripoti kisa cha kwanza cha ugonjwa wa Monkeypox
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Dalili kubwa ya ugonjwa wa monkeypox ni upele mbaya na wenye matuta
Morocco imeripoti kisa chake cha kwanza cha ugonjwa wa monkeypox
kilichothibitishwa, nchi ya kwanza isiyo na ugonjwa huo barani Afrika kufanya
hivyo.
Mtu aliyeambukizwa ana historia ya kusafiri kwenda
Ufaransa na ametengwa, kulingana na Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia
Magonjwa (CDC).
Mwishoni mwa Mei, kituo cha CDC Afrika kilisema wale
ambao walipima virusi vya ugonjwa huo katika bara hilo hawakujulikana kuwa
walisafiri nje ya nchi kabla ya kuambukizwa.
Kunganisha usafiri hadi Ufaransa kuna hitaji uchunguzi wa
kina zaidi na mpangilio katika bara hilo.
Wakati wa mkutano wake wa kila wiki, Dk Ahmed Ogwell,
kaimu mkuu wa Afrika CDC, alisema kuwa ingawa ugonjwa wa monkeypox unaenea
kimataifa, uingiliaji kati wowote, na mipango yoyote ya kudhibiti virusi vya
ugonjwa huo, inapaswa kuanza barani Afrika.
‘’Mahali pa kuanzia chanjo inapaswa kuwa Afrika na sio
kwingineko,’’ alisema.
Wakazi wa Afrika Kusini waambiwa ‘wasihofu’ juu ya harufu ya mayai yaliyooza mjini
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Wakazi waliambiwa kwamba harufu mbaya labda ni tukio la muda ‘mfupi.’
Mamlaka
katika mji wa Johannesburg nchini Afrika Kusini imewaambia wakazi wasiwe na
hofu kuhusu harufu mbaya ambayo imekuwa ikienea katika baadhi ya maeneo katika
siku chache zilizopita.
Harufu mbaya
inayofananishwa na mayai yaliyooza, imechunguzwa na ripoti ikawasilishwa, diwani
wa Johannesburg Michael Sun, ilituma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter ambaye
pia anawakilisha Idara ya Mazingira na Huduma za Miundombinu ya eneo hilo
(EISD) kwenye kamati ya meya.
‘Harufu hiyo
ilienea katika jiji lote lakini hilo halijumuishi uwezekano wa chanzo kuwa mjini
Johannesburg,’’ tovuti ya The Citizen ya Afrika Kusini inamnukuu akisema.
‘’Katika
hatua hii ninawaomba watu wa Johannesburg wasiwe na hofu. Ilihitimishwa na
wachunguzi wa EISD kwamba jiji linaweza kushughulika na chanzo cha uchafuzi wa
mazingira,’’ nukuu iliendelea.
Bw Sun pia
alisema harufu mbaya huenda ni tukio la ‘’muda mfupi’’ kulingana na hali ya
hewa na ‘’kwamba ubora wa hewa huko Johannesburg unasalia katika viwango
vinavyokubalika.’’
Watu
mtandaoni wamekuwa wakilalamika sana kuhusu harufu hiyo, wakiita ‘’mbaya sana’’,
na ya ‘’ajabu’’.
Habari za hivi punde, Urusi kuidhibiti miji ya Donbas na Lohansk hivi karibuni - Mjumbe wa Urusi UN
Urusi itaidhibiti maeneo ya Donetsk na Luhansk nchini
Ukraine hivi karibuni, balozi wa Moscow wa Umoja wa Mataifa Vassily Nebenzia
ameambia kipindi cha Hardtalk cha BBC.
Kama tulivyoripoti hapo awali, anasema Urusi inapiga
hatua katika kanda hizo mbili, ambazo zinajumuisha Donbas.
Maelezo ya picha, Mfumo wa hali ya juu wa ufyatuzi wa maroketi aina ya M142
Mapigano yameongezeka
huko Severodonetsk na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema vita katika
mji huo vitaamua mustakabali wa eneo la Donbas.
Serhiy
Haidai, gavana wa eneo la Luhansk, alisema ikiwa nchi za Magharibi zitatoa
silaha za masafa marefu, Ukraine itakuwa na nguvu inayohitaji kurudisha nyuma
vikosi vya Urusi.
Alisema
ikiwa Ukraine itapata silaha za masafa marefu za Magharibi, Urusi ‘itapoteza
kwa Magharibi, na watetezi wetu wataweza kusafisha Severodonetsk katika siku
mbili hadi tatu’.
Haidai
aliongeza kuwa ‘kimya huko Severodonetsk hudumu tu wakati bunduki zinapakiwa
tena’ na uhamishaji kutoka jiji ‘bado hauwezekani.’
Maelezo ya picha, Mavuno huko Zaporizhzhia: Ukraine ni muuzaji mkuu wa nafaka barani Afrika na Mashariki ya Kati
Tumekuwa tukiripoti kuhusu mgogoro wa nafaka
uliosababishwa na vita nchini Ukraine katika siku chache zilizopita, ikiwa ni
pamoja na madai kwamba Urusi imekuwa ikiiba - na kuuza nje - baadhi ya bidhaa.
Moscow imekanusha madai hayo, lakini tatizo ni kwamba
yalitoka kwa maafisa walioteuliwa na Urusi katika eneo la kusini mwa Ukraine
linalokaliwa kwa mabavu.
Hii ni juu ya madai - ambayo BBC haijaweza kuyathibitisha
- na maafisa wa Ukraine ambao wameishutumu Urusi kwa kuiba takriban tani 600,000
za nafaka zake na kuuza nje baadhi yake.
Yevgeny Balitsky, anayesimamia maeneo yanayoshikiliwa na
Urusi katika eneo la Zaporizhzhia nchini Ukraine, alisema nafaka zimeondoka
eneo hilo kwa treni za mizigo zikielekea Crimea - ambayo Urusi iliiteka mwaka
2014 - na, kutoka huko, Mashariki ya Kati.
Maelezo ya picha, Majengo yaliyoharibiwa huko Mariupol yanaondolewa na Warusi wanaokalia eneo
Mamia ya
miili imepatikana kwenye vifusi vya majengo yaliyoharibiwa huko Mariupol,
kulingana na mshauri wa meya wa jiji hilo.
Petro
Andryushchenko alizungumza kwenye ujumbe wa Telegramu kuhusu ‘’msafara usioisha
wa vifo’’ katika jiji la bandari linalokaliwa, ambapo miili kati ya 50 na 100
kwa kila eneo la orofa inachukuliwa kutoka chini ya vifusi na kusafirishwa hadi
kwenye vyumba vya kuhifadhia maiti au - kulingana na mahali miili hiyo iko. -
kutupa taka.
Katika
chapisho hilo, lililochapishwa jana, alisema majengo takriban thuluthi mbili yamekaguliwa
na wanajeshi waliovamia hadi sasa.
Mwezi
uliopita, mkuu wa Jamhuri ya Watu wa Donetsk kama inavyojiita alisema kuwa 60%
ya majengo huko Mariupol yameharibiwa, ambayo 20% yao hayawezi kujengwa tena.
Lakini
katika chapisho la kufuatilia asubuhi ya leo, Andryuschenko anasema utafutaji
katika wilaya ya Ukingo wa Kushoto imesitishwa, akisema: ‘’Wavamizi hatimaye wameanza
kubomoa majumba na kukataa kutafuta miili ya waliouawa chini ya vifusi.’’
Anasema haijajulikana kamwe ni wakazi wangapi wa Mariupol
walikufa na bado wako chini ya vifusi - na watazikwa pamoja na takataka.
Nigeria sasa yathibitisha watu 40 walifariki katika shambulio la kanisa Nigeria
Chanzo cha picha, AFP
Takriban watu 40 waliuawa katika shambulio la Jumapili huko Owo katika jimbo la Ondo nchini Nigeria, gavana wa eneo Oluwarotimi Akeredolu sasa anasema.
Hapo awali mamlaka ilikuwa imesema watu 22 walikufa.
Katika taarifa yake, gavana huyo alisema kuwa watu 61 kwa sasa wamelazwa katika hospitali za karibu kwa matibabu na 26 wameruhusiwa.
Kulikuwa na watu 127 kanisani wakati shambulio hilo lilipotokea, alisema.
Aliongeza kuwa serikali itaanzisha uwanja wa kumbukumbu kuwakumbuka wahasiriwa wa shambulio hilo.
Ukaguzi wa Kenya wapata watu 250,000 waliofariki kwenye sajili ya wapiga kura
Chanzo cha picha, AFP
Tume ya Huru ya Uchaguzi Mipaka nchini Kenya (IEBC) inasema ukaguzi unaoendelea wa daftari la wapiga kura umepata majina ya karibu wapiga kura 250,000waliofariki kwenye sajili hiyo.
Takriban wapiga kura nusu milioni walipatikana kuwa na rekodi mbili na zaidi ya watu 226,000 walisajiliwa kwa kutumia stakabadhi ambazo si zao.
Wengine walikuwa wamejiandikisha na hati batili,
Kwenye taarifa tume hiyo ya imesema hitilafu hizo zinazoathiri zaidi ya watu milioni moja.
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alisema kutokana na hilo "utekelezaji wa matokeo ya awali ya ukaguzi" tume itachelewa kuidhinisha sajili ya mwisho ya wapiga kura..
Awali tume hiyo ilisema ingechapisha sajili ya wapiga kura kabla ya Juni 9 lakini imesogeza mbele mpango huo hadi Juni 20 inapojaribu kushughulikia matokeo ya KPMG, kampuni iliyopewa kandarasi ya kufanya ukaguzi huo.
Hitilafu ya uchaguzi katika chaguzi zilizopita nchini Kenya yamesababisha ghasia mbaya.
Uchaguzi wa mwaka huu utafanyika tarehe 9 Agosti.
Wagombea wanne wa urais wameidhinishwa kushiriki uchaguzi huo - David Mwaure, George Wajackoyah, Raila Odinga na William Ruto.
Somalia: Usalama waimarishwa huku rais akitarajiwa kuapishwa
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Rais Hassan Sheikh Mohamud (kushoto) alichaguliwa tarehe 15 Mei
Hali
ya usalama imeimarishwa katika mji mkuu wa Somalia na maeneo yanayozingira Uwanja
wa ndege wa Aden Adde , kabla ya kuapishwa kwa Rais wa Somalia Hassan Sheikh
Mohamud siku ya Alhamisi.
Barabara kuu mjini Mogadishu zimefungwa Jumatano huku polisi
wakisambazwa kwa wingi na magari ya kijeshi yameoneka mitaani yakielekea katika
kasri la rais.
Mji ulikuwa chini ya amri ya kutotoka nje usiku.
Viongozi wa Ethiopia, Kenya na Djibouti wanatarajiw akuhudhuria sherehe za
kuapishwa kwa Rais Hassan Sheikh Mohamud.
Kiongozi wa Djibouti Ismail Omar Guelleh na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta – ambaye uhusiano wa serikali
yake na Somalia uliingia dosari wakati wa utawala wa rais anayeondoka
madarakani Mohamed Abdullahi Farmajo – sasa anatarajia kurejesha uhusiano mpya
na utawala mpya wa Somalia.
Mshambuliaji wa Arsenal Lacazette ajiunga na Lyon
Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambulizi wa Arsenal Alexandre Lacazette amesajiliwa tena Lyon kwa uhamisho wa bila malipo - miaka mitano baada ya kuondoka na kujiunga na The Gunners kwa rekodi ya klabu wakati huo ya £46.5m.
Lacazette anarejea katika klabu hiyo ya Ufaransa kwa mkataba wa miaka mitatu hadi Juni 2025.
Mshambuliaji huyo wa Ufaransa alifunga mabao 54 katika mechi 158 za Ligi ya Primia akiwa na Arsenal na kusaidia The Gunners kushinda fainali ya Kombe la FA 2020.
Akizungumza na Canal Plus mwezi Aprili, Lacazette alisema "hajawahi kukata mawasiliano" na klabu ya nyumbani ya Lyon.
Lyon walisema "walijivunia sana na wana furaha sana" kutangaza kurejea kwa Lacazette katika klabu aliyojiunga nayo akiwa na umri wa miaka 12, na kuongeza kuwa mkataba "umekuwa kipaumbele cha klabu kwa miezi kadhaa".
Lacazette, 31, alipanda timu za vijana huko Lyon na kufunga mabao 129 katika mechi 275 katika mashindano yote baada ya kuingia kwenye kikosi cha kwanza katika kampeni za 2009-10.
Alisajiliwa na Arsene Wenger mwaka wa 2017 kwa mkataba huo - hadi £52.6m na nyongeza - kupita £42.4m Arsenal ililipa Real Madrid kwa Mesut Ozil mwaka 2013.
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Arsene Wenger alikuwa mkufunzi wa Arsenal wakati Alexandre Lacazette aliposajiliwa 2017
Mtume Mohammad: Al-Qaeda yazungumza kwa mara ya kwanza kuhusu kutusiwa Mtume India
Chanzo cha picha, NUPURSHARMABJP
Kikundi cha Al-Qaeda katika
Asia Kusini kimetishia kufanya mashambulio dhidi ya India na kupiga mabomu.
Kikundi hicho kimesema kitamlipua au kumuua yeyote anayemtusi Mtume Mohammad.
Al-Qaeda imetoa tisho hilo kujibu matamshi yenye utata
yaliyotolewa namsemaji wa zamani wa
chama tawala cha India Bharatiya Janata
Party (BJP) Bi Nupur Sharma na maafisa
wengine wa ngazi ya juu kumuhusu Mtume Muhammad.
Taarifa ya Al-Qaeda
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Osama bin Laden (kushoto) na Ayman Al-Zawahiri
Al-Qaeda imetoa taarifa yake katika lugha za Urdu na Kiingereza, ambayo imetumwa kwenye intaneti, pamoja na mitandao ya kijamii kama vile , RocketChat and ChirpWire.
Taarifa hiyo imewalenga watu wanaomtusi Mtume Mohammad na mke wake Aisha waliozungumza kwenye televisheni ya India.
Imeandikwa : "Tutawauwa wale wanaozungumza dhidi yao, kama vile kuwatusi, hususan magaidi wanaounga mkono Wahindu wanaotawala India. Tutawaonesha kuwa wale ‘’wanaomtukana Mtume Mohammad hawatawahi kuonyeshwa " huruma. "Hawapaswi kutukanwa, wanaofanya hivyo watashugulikiwa vibaya. Mwisho wa ugaidi katika Mumbai, Delhi, Uttar Pradeshna Gujarat ni dhahiri. Hawatakuwa salama katika nyumba zao."
Kikundi hicho kimejaribu kujieleza kama Waislam wanaoishi nchini India na walinzi wa Uislamu.
Unaweza pia kusoma:
Mtume Muhammad: Mfahamu mwanamke wa India aliyemtusi Mtume Muhammad
Nabii Muhammad: Putin atuma ujumbe kwa India baada ya kumtusi Mtume Mohammad
Wanajeshi walinda amani wa Tanzania wajeruhiwa katika mapigano na M23 DRC
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Wanajeshi wa MONUSCO walipambana na M23 mwezi uliopita
Jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasi
ya Congo, FARDC, limetangaza kuwa wanajeshi watatu
wa Tanzania wanaohudumu katika kikosi cha walinda amani cha Umoja wa Mataifa MONUSCO
wamejeruhiwa wakati wapiganaji wa M23 waliposhambulia ngome yao iliyopo Rutshuru.
MONUSCO imethibitisha kuwa
wanajeshi wake watatu wamejeruhiwa na kupelekwa kutibiwa katika hospitali ya
mjini Goma uliopo mashariki. Katika tangazo hilo jeshi la serikali ya Congo
limesema mmoja wa wanajeshi hao amejeruhiwa vibaya.
Kundi la M23 linasema kuwa
majeshi ya FARDC na MONUSCO ndio waliokuwa wa kwanza kufanya mashambulizi dhidi yao katika ngome yao iliyopo katika eneo la Jomba
Jumatatu.
Hii inakuja wakati mapigano
yakiendelea kwa siku ya nne mfulurizo kati ya pande hizo yaliyoibuka baada ya mapigano
hayo kusitishwa kwa muda wa wiki mmoja-
mapigano yanayoendelea katika eneo la Rutshuru katika eneo la Kivu ya Kaskazini.
MONUSCO ilitangaza kuwa ipo
katika mapigano ikilisaidia jeshi la Congo, FARDC linalopigana na wapiganaji wa M23.
Tanzania ina wanajeshi zaidi ya 800 katika kikosi cha MONUSCO kinachohudumu Mashariki mwa
DRC.
Katika taarifa yake iliyotolewa Jumatano usiku,
jeshi la DRC, FARDC linaishutumu Rwanda kutuma kikosi chake maalum
cha wanajeshi 500 kuwasaidia wapiganaji
wa M23, likisema kuwa walikuja wakiwa
wamevalia mavazi yenye rangi ya kijani kibichi na nyeusi.
Serikali ya Rwanda kwa upande wake imekuwa ikikana mara kwa mara kuwa inawasaidia M23, ikisisitiza kuwa tatizo
lao liko ndani ya nchi yao wenyewe ya
DRC.
Kikundi cha M23 Jumatano pia kilitoa
tangazo kikiishutumu serikali kwa ‘’kuchagua njia ya vita’’, kwa vikosi vyake
kushirikiana na wanajeshi wa MONUSCO na
wapiganaji wa kundi linaloshutumiwa na Rwanda kufanya mauaji ya kimbari ya
mwaka 1994 la FDLR kuwashambulia.
Tangazo hil la M23 linasema: “Kuchagua vita kwa serikali ya Congo badala ya kuchagua mazungumzo ya
amani, ni tatizo katika kurejesha amani katika mashariki mwa DRC”.
Wakati huo huo, jeshi la DRC- FARDC
limetangaza kuwa maazimio ya kikao cha wakuu wa majeshi kilichofanyika Goma ya kubuni kikosi maalumu cha kupigana na
makundi ya wanamgambo mashariki mwa
Congo, yatawasilishwa mbele ya kikao cha wataalamu wa masuala ya kijeshi na
wakuu wa majeshi kitakayofanyika kati ya
tarehe 15 na 19 mwezi huu mjini Nairobi Kenya, kabla ya kuidhinishwa na marais wa Kanda.
Unaweza pia kusoma:
Mzozo wa DRC na Rwanda : M23, majirani na bahati mbaya ya DRC
Rwanda: Hatuhusiki na mashambulizi ya M23 DRC
DR Congo: FARDC yaishtumu Rwanda kwa kuisaidia M23
Bondia wa Afrika Kusini Simiso Buthelezi afariki katika pambano la ndondi
Bondia wa Afrika Kusini Simiso Buthelezi amefariki dunia baada ya kuvuja damu kwenye ubongo kufuatia pambano la ndondi lililofanyika mwishoni mwa juma mjini Durban.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alipambana na mwenzake Siphesihle Mntungwa kuwania taji la WBF All Africa uzani mwepesi siku ya Jumapili, lakini pambano hilo la raundi 10 lilisitishwa na mwamuzi baada ya Buthelezi kuonekana kuwa kivuli cha mpinzani asiyeonekana.
Picha za pambano hilo zilimuonyesha Mntungwa akianguka kupitia kamba na kisha, baada ya pambano hilo kuanza tena, Buthelezi alisonga mbele kuelekea kwenye kona tupu ambapo alianza kupiga ngumi.
Mntungwa alitangazwa mshindi na baadaye Buthelezi alianguka na kukimbizwa hospitalini.
Aliwekwa katika hali ya kukosa fahamu baada ya kugundulika alikuwa anavuja damu kwenye ubongo.
Shirikisho la mchezo wa ndondi Afrika Kusini (BSA) lilithibitisha kuwa Buthelezi alifariki Jumanne jioni katika taarifa iliyotolewa kwa pamoja na familia ya bondia huyo.
Buthelezi alitambuliwa kama "bondia mkubwa ambaye alikuwa mfano mzuri nje na ndani ya ulingo".
BSA pia ilisema itafanya ukaguzi huru wa matibabu wa tukio hilo.
"Katika hospitali Bw Buthelezi alipewa huduma bora zaidi lakini hata hivyo alifariki dunia," taarifa hiyo ilisema.
Times: Vikosi vya NATO vinafanya zoezi kubwa zaidi la ulinzi wa anga
Chanzo cha picha, EPA
Maelfu ya wanajeshi wa NATO wanashiriki katika zoezi kubwa kuwahi kutokea la kujaribu mifumo yao ya ulinzi wa anga na makombora huku kukiwa na hofu kwamba vita vya Ukraine vinaweza kuenea katika maeneo mengine, linaandika gazeti la Uingereza Times.
Wakati ndege, zikichukua nafasi ya adui ndani ya mfumo wa mazoezi ya kijeshi, zilipokuwa zikiruka juu ya Poland na nchi za Baltic, mawaziri wa ulinzi wa NATO walijadili hali ya Ukraine huko Iceland.
Akizungumza huko Reykjavik, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iceland Thordis Gilfadottir aliwaambia wenzake kutoka nchi za Nordic, ikiwa ni pamoja na Uingereza, kwamba wanapaswa kuwa tayari kwa hali mbaya zaidi inapokuja suala la Urusi.
Wanajeshi 3,000 wa NATO kutoka mataifa 17 Washirika wanashiriki katika zoezi la Urithi wa Ramstein nchini Poland, Lithuania, Latvia na Estonia kwa kutumia ndege, mifumo ya ulinzi wa makombora na mifumo ya vita vya kielektroniki.
"Tishio la uvamizi wa kijeshi wa moja kwa moja dhidi ya nchi ya NATO haliwezi kupuuzwa tena," alisema.
Jumla ya ndege 50 za kivita na ndege nyingine za kivita ziliruka kutoka kote Ulaya, na mifumo 17 ya ulinzi wa anga na makombora ya ardhini inahusika katika zoezi hilo.
Mapigano ya Severodonetsk yataamua matokeo ya vita mashariki mwa Ukraine- Zelensky
Rais wa Ukraine
Volodymyr Zelensky amesema kuwa mapigano katika mji wa Severodonetsk huenda yakaamua
matokeo ya vita mashariki mwa nchi hiyo.
"Kwa kila
hali, hatima ya Donbas inaamuliwa huko," alisema wakati mapigano
yakiendelea katika ukanda wa viwanda na vikosi vya Urusi na vile vya waasi wanaotaka
kujitenga.
Alisema
wanajeshi wake wamewapatia hasara hasara kubwa kwa vikosi vya adui.
Lakini vikosi
vya Ukraine vimerudishwa nyuma hadi viungani, kulingana na afisa mkuu wa jimbo
la Ukraine.
Serhiy Haidai, gavana wa jimbo la Luhansk (ambalo linajumuisha Donbas
na eneo Donetsk), amesema vikosi maalum vimerejea nyuma baada ya Urusi "kuanza
kushambulia eneo hilo kwa makombora ya angani".
"Vikosi [vyetu] sasa vimechukua tena udhibiti viungani mwa
mji," aliambia vyombo vya habari vya ndani.
"Lakini mapigano bado yanaendelea, [vikosi]vyetu vinalinda Severodonetsk."
"Ni vigumu kusema kuwa Warusi wameudhibiti kabisa mji,"
aliongeza.
Karibu raia 15,000 walisalia Severodonetsk na katika mji wa karibu
wa Lysychansk, gavana alisema.
Unaweza pia kusoma
YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Alhamisi 09.06.2022.