Job Ndugai:Maoni mseto yatolewa kuhusu kujizulu kwake kama spika

Huku wengine wakimsifu kwa uamuzi huo ikizingatiwa kwamba tayari alikuwa chini ya shinikizo ,kunao waliokaribisha uamuzi wake wakionekana kufurahia alichokifanya Ndugai.

Moja kwa moja

  1. Na hadi hapo tumefika mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja leo.Hadi hapo kesho panapo majaaliwa

  2. Job Ndugai:Maoni mseto yatolewa kuhusu kujizulu kwake kama spika

    th

    Chanzo cha picha, Bunge/Tanzania

    Hatua ya Job Ndugai kujizulu imevutia mesto wa maoni kutoka kwa viongozi na Watanzania kupitia mitandao ya kijamii

    Huku wengine wakimsifu kwa uamuzi huo ikizingatiwa kwamba tayari alikuwa chini ya shinikizo ,kunao waliokaribisha uamuzi wake wakionekana kufurahia alichokifanya Ndugai.

    Sauti zilizosikika sana ni kutoka kwa viongozi wa vyama vya upinzani ambao walitoa maoni yao katika mitandao ya kijamii .Tundu Lissu wa Chadema amesema kwamba kujiuzulu kwa Ndugai kunaonyesha kwamba kuna mhimili mmoja tu wenye wa dola’usihojiwa wala kudhibitiwa’.

    Hata hivyo mbunge John Heche wa Chadema alisema haikufaa kufurahiwa kwamba Ndugai amejiuzulu kwa sababu ni hatua iliyosababishwa na mhimili mwingine kwa kiongozi wa bunge .

    Ruka X ujumbe, 1
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 1

    Ruka X ujumbe, 2
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 2

    Ruka X ujumbe, 3
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 3

    Ruka X ujumbe, 4
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 4

    Ruka X ujumbe, 5
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 5

    Ruka X ujumbe, 6
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 6

    Ruka X ujumbe, 7
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 7

    Ruka X ujumbe, 8
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 8

    Ndugai amejiuzulu wadhifa wake leo Alhamisi tarehe 6 Januari 2022.

    Kwa mujibu wa barua aliyomuandikia Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema uamuzi huo wa kuachia nafasi hiyo ameufanya kwa hiari.

    "Naomba kutoa taarifa kwa umma wa Watanzania kuwa leo Tarehe 06 Januari 2022 nimeandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiuzulu nafasi ya Spika wa bunge la Jamhuri .." imesema sehemu ya taarifa hiyo nakuongeza;

    "Pia nakala yangu hiyo ya kujiuzulu nimewasilisha kwa katibu wa Bunge kwa ajili ya hatua stahiki kwa mujibu wa katiba ya nchi na sheria nyingine" amesema Ndugai kwenye taarifa yake kwa umma.

  3. Afcon 2021: Mchezaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang apatikana na virusi vya Covid-19

    th

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Nahodha wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang amepimwa na kukutwa na virusi vya corona siku nne tu kabla ya mchezo wa kwanza wa nchi yake kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika.

    Mshambulizi huyo wa Arsenal na kiungo wa kati wa Nice Mario Lemina walirejesha vipimo vyao baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Yaounde nchini Cameroon.

    Kocha Msaidizi Anicet Yala pia alipatikana na Covid-19.

    Kocha wa Gabon Patrice Neveu aliiambia AFP kwamba watatu hao, ambao wote hawana dalili, wanajitenga katika vyumba vyao vya hoteli na wanasubiri matokeo ya vipimo vya PCR.

    Gabon watacheza mechi yao ya ufunguzi ya Kundi C dhidi ya Comoro siku ya Jumatatu, na mchezo wao wa pili wa kundi dhidi ya Ghana Ijumaa, 14 Januari.

    Aubameyang alitemwa na The Gunners na kuvuliwa unahodha na Premier League mwezi uliopita kwa sababu za kinidhamu.

    Wenyeji Cameroon watacheza katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Mataifa dhidi ya Burkina Faso Jumapili (16:00 GMT).

    Kwingineko Maneja wa Manchester city Pep Guardiola na mwenzake wa Burnley Sean Dyche watakosa mechi zao za raundi ya tatu ya Kombe la FA baada ya kukutwa na virusi vua corona .

  4. China kumteua mjumbe maalum katika Upembe wa Afrika

    th

    Chanzo cha picha, AFP

    China itamteua mjumbe maalum wa Pembe ya Afrika kusaidia kukabiliana na changamoto za usalama katika eneo hilo.

    Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi alitoa tangazo hilo siku ya Alhamisi wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika mji wa Mombasa nchini Kenya.

    "Tutaendelea kutekeleza jukumu kubwa zaidi kwa amani na utulivu katika eneo hili," Bw Wang alisema.

    Waziri huyo yuko katika ziara ya kutembelea nchi tatu za Afrika mashariki iliyoanzia Eritrea na kuhitimishwa katika kisiwa cha Comoro kilicho katika Bahari ya Hindi.

    Siku ya Jumatano, alilaani vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Eritrea, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikichukuliwa kuwa nchi iliyofeli na mataifa ya Magharibi. Marekani iliiwekea Eritrea vikwazo mwaka jana kutokana na kuhusika katika mzozo wa Ethiopia.

    Ziara ya waziri wa China katika eneo hilo inasadifiana na ziara ya mjumbe maalum wa Marekani katika Pembe ya Afrika, Jeffrey Feltman, ambaye anatatarajiwa kuwasili nchini Ethiopia siku ya Alhamisi kuzungumzia vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miezi 14 katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.

  5. Usafiri warejea kati ya Chokocho na Panza palikotokea msiba wa boti Pemba

    Safari kati ya Chokocho na Kisiwa kidogo Panza zimerejea baada ya kusitishwa kwa zoezi la uokoaji

    Mwandishi wetu Eagan Salla ametuandalia taarifa ifuatayo

    Maelezo ya video, Usafiri warejea kati ya Chokocho na Panza palikotokea msiba wa boti Pemba
  6. Watu kadhaa wauawa katika mapambano ya kumaliza ghasia Kazakhstan

    Wanajeshi

    Chanzo cha picha, Reuters

    Vikosi vya usalama nchini Kazakhstan vinasema kuwa vimewaua makumi ya waandamanaji wanaoipinga serikali katika operesheni ya kurejesha utulivu katika mji mkuu wa Almaty.

    Waliingia baada ya waandamanaji kujaribu kudhibiti vituo vya polisi mjini, msemaji wa polisi alisema.

    Wanajeshi 12 wa vikosi vya usalama wameuawa na wengine 353 kujeruhiwa katika machafuko hayo, yaliyosababishwa na kuongezeka maradufu kwa gharama ya gesi ya kupikia (LPG).

    Urusi inatuma wanajeshi kwa ombi la rais wa Kazakhstan.

    Watatumwa kusaidia "kuweka utulivu" nchi, ambayo ni mwanachama wa Shirika la Mkataba wa Usalama wa Pamoja (CSTO) na Urusi, Belarus, Tajikistan, Kyrgyzstan na Armenia.

    CSTO ilithibitisha askari wa miamvuli wa Urusi walikuwa wakitumwa kama walinzi wa amani, na vitengo vya mapema tayari vimetumwa, na picha zilizotolewa na vyombo vya habari vya Urusi zilionyesha askari wakipanda ndege ya usafirishaji ya kijeshi.

    Maandamano yalianza siku ya Jumapili wakati serikali ilipoondoa bei yake ya kikomo ya LPG, ambayo watu wengi hutumia mafuta ya magari yao, lakini machafuko hayo yameenea na kujumuisha malalamiko ya kisiasa.

  7. Burundi yawafukuza Wanyarwanda 12 kwa kukataa chanjo ya Covid

    Wanyarwanda 12 wakiwemo wanawake na watoto wamefukuzwa na mamlaka ya Burundi baada ya kukataa kupata chanjo ya Covid.

    Raia hao wa Rwanda walikaa zaidi ya siku tano katika eneo la Nyakarama hill katika jimbo la Kirundo kaskazini mwa Burundi.

    Walisema wamekimbia kampeni ya lazima ya chanjo inayoendelea nchini Rwanda.

    Gavana wa jimbo la Albert Hatungimana aliagiza warudishwe Rwanda.

    Alhamisi iliyopita, raia wengine tisa wa Rwanda walirejeshwa nchini kwao na mamlaka ya Burundi katika jimbo hilo.

    Pia walikuwa wamekimbia kampeni ya lazima ya chanjo.

    Katika mkutano wa usalama, gavana alisema Jumanne kwamba hangeweza kuwakaribisha watu ambao hawafuati mpango wa serikali wa kukabiliana na Covid-19.

    Alisema kila mtu alipaswa kupata chanjo ili kuruhusiwa kukaa nchini humo.

  8. Zoezi la uokoaji Pemba limesitishwa

      • Author, Eagan Salla
      • Nafasi, BBC Swahili, Dar es Salaam
    pemba

    Uamuzi huo umekuja baada ya kiongozi wa timu ya kikosi cha wapiga mbizi KMKM Kasim Khalfan kuthibitisha kuwa taarifa za sasa hazioneshi ushahidi wa watu waliopotea majini.

    Usiku wa kwanza miili kumi ilipatikana na watu kumi waliokolewa.

    Hata hivyo siku ya pili timu ya uokoaji haikumpata mtu mwingine yeyote.

    Mamlaka za eneo hilo ziliulizwa kuripoti ikiwa kuna watu wengine zaidi waliopotea na hakuna yeyote mpaka sasa.

    p

    Familia zilizopoteza wapendwa wao bado zinaendelea kuomboleza na miili yote kumi imezikwa tayari.

    Kwa mujibu wa walionusurika wanasema injini ilizima mara mbili kisha boti ikaanza kuzama.

    Amour Nassor alikuwa kwenye boti hiyo na anasema alimuona mpwa wake akiomba msaada kabla hajafariki.

    Wananchi wa eneo hilo hawajafurahishwa na kitengo cha uokoaji cha KMKM kwa kuwa walichelewa kufika licha ya kituo chao kuwa karibu na watu wengi waliokolewa na wanakijiji wanaojua kuogelea katika eneo hilo.

  9. Mbunge wa Kenya afukuzwa kwa kugawanya peremende bungeni

    Mbunge wa Kenya siku ya Jumatano alifurushwa kikaoni kwa siku moja baada ya kupatikana akifawanya peremende kwa wenzake wakati mjadala ulipokuwa ukiendelea.

    Fatuma Gedi alisema "viwango vya sukari vilikuwa vimeshuka" baada ya kushiriki kikao kirefu.

    Alikuwa ametuhumiwa na mbunge mwenzake Ndindi Nyoro kwamba alikuwa akigawanya pesa ndani ya ukimbi wa bunge.

    Bw Nyoro aliombwa kuthibitisha madai yake ya hongo na kuzuiliwa kuhudhuria vikao kwa siku mbili baada ya kukosa kufanya hivyo.

    Bi Gedi alizuiliwa kuhudhuria kikao kimoja kwa kosa la kugawanya bungeni.

    Wabunge waliidhinisha marekebisho kadhaa katika mswada wa vyama vya siasa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu

    Tazama kilichotokea wakati wabunge walipotoa madai ya hongo:

  10. Papa Francis:Kuchagua kuwapenda wanyama badala ya watoto ni ubinafsi

    m

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Papa Francis amependekeza kuwa watu wanaochagua kuwapenda wanyama zaidi ya watoto ni ubinafsi.

    Papa alizungumza hayo alipokuwa akijadili kuhusu suala la uzazi huko Vatican Roma.

    "Leo ... tunaona aina tofauti ya ubinafsi," aliwaambia . “Tunaona baadhi ya watu hawataki kupata mtoto.

    "Wakati wengine wana mtoto mmoja tu, lakini wana mbwa na paka ambao huchukua nafasi ya watoto.

    "Hii inaweza kufanya watu kucheka, lakini ndio uhalisia."

    Kitendo hicho "ni kukataa kuwa baba na mama na kibaya, kinaondoa ubinadamu wetu", aliongeza.

    Papa Francis alisema kwamba watu ambao hawawezi kupata watoto kwa sababu za kibaiolojia wanapaswa kuzingatia kuasili, na kuwataka watu "wasiogope" kuwa wazazi.

    Pia alizungumza juu ya "msimu wa baridi huku idadi ya watu isiyotaka kupata watoto ikiongezeka - "tunaona kwamba watu hawataki kupata watoto zaidi na zaidi.".

    Si mara ya kwanza kwa Papa Francis kulenga watu wanaochagua kuwapenda wanyama badala ya watoto.

    Mnamo mwaka wa 2014, alisema kuwa na mapenzi na wanyama badala ya watoto lilikuwa "jambo jingine la uharibifu wa kitamaduni", na kwamba uhusiano wa kihisia na wanyama ulikuwa "rahisi" kuliko uhusiano kati ya wazazi na watoto

  11. Magereza ya Liberia yaishiwa na chakula cha wafungwa

    Mfungwa

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Magereza yote 15 nchini Liberia wiki hii yameishiwa na chakula cha wafungwa.

    Hii imesababisha magereza mawili, ikiwa ni pamoja na Gereza Kuu la Monrovia, kusitisha kwa muda kuwapokea wafungwa wapya muda, maafisa wa magereza wamesema.

    Hali hiyo imechangiwa na masuala kadahaa ikiwemo kucheleweshwa kwa fedha za chakula na usimamizi wa magereza.

    Lakini mkurugenzi wa magereza, Sainleseh Kwaidah, ameambia BBC siku ya Jumatatu kwamba serikali ilikuwa inafanya kila iwezekanavyo kushughulikia suala hilo.

    Alisema baada ya hatua kuchukuliwa magereza mawili ambayo yalikuwa yamesitisha kuwapokea wafungwa yalifunguliwa na vyakula vinapelekwa katika magereza mengine yaliyosalia.

    Askari magereza aliiambia BBC kuwa magereza yamefunga milango ili kuzuia kuwaweka watu zaidi hatarini kwa sababu ya uhaba wa chakula. Alisema pia kuna uwezekano kwamba wafungwa wenye hasira wanaweza kupanga njama ya kutoroka jela

    Maafisa wa magereza katika siku za hivi majuzi wamekosoa jinsi serikali inavyoshughulikia masuala ya vituo hivyo vya kurekebisha tabia vilivyojaa watu.

  12. Novak Djokovic: Australia yafuta visa ya mchezaji bora wa tenisi duniani

    m

    Visa ya nyota wa mchezo wa tenisi Novak Djokovic ya kuingia Australia ilibatilishwa alipowasili Melbourne.

    Mchezaji huyo nambari moja duniani alishikiliwa katika uwanja wa ndege wa jiji hilo kwa saa kadhaa kabla ya vikosi vya mpakani kutangaza kuwa hajakidhi sheria za kuingia na atafukuzwa.

    Inasemekana kuwa sasa amepelekwa katika hoteli ya kuzuilia watu ya serikali akisubiri kuondoka kwa ndege ya nje.

    Matukio hayo yanakuja huku kukiwa na msukosuko kuhusu kutotozwa chanjo Djokovic alisema alistahili kucheza katika michuano ya wazi ya Australian Open.

    Djokovic hajatoa tamko lolote kuhusiana na hali yake ya chanjo , lakini mwaka jana alisema kuwa "anapinga chanjo".

    Tenisi Australia ilithibitisha msamaha wa kimatibabu kwa mchezaji huyo "kufuatia mchakato mkali wa ukaguzi unaohusisha majopo mawili tofauti" lakini matatizo yaliibuka baada ya Djokovic kuwasili Melbourne Jumatano jioni kutoka Dubai.

    Katika taarifa, Jeshi la Mpakani la Australia lilisema Djokovic "alishindwa kutoa ushahidi ufaao ili kukidhi mahitaji ya kuingia Australia, na visa yake imefutwa.

    Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison amekanusha kuwa Djokovic anatengwa na kusema hakuna mtu aliye juu ya sheria za nchi.

    Katika mkutano na wanahabari siku ya Alhamisi, Bw Morrison alisema kuwa alishauriwa kuwa hakuna ruhusa ya matibabu kwa mchezaji huyo kuingia na kuongeza kwamba ushahidi uliotolewa "hautoshi".

  13. Habari...karibu katika matangazo ya moja ya ukurasa wa BBC Swahili leo ikiwa Alhamisi 06/01/2022