Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
'Tunataka kuishi, lakini majirani zetu wanataka kutuangamiza' - Zelensky
Rais wa Ukraine ahutubia bunge la Israel kwa njia ya matandao, kama sehemu ya juhudi za kutafuta uungwaji mkono kimataifa.
Moja kwa moja
Zelensky awianisha uvamizi wa Urusi na Vita Vikuu vya Pili vya Dunia
Rais Zelensky wa Ukraine amelinganisha uvamizi wa Urusi dhidi ya nchi yake na Vita Vikuu vya Pili Vya Dunia.
Anasema uvamizi huo "sio oparesheni ya kijeshi".
"Ni vita kamili inayolenga kuangamiza watu wetu, tkuangamiza watoto wetu, familia, utaifa, miji, uatamaduni na ka]ila kitu kinachowatambulisha kama Waukraine."
"Hiyo ndio sababu naweza kuwianisha historia. Mapambano yetu ya kuishi na Vita Vikuu vya pili vya Dunia."
Rais Zelensky pia alimnukuu marehemu Waziri Mkuu wa Israel Golda Meir, katika ujumbe wake wa video, na maneno "tunataka kuishi, lakini majirani zetu wanataka kutuuwa".
Bwana Zalensky alikuwa akitoa uwiano wa moja kwa moja kati ya Ukraine sasa na historia ya Israel inavyokabiliwa na uadui.
Wakati huo huo Rais Zelensky ametoa wito kwa Israel kuisaidia Ukraine kwa silaha na kuuiliza kuhoji kwanini haijaiwekea Urusi vikwazo.
Aliongeza kuwa IIsrael ina ulinzi bora wa anga duniani na kusema"kwa hakika mnaweza kuwasaidia watu wetu, kuokoa maisha ya Waukraine".
Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Vita vya Ukraine: Majasusi wa nchi za Magharibi wataka kuingia 'ndani ya kichwa cha Putin'
Kiongozi wa Urusi Vladimir Putin amenaswa katika ulimwengu uliofungiwa wa kujitengenezea mwenyewe, majasusi wa nchi za Magharibi wanaamini. Na hilo linawatia wasiwasi.Soma zaidi.
Papa awataka viongozi kukomesha 'vita hivi vya kuchukiza'
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis ametumia hotuba yake ya Jumapili katika Jiji la Vatican kusema mzozo wa Ukraine ulikuwa "mauaji ya kinyama" na kutoa wito kwa viongozi kukomesha "vita hivi vya kuchukiza".
"Uchokozi mkali dhidi ya Ukraine kwa bahati mbaya haupungui," Papa alisema kwa maelfu ya watu waliokuwa wamekusanyika katika uwanja wa St Peter's.
"Ni mauaji yasiyo na maana ambapo kila siku mauaji na ukatili unarudiwa," aliongeza.
Pia unaweza kusoma:
Matukio yanayojiri Ukraine kwa mukhtasari
Ikiwa ndio mwanzo unajiunga nasi,haya ndio matukio ya hivi punde kutokaUkraine:
- Naibu Waziri Mkuu wa Ukraine Olha Stefanishyna ameishutumu Urusi kwa "mauaji ya halaiki" na kudai kuwa "wanawake wamebakwa kwa saa kadhaa na kisha kuuawa"
- Maafisa katika mji uliozingirwa wa Mariupol kusini-mashariki mwa Ukraine wanadai kuwa maelfu ya wakazi wamesafirishwa hadi Urusi bila ridhaa yao.
- Huku hayo yakijiri, mamlaka huko Mariupol zinasema vikosi vya Urusi vimeshambulia shule iliyokuwa ikiwahifadhi watu 400, na kuharibu jengo hilo na kwamba watu kadhaa wamekwama chini ya vifusi.
- Jeshi la wanahewa la Urusi limesema kuwa limerusha kombora la hypersonic katika eneo linalolengwa na Ukraine kwa siku ya pili mfululizo
- Kwengineko, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema vikosi vya Urusi vimepiga "hatua chache" katika uvamizi huo na badala yake wamegeukia kwa kushambulia miji ya Ukraine "bila kujali"
- Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ameitaka China kulaani vikali uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, akieleza vita hivyo kuwa ni vita kati ya wema na uovu.
Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Ukraine yadai kuwaua wanajeshi 15,000 wa Urusi
Maafisa wa kijeshi wa Ukraine wamedai kuwa takriban wanajeshi 15,000 wa Urusi wameuawa tangu Rais Vladimir Putin alipoanzisha uvamizi wake zaidi ya wiki tatu zilizopita.
Katika sasisho lililotumwa kwenye ukurasa wa Facebook wa wafanyikazi wakuu wa Ukraine, maafisa walisema kuwa wanajeshi 14,700 wa Urusi wameuawa katika siku 25 za mapigano.
Taarifa hiyo pia ilidai kuwa kiasi kikubwa cha vifaa vya kijeshi vya Urusi vimeharibiwa katika mzozo huo, vikiwemo takriban vifaru 476, zaidi ya ndege 200 za kivita, helikopta na ndege zisizo na rubani na karibu wabeba silaha 1,487.
BBC haijafanikiwa kuthibitisha madai haya kibinafsi hili, ijapokuwa vyanzo vya Magharibi vinaamini kuwa Urusi imepata hasara kubwa na maafisa wa ulinzi wa Marekani wamekadiria kuwa takriban wanajeshi 7,000 wa Urusi wameuawa wakiwa vitani, huku wengine karibu 21,000 wakijeruhiwa.
Pia unaweza kusoma:
Urusi inasema makumi ya 'mamluki' waliuawa katika shambulio la kombora
Wizara ya ulinzi ya Urusi inasema umewaua makumi ya "mamluki" ikatika shambulio la kombora dhidi ya kituo cha mafunzo magharibi mwa Ukraine, shirika la habari la RIA linaloendeshwa na serikali limeripoti.
Maja Jenerali Igor Konashenkov, msemaji wa wizara hiyo, amesema zaidi ya wanajeshi 100 wa Ukraine na"mamluki wa kigeni" waliuawa baada ya "kombara la hali ya juu" kulipua kambi karibu na Ovruch mjini Zhytomyr Oblast.
"Makombora yetu yalilipua kambi ya vikosi maalu vya jeshi la Ukraine ambako mamluki wa kigeni waliowasili Ukraine wanaishi," Konashenkov alisema.
BBC haijafanikiwa kuthibitisha madai.
Vita vya Ukraine: Wakazi wa Mariupol wanapelekwa Urusi kwa nguvu
Maafisa wa mji wa Mariupol nchini Ukraine wanailaumu Urusi kwa kuwavusha mpaka wakazi wa mji huo na kuwaingiza Urusi bila ridhaa yao kwa wiki kadhaa zilizopita.
BBC haijathibitisha madai hayo – lakini mashuhuda kadhaa wameazungumzia visa hivyo.
Mafisa mmoja, Pyotr Andryuschenko ameambia gazeti la New York Times kwamba kati ya wakazi 4,000 na 4,500 wamepelekwa Tangarog, mji uliopo eneo la Rostov ambalo linapakana na Ukraine upande wa kusini - mashariki. Aliongeza kuwa walipelekwa huko bila pasipoti zao.
Mwanamume mmoja raia wa Ukkraine ameambia gazeti hilo kwamba jamaa zake watatu waliohamishwa kwa nguvu wamewasiliana naye.
“Sasa Warusi wanapita kwenye vyumba vya chini ya ardhi, na ikiwa kuna watu walioachwa huko, wanawapeleka kwa nguvu hadi Taganrog,” alisema Eduard Zarubin, daktari aliyeondoka jijini humo mapema wiki hii.
Urusi haijajibu madai hayo moja kwa moja, lakini wizara ya ulinzi siku ya Ijumaa iladai kuwa maelfu ya Waukraine waliomba "kuingia Urusi" na serikali inawasaidia.
Mariupol kwa sasa inakabiliwa na mapigano makali kati ya wanajeshi wa Urusi na Ukraine. Mji huo umeshambuliwa kwa mabomu kwa zaidi ya wiki mbili na maafisa wake wanakadiria karibu watu 2,400 wameuawa.
Ni vigumu kubaini. kinachoendelea mjini humo kwa sababu mawasiliano ya simu yamekatizwa, hakuna mafuta wa maji huku msaada wa chakula ukitolewa kwa mgao,
Ukraine inasema Urusi pia imesimamisha misafara ya misaada ya kibinadamu inayoingia mjini humo.
Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Maafisa wa Ukraine: Urusi ilishambulia shule iliyohifadhi watu 400
Baraza la jiji la Mariupol linasema kuwa vikosi vya Urusi vilishambulia kwa mabomu shule ambayo watu 400 walikuwa wakipata hifadhi siku ya Jumamosi.
Katika sasisho kwenye Telegraph, inasema jengo liliharibiwa na watu wako chini ya vifusi. Wanawake, watoto na wazee walikuwa shuleni, maafisa walisema.
Bado hakuna taarifa kuhusu majeruhi.
Mawasiliano na Mariupol ni magumu sana, na BBC imeshindwa kuthibitisha dai hilo mara moja.
Ugaidi wa Mariupol utasalia katika historia - Zelensky
Rais wa Ukrain, ambaye alitoa hituba ya video usiku wa manane ametoa tamko kuhusu mashambulizi la Urui dhidi ya jiji la Mariupol .
Rais Volodymyr Zelensky alilaani mashambulizi ya Urusi ya mara kwa mara dhidi ya Mariupol, mji wa bandari uliozingirwa na wanajeshi wa Urusi kusini-mashariki.
Alidai kuwa vikosi vya Urusi katika jiji hilo "vitaingia katika historia" kama kuwajibika kwa "uhalifu wa kivita".
"Kufanya hivi kwa jiji lenye amani, walichofanyia wakaaji, ni ugaidi ambao utakumbukwa kwa karne nyingi zijazo," alisema.
Kwa zaidi ya wiki mbili sasa, jiji hilo limeshuhudia mashambulizi ya mara kwa mara ya mabomu ambayo yamekata umeme, gesi, maji ya mfereji na vifaa vingine.
Mashambulizi ya Urusi yamegonga makazi ya raia, hospitali ya watoto na uzazi, na majengo kadhaa ya makazi. Siku ya Alhamisi, bomu lilianguka kwenye ukumbi wa michezo ambapo mamia ya watu walikuwa wamekimbilia.
Zaidi ya watu 2,400 wanasemekana kuuawa katika mji huo; kuna makaburi na miili ya watu wengi mitaani.
Vikosi vya Urusi vimeingia ndani zaidi ya jiji. Pamoja na makombora ya angani, pia sasa kuna ripoti za mapigano makali mitaani.
Siku ya Jumamosi, afisa mkuu wa ulinzi wa Uingereza aliiambia BBC kuwa Urusi inatumia mkakati wa ukatili na ulipizaji kisasi kushambulia Ukraine.
Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Luteni jenerali wa Urusi auawa nchini Ukraine: Jeshi la Ukraine ladai
Mwanajeshi wa Urusi aliuawa katika mji wa Chernobayevka nchini Ukraine baada ya shambulio la mizinga, alisema Mkuu wa Jeshi la Ukraine katika chapisho la Facebook Jumamosi.
Katika chapisho hiloilidaiwa Luteni Jenerali Andrei Mordvichev, kamanda wa Jeshi la 8 la Silaha za Pamoja la Wilaya ya Kijeshi ya Kusini ya Vikosi vya Wanajeshi wa Urusi amekufa.
Pia iliongeza kuwa mstari wa mbele wa vita haujabadilika sana katika masaa 24 iliyopita, lakini ilisema kuwa wanajeshi wa Ukraine wameweza kuharibu safu kadhaa na wanajeshi wa Urusi katika mkoa wa Mykolaiv na Sumy.
BBC haijaweza kuthibitisha madai haya kwa uhuru.
Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Jeshi la Ukraine : Russia inajaribu kujipanga upya na kukadiria hasara
Katika taarifa yake kila siku asubuhi kuhusu hali ya vita , jeshi la Ukraine linasema kuwa badala ya kuanzisha mashambulizi mapya, vikosi vya Urusi vililenga kwa kiasi kikubwa kukadiria hasara zao na kukarabati vifaa vilivyoharibika Jumamosi nzima.
Pia iliishutumu Urusi kwa "kuweka mazingira kwa makusudi kwa ajili ya mzozo wa kibinadamu" katika maeneo ambayo majeshi yake yalikuwa yanakalia, kwa kuzuia msafara wa misaada kufika Kherson jana usiku.
Katika chapisho la awali, jeshi lilidai kurejesha safu yake ya ulinzi kusini katika maeneo kadhaa, na kusema kuwa imefanikiwa kusitisha mashambulizi ya Urusi karibu na Izyum mashariki.
BBC haiwezi kuthibitisha madai haya kwa uhuru.
Matukio ya hivbi punde kutoka Ukraine kwa muhtasari
• Maafisa wa jiji la Mariupol wanasema maelfu ya wakaazi wamechukuliwa kwa nguvu na vikosi vya Urusi hadi miji ya Urusi wiki iliyopita - BBC bado haijathibitisha madai haya.
• Mariupol imekuwa chini ya mlipuko mkali wiki nzima na wenyeji huko wamebaki wamenaswa bila umeme, gesi au maji ya mfereji katika baadhi ya maeneo.
• Vikosi vya Urusi vimeingia katika mji wa kusini, ambapo meya aliiambia BBC kwamba mapigano ya mitaani pia yanazuia juhudi za kuwaokoa manusura waliokuwa wamekwama chini ya jumba la maonyesho ambalo lilipigwa makombora siku ya Alhamisi.
• Siku ya Jumamosi kombora la Urusi pia lilipiga kambi ya kijeshi ambako wanajeshi 200 walikuwa wamelala - katika kile kinachoaminika kuwa mojawapo ya mashambulizi mabaya zaidi ya roketi katika vita hivi.
• Waziri Mkuu wa Ukraine Zelensky alihimiza tena Urusi kujitolea kwa mazungumzo ya amani yenye maana
• Ukraine pia iliitaka China kuchukua msimamo dhidi ya uchokozi wa Urusi. Waziri Mkuu wa Uingereza vile vile alishinikiza Beijing.
• Lakini afisa mkuu wa serikali ya China anasema kuwa vikwazo vilivyowekwa na mataifa ya Magharibi dhidi ya Urusi vinazidi kuwa "vya kuchukiza"
• Zaidi ya raia milioni mbili wa Ukraine wamekimbilia Poland, kati ya wakimbizi wapatao milioni 3.3 kufikia sasa
• Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema takriban raia 847, wakiwemo watoto 64, wameuawa nchini Ukraine tangu uvamizi huo uanze, wengi wao wakiwa na makombora na mashambulizi ya anga.
Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Hali inawekwa kwa ajili ya mzozo hatari usiokuwa na mshindi kamili – Taasisi ya Marekani
Urusi inapiga hatua chache tu katika uvamizi wake wa Ukraine na mashambulizi yake ya awali, Taasisi ya Uchunguzi wa Vita imesema.
Taasisi hiyo yenye makao yake makuu nchini Marekani ilikamilisha tathmini juu ya ufanisi wa kampeni ya mapema ya Urusi.
Haya hapa baadhi ya matokeo muhimu ya taasisi ya utafiti:
- Masharti yanawekwa kwa ajili ya vita katika sehemu kubwa ya Ukraine kuwa mkwamo usio na mshindi ambao unaweza kudumu kwa wiki au miezi
- Kadiri hali inavyoendelea kwa muda mrefu, ndivyo inavyoweza kuwa mbaya zaidi Vikundi vidogo vya askari wa Kirusi vinalenga mapigano ya ndani, badala ya kuanzisha operesheni kubwa.
- Iwapo Mariupol itawaangukia Warusi, hakuna uwezekano wa kuwaachilia huru wanajeshi kwa ajili ya kampeni kubwa zaidi, kutokana na uharibifu mkubwa unaoletwa na watetezi wa Ukraine.
- Vikosi vya Urusi vina uwezekano wa kukamata Mariupol au kulazimisha jiji kusalimu amri ndani ya wiki zijazo.
- Huenda Warusi wameachana na mipango ya kuizingira Kyiv kutoka magharibi au kushambulia ili kuuteka mji huo kutoka magharibi katika siku za usoni.
- Badala yake kuna uwezekano wanatafuta kuweka masharti ya kupanuliwa kwa silaha na mashambulizi ya makombora ya Kyiv kwa kuhamia katika safu madhubuti ya mizinga ya kituo chake.
- Kuendelea na kupanuliwa msaada wa Ukraine na mataifa ya Magharibi itakuwa muhimu
Urusi imeshindwa kupata udhibiti wa anga ya Ukraine, Uingereza yasema
Urusi inashindwa kupata udhibiti wa anga ya Ukraine - mojawapo ya malengo makuu ya Moscow, wizara ya ulinzi ya Uingereza inasema.
Taarifa ya hivi punde ya kijasusi ya wizara hiyo inasema Urusi "imeshindwa kupata udhibiti wa anga na kwa kiasi kikubwa inategemea silaha za zilizozinduliwa kutoka anga ya Urusi.
"Kupata udhibiti wa anga lilikuwa mojawapo ya malengo makuu ya Urusi kwa siku za mwanzo za mzozo na kuendelea kwao kushindwa kufanya hivyo kumezuia kwa kiasi kikubwa maendeleo yao vitani ," wizara hiyo inasema.
Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Hujambo na karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Jumapili 20.03.2022.