Kombora jipya:Urusi yatangaza kufanyia majaribio kombora jipya la masafa marefu
Rais Vladimir Putin amesisitiza kuwa Urusi itafikia malengo yake ya kijeshi katika eneo la Donbas mashariki mwa Ukraine ambayo, anasema, yatawaruhusu watu kuendelea na maisha yao ya kawaida.
Moja kwa moja
Kombora jipya:Urusi yatangaza kufanyia majaribio kombora jipya la masafa marefu
Chanzo cha picha, Getty Images
Urusi
inasema imefanya majaribio ya kombora lake jipya la masafa marefu la Sarmat.
Rais
Vladimir Putin alisema majaribio hayo sasa yatazipa cha kufikiria nchi
ambazozinajaribu kutishia Urusi.
Alioneshwa
kwenye runinga akifahamishwa na jeshi kwamba kombora hilo
lilirushwa kutoka Plesetsk kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo na kulenga shabaha
kwenye rasi ya Kamchatka mashariki ya mbali ya Urusi.
Putin: Maisha yatakuwa bora
Chanzo cha picha, AFP
Rais
Vladimir Putin amesisitiza kuwa Urusi itafikia malengo yake ya kijeshi katika
eneo la Donbas mashariki mwa Ukraine ambayo, anasema, yatawaruhusu watu
kuendelea na maisha yao ya kawaida.
Akizungumza
katika mkutano katika Ikulu ya Kremlin unaolenga kuitangaza Urusi kama nchi
yenye fursa, Putin alisema Moscow imelazimika kuanzisha "operesheni ya
kijeshi" nchini Ukraine kwa sababu ya "janga" linalofanyika
Donbas.
"Nilisema
mwanzoni kabisa - madhumuni ya operesheni hii ni kusaidia watu wetu wanaoishi
Donbas," alisema.
Akihutubia
msichana ambaye alijiunga na mkutano kutoka Sevastopol huko Crimea, ambao Urusi
ilitwaa kutoka Ukraine mnamo 2014, alisema: "Tutachukua hatua mara kwa
mara na kuhakikisha kuwa maisha ya huko yatakuwa ya kawaida, yatabadilika na
kuwa bora - kama ilivyotokea’
Putin
hutumia mara kwa mara kumbukumbu ya kunyakuliwa kwa Crimea kuangazia upendo wa
nchi hiyo.
Mahakama ya Rwanda yamhukumu kifungo raia wa China aliyewachapa wafanyakazi viboko
Chanzo cha picha, Social media
Mahakama nchini Rwanda imemhukumu raia wa China kwa mateso baada ya video kumuonesha akiwachapa wanaume waliokuwa wamefungwa kwenye mti.
Mahakama siku ya Jumanne ilimhukumu Sun Shujun kifungo cha miaka 20 jela, mwandishi wa habari ambaye alihudhuria mahakamani aliiambia BBC.
Mwanaume mmoja raia wa Rwanda anayesemekana kuwa mfanyakazi wake pia alihukumiwa kifungo cha miaka 12 jela kwa kusaidia kutekeleza uhalifu huo.
Waathiriwa hao wanaripotiwa kuwa wafanyakazi wa zamani katika mgodi unaoendeshwa na Bw Shujun katika wilaya ya Rutsiro na ambao wanadaiwa kuhusishwa na wizi.
Bw Shujun alisema awali alikuwa amewaonya wezi baada ya mali zake kuibiwa mara kwa mara.
Mnamo Agosti mwaka 2021, video hiyo ya dakika tatu ilisambaa nchini Rwanda na kusababisha kukamatwa kwa Bw Shujun - ambaye aliachiliwa kwa dhamana baadaye.
Video hiyo ilichukuliwa na wafanyakazi wenye hasira na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
Ubalozi wa China mjini Kigali umelaani "vitendo visivyo halali" kwenye video hiyo, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.
Mashahidi waliiambia mahakama kuwa Bw Shujun alikuwa ameweka msalaba ambapo wale walioshukiwa kumuibia walifungwa na kuchapwa viboko.
Tarehe ya mwisho yapita kwa wanajeshi wa Ukraine huko Mariupol kujisalimisha
Chanzo cha picha, Getty Images
Tarehe ya mwisho ya iliyotolewa na Urusi kwa vikosi vya Ukraine huko Mariupol kuweka silaha chini imepita - bila dalili za kujisalimisha.
Ingawa jiji la bandari limezingirwa na vikosi vya Urusi, bado halijaanguka.
Lakini kamanda wa kikosi cha wanamaji aliye katika kiwanda cha chuma cha Azovstal - ngome ya mwisho ya Ukraine katika jiji la Azov - alisema kwenye video kwamba inawezekana kwamba "zimesalia siku au saa".
Meja Serhiy Volyna alisema: "Hii ndiyo hotuba yetu ya mwisho kwa ulimwengu. Huenda ikawa ni hotuba yetu ya mwisho."
Alisema wanajeshi wake hawatajisalimisha, lakini aliomba msaada wa kimataifa. Meja Volyna aliongeza kuwa wanajeshi 500 waliojeruhiwa na mamia ya wanawake na watoto walikuwa kwenye hifadhi kando yao.
Naibu Waziri Mkuu wa Ukraine Iryna Vereshchuk alisema inataka kuwahamisha raia kupitia njia za kibinadamu kwa wanawake, watoto na wazee. Lakini bado hakuna neno kutoka kwa Kremlin kuhusu hili.
Karibu Polisi 2,000 wa Kenya 'wana matatizo ya afya ya akili' kuhudumu
Chanzo cha picha, AFP
Takriban maafisa 2,000 wa polisi wa Kenya hawana uwezo wa kiakili kufanya kazi yao, mkuu wa huduma ya kitaifa ya polisi nchini anasema.
Inspekta Jenerali Hilary Mutyambai amesema hayo leo katika kongamano la maaskofu na makasisi wakuu akiongeza kwamba wamebaini visa hivyo "vya kushangaza" baada ya kuwafanyia uchunguzi wa kimatibabu maafisa wote wa polisi.
Kenya ina maafisa 100,000 wa polisi wanaofanya kazi chini ya Huduma ya Kitaifa ya Polisi.
Ufichuzi huo unakuja huku kukiwa na ongezeko la idadi ya visa vya maafisa kujitoa uhai ndani ya jeshi la polisi.
Bw Mutyambai amesema shughuli ya kuwaondoa kazini baadhi ya maafisa wa polisi walioathiriwa imeanza kwa kuzingatia umuhimu wa kuwa na polisi walio sawa kiakili.
"Zana yetu ya kazi ni bunduki, na risasi moja inapotolpigwa, madhara yake ni makubwa," alisema.
Hata hivyo alisema mchakato wa kuwaondoa maafisa hao kazini sio rahisi kwa sababu ya taratibu za kina zinazohusika.
Kumekuwa na wasiwasi unaoongezeka katika miaka ya hivi karibuni juu ya afya ya akili ya maafisa wa polisi na serikali imekuwa ikisonga kushughulikia suala hilo.
Bw Mutyambai alisema kwa sasa polisi wana bodi ya kitaalamu ya afya inayojumuisha washauri na madaktari wa akili walioidhinishwa na wizara ya afya kutoa huduma za afya ya akili.
Kituo cha televisheni cha NTV kimeshiriki video inayaoangazia baadhi ya maelezo ya mkuu wa polisi:
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje Mitandao ya kijamii inaweza beba matangazo
Mwisho wa YouTube ujumbe
Habari za hivi punde, 'Tumesalia na saa chache, tusaidieni' - Kamanda wa Ukraine Mariupol
Maelezo ya picha, Kamanda wa Ukraine Mariupol
Kamanda
mmoja wa jeshi la wanamaji nchini Ukraine akiwa miongoni mwa wanajeshi
waliozungukwa na Urusi katika mji wa Mariupol ametoa kanda ya videomapeme leo alfajiri akisema wanajeshi wenzake
wamesalia na saa chache.
Katika kanda
ya video iliotumwa kwa BBC na vyombo vingine vya habari , Meja jenerali Serhiy
Volyna alisema wanajeshi wake hawatasalimu amri , lakaini akatoa wito kwa
mataifa ya kigeni kutoa usaidizi kwa wanajeshi 500 waliojeruhiwa na mamia ya
wanawake na watoto wanaojificha nao katika kamapuni moja ya kuunda vyuma mjini
humo.
‘’Huu ndio
wito wetu wa mwisho duniani., huenda ukawa wetu wa mwisho kabisa. Inawezekana
kwamba tumesalia na saa chache’’, Meja Volyna alisema.
‘’Tunatoa
wito kwa viongozi kote duniani kutusaidia’’ aliongezea. ‘’Tunawaomba kuja
kutusaidia kuondoka na kwenda katika nhci nyingine’’.
Ndege ya RwandAir yapoteza mwelekeo baada ya kuteleza katika uwanja wa ndege wa Entebbe
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Shirika la ndege la Rwanda linasema abiria wote na wahudumu wa ndege wako salama
Ndege ya abiria iliteleza na kutoka kwenye njia yake ilipokuwa ikitua katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda Jumatano asubuhi.
Katika taarifa, RwandAir ilisema tukio hilo "lilitokana na hali mbaya ya hewa".
Abiria wote na wafanyakazi wa ndege walishuka salama bila majeraha yoyote, iliongeza.
Mdhibiti wa anga alisema njia mbadala ya ndege kurukia inafanya kazi kwa ajili ya ndege ndogo na nyepesi.
"Juhudi zote zinaendelea ili kuondoa ndege kwenye ukanda wa kuruka na kutua ndege ili njia kuu ya kuruka na kutua ndege irudi kutumika kikamilifu," ilisema.
Gazeti la Daily Monitor nchini Uganda, limeripoti kuwa abiria 20 kati ya 60 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo wameratibiwa kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa kwa mtoto wa Rais Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba.
Inaripoti kuwa tafrija ya kuzaliwa kwa Jenerali Kainerugaba ya kutimiza miaka 48 imepangiwa kufanyika Jumapili.
Jenerali Kainerugaba, ambaye pia ni kamanda wa majeshi ya nchi kavu, alichapisha ujumbe mtandaoni siku ya Jumatatu kwamba aliyekuwa Miss Rwanda atakuwa miongoni mwa wageni watakaohudhuria hafla hiyo.
Vijidudu vya mkojo huenda ni dalili ya saratani ya tezi dume
Chanzo cha picha, Getty Images
Wanasayansi wanasema wamegundua bakteria ya mkojo ambayo inahusishwa na saratani ya kibofu kali.
Ugunduzi huo unaweza kutoa njia mpya za kugundua na hata kuzuia uvimbe huu hatari, wataalam wanatumai.
Ni mapema sana kubaini ikiwa bakteria wanaweza kusababisha saratani, badala ya kuwa ishara ya kusaidia.
Kundi la watafiti Chuo Kikuu cha Anglia Mashariki inafanya uchunguzi zaidi mpango kubaini ikiwa kutibu maambukizi kwa dawa za antibiotiki kunaweza kuzuia uvimbe mbaya.
Maambukizi ya bakteria yanajulikana kuwa na sehemu katika maendeleo ya saratani nyingine - mdudu anayeitwa H. pylori anaweza kusababisha saratani ya tumbo, kwa mfano, na dozi ya tiba ya antibiotiki inaweza kuzuia hatari hiyo.
Saratani ya tezi dume sio hatari kwa maisha kila wakati - uvimbe fulani hukua polepole sana hivi kwamba haiwezi kusababisha matatizo yoyote.
Changamoto ni kuwatambua na kuwatibu haraka wanaume walio na uvimbe unaokuwa kwa kasi, na kuwaepusha wengine na matibabu yasiyo ya lazima.
Vipimo vinavyopatikana kwa sasa, ni kama vile uchunguzi wa damu wa PSA na biopsy, sio kila mara vinaweza kutabiri ni saratani zipi zitakuwa na madhara.
Soma zaidi:
Je, unafahamu nini juu ya saratani ya tezi dume?
Je ni wanaume gani katika hatari ya kupata tezi dume?
Urusi yatoa makataa mpya kwa wanajeshi wa Ukrane kujisalimisha huko Mariupol
Chanzo cha picha, Getty Images
Ikiwa unajiunga nasi muda huu haya ndio matukio ya hivi punde nchini Ukraine:
Wanajeshi wanaopingana wameendelea na makabiliano katika kwenye mstari wa mbele wa maili 300 (480km).
Wizara ya ulinzi ya Urusi imewapa wanajeshi wa Ukraine, ambao wamezuiliwa katika jengo la ujenzi wa chuma la Azovstal katika mji wa bandari wa Mariupol, uamuzi mpya, kuweka chini silaha zao ifikapo 1100 GMT siku ya Jumatano.
Hakuna hata mwanajeshi mmoja wa Ukraine aliyekubali ofa kama hiyo Jumanne, wizara ilisema katika taarifa yake.
Hakuna hata mwanajeshi mmoja wa Ukraine aliyekubali ofa kama hiyo Jumanne, wizara ilisema katika taarifa yake
Lakini Ukraine imefikia makubaliano ya awali na Urusi kuwahamisha raia, naibu Waziri Mkuu anasema.
Haya yamekuwa magumu kutekeleza katika vita hadi sasa
Mwakilishi wa Uingereza ameishutumu Urusi kwa "mashambulizi ya kiholela" katika mji wa bandari wa Mariupol
Katika kukabiliana na mashambulizi ya Moscow, wanajeshi wa Ukraine hadi sasa wameshikilia mstari huo, kwa mujibu wa Mkuu wa Jeshi la Wanajeshi wa Ukraine.
Hakuna hata mwanajeshi mmoja wa Ukraine aliyekubali ofa kama hiyo Jumanne, wizara ilisema katika taarifa yake.
Lakini Ukraine imefikia makubaliano ya awali na Urusi kuwahamisha raia, naibu.
Waziri Mkuu anasema. Haya yamekuwa magumu kutekeleza katika vita hadi sasa.
Mwakilishi wa Uingereza ameishutumu Urusi kwa "mashambulizi ya kiholela" katika mji wa bandari wa Mariupol
Katika kukabiliana na mashambulizi ya Moscow, wanajeshi wa Ukraine hadi sasa wameshikilia mstari huo, kwa mujibu wa Mkuu wa Jeshi la Wanajeshi wa Ukraine.
Damaris Muthee Mutua: Polisi wa Kenya waanzisha msako baada ya mwanariadha kuuawa
Chanzo cha picha, AFP
Polisi nchini Kenya wameanzisha msako baada ya mwili wa mwanariadha wa kike kupatikana ukiwa na majeraha ya kuchomwa kisu katika mji wa Iten, ambao ni maarufu kwa wakimbiaji wa mbio za masafa marefu.
Polisi wanasema wanamsaka mpenzi wake raia wa Ethiopia.
Damaris Muthee Mutua, 28, ni mzaliwa wa Kenya lakini alikuwa akishindania Bahrain.
Yeye ni mwanariadha wa pili wa kike kuuawa huko Iten katika mwaka mmoja.
Mwaka jana, Wakenya walishangazwa na mauaji ya mwanariadha wa Olimpiki Agnes Tirop.
Mumewe bado yuko kizuizini na anakanusha kuhusika na mauaji hayo.
Polisi wanasema mwili wa Mutua ulipatikana katika "hali mbaya" katika mji wa Iten, mkuu wa polisi wa eneo hilo Tom Makori aliambia shirika la habari la AFP.
Mpenzi wa Mutua pia alikuwa akifanya mazoezi katika eneo la Iten na huenda aliondoka nchini, polisi wanasema.
“Mshukiwa alimpigia simu rafiki yake ambaye walikuwa wakifanya mazoezi pamoja na kumuarifu kwamba amemuua mpenziwe na mwili ulikuwa ndani ya nyumba,” Bw Makori aliambia shirika la habari la Reuters.
Mutua aliiwakilisha Kenya kama mwanariadha mdogo lakini baadaye akabadili msimamo na kuamua kukimbilia Bahrain.
Rais Zelensky: 'Tungemaliza vita iwapo Ukraine ingekuwa na silaha bora'
Chanzo cha picha, Zelensky/Telegram
Maelezo ya picha, Rais Zelensky wa Ukraine
Katika hotuba
yake ya mara kwa mara katika kanda ya video
kwa taifa lake, rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema kwamba iwapo Ukraine
ilikuwa ikimiliki silaha bora ikilinganishwa na zile za Urusi , ingekuwa
imemaliza vita.
Rais
Zelensky alisema kwamba katika mahojiano yakena majadiliano na viongozi wa mataifa yaliopiga hatua kubwa kidemokrasia,
‘’sio haki kwa Ukraine kuendelea kuomba usaidizi wa kile ambacho washirika wake
wamekuwa wakihifadhi kwa miaka kadhaa’’.
Alisema
kwamba iwapo mataifa hayo yanamiliki silaha ambazo Ukraine inahitaji ni jukumu
lao kusaidia kulinda na kuokoa maisha ya
maelfu ya raia wa Ukraine.
Aliongezea
kwamba iwapo taifa lake lingefanikiwa kupata silaha hizo ambazo wameahidiwa
wiki zijazo, zingesaidia kuokoa maisha ya maelfu ya watu.
Rais
aliongezea kwamba uwezo wa mashambulizi ya Urusi katika maeneo ya Kharkiv,
Donbasna Dnipropetrovsk
umeongezekana hata kulenga makaazi ya
raia.
‘’Hatma ya makumi
ya maelfu ya wakaazi wa Mariupol ambao walipelekwa katika maeneo
yanayodhibitiwa na Urusi haijulikani’’, alisema Zelensky’’.
Hatua hii
inajiri huku wizara ya ulinzi ya Urusi ikitoa masharti mapya kwa wanajeshi wa
Ukraine waliozungukwa katika mji wa Mariupol kusalimu amri.
Ukraine: Silaha za kemikali ni nini na je Urusi inaweza kuzitumia?
Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Habari za hivi punde, Biden atangaza msaada mwingine wa kijeshi kwa Ukraine
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Joe Biden
Utawala wa
Biden unapanga kutangaza kifurushi kingine cha msaada wa kijeshi wenye thamani
ya $800m (£615m) kwa Ukraine, kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.
Alipoulizwa
Jumanne huko Portsmouth, New Hampshire, ikiwa angetuma silaha zaidi kwa
Ukraine, Rais Biden alijibu: "Ndiyo."
Ikulu ya White House wiki iliyopita ilitangaza
kutuma msaada wa kijeshi wa thamani ya $800m kwa Ukraine ambao utajumuisha
raundi 40,000 za mizinga na Howitters 18 (155mm.
Vita vya Ukraine: Kwa nini maneno ya 'kuropoka' ya Biden kuhusu Putin ni hatari sana
Mzozo wa Ukraine: Kwanini Biden ameamua kutopeleka jeshi Ukraine
Liverpool yaicharaza Manchester United 4-0 bila huruma
Liverpool waliwashinda Manchester United waliokata tamaa katika mchezo wa aibu uliozidi upande mmoja kwenye uwanja wa Anfield na kupanda hadi kileleni mwa Ligi ya Premia.
Manchester City huenda wakachukua nafasi yao kilelelni mwa ligi hiyo dhidi ya Brighton siku ya Jumatano , lakini mechi hii imeonesha jinsi timu hiyo ya Jurgen Kllop iko tayari kuwafukuza hadi siku ya mwisho ili kuweza kushinda mataji matatu mwaka huu.
Pia ilikuwa mechi ambayo ilionesha jukumu kubwa analotarajia mkufunzi mpya aliyeteuliwa kuinoa klabu hiyo Erik ten Hag huku United ikizidiwa katika kila safu ya mchezo .
United ilimkosa nyota wao Cristiano Ronaldo kufuatia kifo cha mtoto wake aliyezaliwa huku wafuasi wa timu zote mbili wakituma rambirambi zao katika dakika ya saba ya mechi.
Liverpool tayari ilikuwa kifua mbele wakati huo baada ya Luis Diaz kufunga pasi muruwa ya Mohammed Salah kabla ya mshambuliaji huyo wa Misri kumaliza njaa yake ya mabao katika mech inane kufuatia pasi ya Sadio Mane kunako dakika ya 22.
Mane alifuta matumaini yoyote ya Man United kwa kufunga bao kunako dakika ya 69 alipopata pasi nzuri kutoka kwa Diaz huku Salah akifunga goli la nne ikiwa imesalia dakika 5 za mchezo.
Baada ya mabao 5-0 katika uwanja wa Old Trafford mwezi Oktoba, Liverpool sasa ndio klabu ya kwanza kufunga magoli manane dhidi ya Manchester United katika msimu mmoja.
Manchester United vs Liverpool: Nani kuibuka mbabe?
Mafanikio mengi ya Urusi yazuiwa Donbas - Uingereza
Chanzo cha picha, Reuters
Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imetoa taarifa yake hivi karibuni kuhusu mapigano nchini Ukraine, ikiangazia hali ya mashariki mwa nchi hiyo.
Katika kurasa ya tweeter, MoD anasema:
The MoD anasema Ukraine ilijaribu mara kadhaa kuviondoa vikosi vya Urusi.
Mashambulizi ya makombora na mashambulizi ya Urusi kwenye udhibiti katika eneo la Donbas mashariki mwa Ukraine yanaendelea kuongezeka
Urusi bado inatatizwa na "changamoto za mazingira, vifaa na kiufundi" ambazo tayari zimeonekana katika vita - na vilevile upinzani "uliochochewa sana" kutoka kwa kuwatetea Waukraine.
Urusi inatumia "mashambulizi ya kiholela" katika mji wa bandari uliozingirwa wa Mariupol.
MoD anasema hii ilionyesha kutokuwa na uwezo wa Moscow kufikia malengo yake haraka kama wangependa.
Mariupol: Jinsi vikosi vya Ukraine vilivyojaribu kuuokoa mji huu muhimu
Je kombora la Neptune lililotumika kuiangamiza meli ya kivita ya Urusi ni kombora la aina gani?
Habari...Karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya kurasa wako wa BBC Swahili, leo ikiwa tarehe 20/04/2022