Mwandishi wa Uganda kushtakiwa kwa 'kufanya mawasiliano ya kukera'
Mkewe, Eva Basiima Rukira-Bashaija anasema mumewe alipigwa vibaya alipokuwa kizuizini huku nguo zake zikiwa na damu na miguu kuvimba.
Moja kwa moja
Mtoto mchanga apatikana kwenye pipa la choo la ndege ya Air Mauritius

Maelezo ya picha, Inasemekana mama na mtoto wanaendelea vyema Wafanyakazi wa uwanja wa ndege nchini Mauritius wamempata mtoto mchanga mvulana aliyetelekezwa kwenye choo cha kuhifadhia taka katika choo cha ndege.
Mwanamke mwenye umri wa miaka 20 kutoka Madagascar , anayeshukiwa kujifungua kwenye ndege, alikamatwa.Ndege ya Air Mauritius, iliyowasili kutoka Madagascar, ilitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sir Seewoosagur Ramgoolam tarehe 1 Januari.
Maafisa wa uwanja wa ndege walifanya ugunduzi huo walipoikagua ndege hiyo kwa ukaguzi wa kawaida wa forodha.Walimkimbiza mtoto huyo katika hospitali ya umma kwa matibabu.
Mwanamke anayeshukiwa kuwa mama wa mtoto huyo ambaye awali alikana mvulana huyo kuwa ni wake, alifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu ambao ulithibitisha kuwa alikuwa amejifungua.
Aliwekwa chini ya uangalizi wa polisi katika hospitali hiyo.Inasemekana kwamba yeye na mtoto wanaendelea vizuri.Mwanamke huyo wa Madagascar, ambaye alifika Mauritius kwa kibali cha kufanya kazi cha miaka miwili, atahojiwa baada ya kuachiliwa kutoka hospitalini na kushtakiwa kwa kumtelekeza mtoto mchanga.
Mwandishi wa Uganda kukabiliwa na mashtaka ya kufanya mawasiliano ya kukera

Chanzo cha picha, PEN PINTER PRIZE
Polisi wa Uganda wamesema mwandishi aliyezuiliwa Kakwenza Rukira-Bashaija atashtakiwa kwa mawasiliano ya kuudhi chini ya Sheria ya matumizi mabaya ya kompyuta.
Uthibitisho huo unakuja wiki moja baada ya mshindi huyo wa tuzo ya PEN ya 2021 kwa Mwandishi wa Kimataifa wa ujasiri kukamatwa na watu wenye silaha waliovaa nguo za kawaida na kuvamia nyumba yake huko Kampala.
Msemaji wa Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Twine Charles anasema Kakwenza alikamatwa kutokana na jumbe za twitter za matusi alizochapisha tarehe 24 na 26 Desemba mwaka jana dhidi ya Rais, Yoweri Museveni na mwanae wa kiume , Lt. Jenerali Muhoozi Kainerugaba.Anatarajiwa kushtakiwa mahakamani siku ya Jumanne.
Mkewe, Eva Basiima Rukira-Bashaija anasema mumewe alipigwa vibaya alipokuwa kizuizini huku nguo zake zikiwa na damu na miguu kuvimba.
Alimwona leo kwa mara ya kwanza tangu kukamatwa kwake baada ya maafisa wa usalama kujitokeza kufanya upekuzi na Kakwenza katika nyumba ya familia huko Iganga, takriban kilomita 120 kutoka Kampala.Iwapo atapatikana na hatia, Kakwenza anaweza kukabiliwa na faini ya $135 ( shilingi za Uganda 480,000 UGX) au kifungo kisichozidi mwaka mmoja au adhabu zote mbili kwa pamoja.
Mawakili wake wamewasilisha ombi tofauti la kuachiliwa kwake bila masharti.
Mwanamke awazaa watoto wake mapacha miaka miwili tofauti

Chanzo cha picha, Natividad/Twitter
Mwanamke mmoja kutoka mji wa California nchini Marekani, Fatima Madrigal amejifungua watoto mapacha wawili waliopishana dakika 15, mmoja akizaliwa mwaka 2021 na mwingine mwaka 2022.
Fatima na mumewe Robert Trujillo walipata watoto hao ambapo mmoja wa kiume alizaliwa Desemba 31 majira ya saa 5:45 usiku aliyepewa jina la Alfredo na baada ya dakika 15 ambayo ilikuwa ni saa 6 usiku na siku nyingine mpya na mwaka mpya wa 2022 walipata mtoto mwingine wa kike aliyepewa jina la Aylin.
"Kwangu ni ajabu kuwa hawa ni mapacha lakini si siku wala mwaka mmoja," alisema Fatima katika taarifa iliyotolewa na hospitali alipojifungulia.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Daktari anayefanya kazi katika hospitali hiyo, Dk. Ana Abril Arias, aliiita "mojawapo ya tukio la kukumbukwa katika kazi yangu," Vile vile katika tukio tofauti nadra, mapacha wa mwanamke wa Indiana walizaliwa kwa siku tofauti, miezi, na miongo kadhaa baada ya kuzaliwa kwa dakika 30 tu tofauti, WRTV iliripoti.
Kulingana na ripoti hiyo, mtoto mmoja alizaliwa mnamo Desemba 31, 2019, na mwingine alikaribishwa ulimwenguni mnamo Januari 1, 2020.
Muungano vyama vya siasa wapinga pendekezo la miaka mitano ya mpito.
Muungano wa vyama vya kisiasa nchini Mali, umekataa pendekezo la muda wa miaka mitano wa kipindi cha mpito lililotolewa ba Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) ambayo inakutana katika kikao maalu kuhusu Mali Januari 9 mjini Accra
Kati atarifa siku ya Jumapili, muungano wa "Cadre d'échange", sulisema unapinge kile ilitaja kuwa ratiba ya upande mmoja na isiyofaa ya tarehe ya mwisho ya mpito nchini Mali.
Wanaona kuwa pamoja na kukiuka Mkataba wake, mfumo wake haujajadiliwa nchini humo na hauwakilishi matarajio ya kina ya watu wa Mali.
Viongozi wa Afrika Magharibi watakutana katika mkutano wa kilele wa ajabu kuhusu Mali mnamo Januari 9 mjini Accra, mwezi mmoja baada ya kuzitaka mamlaka za Mali kufanya uchaguzi Februari 27, 2022, kama vile utawala wa kijeshi ulivyojitolea kufanya hapo awali na kutishia kuweka vikwazo zaidi mwezi Januari.
Serikali ya Mali inahalalisha kuongezwa kwa miaka mitano kwa kipindi cha mpito ikitaja hali ya ukosefu wa usalama nchini humo, ambayo imekuwa chini ya tishio la wanajihadi tangu mwaka 2012.
Watu sita wauawa katika shambulio la Al Shabab Kenya

Takriban watu sita wameuawa na vijiji kuchomwa moto na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Al Shabab katika mji wa pwani wa Lamu nchini Kenya.
Polisi wanasema wapiganaji waliokuwa na silaha nzito walishambulia vijiji vya Widho eneo la majembeni Kaunti ya Lamu mapema Jumatatu.
Gazeti la The Star nchini Kenya limemnukuu Kamishna wa Kaunti ya Lamu Irungu Macharia aliyethibitisha kisa hicho akisema operesheni ya kuwasaka wavamizi hao inaendelea.
Hali ya taharuki imetanda katika eneo hilo huku doria za usalama zikiimarishwa.
Kundi hilo la wanamgambo limefanya mashambulizi mengi katika kaunti ya Lamu ambayo iko mpakani mwa Somalia- katika maeneo yanayofikiriwa kuwa ngome ya kundi hilo linaloshirikiana na mtandao wa Al Qaeda.
Messi ajitenga baada ya kukutwa na corona

Chanzo cha picha, Reuters
Lionel Messi ni miongoni mwa wachezaji wanne wa Paris St-Germain waliopimwa na kukutwa na Covid-19.
Mshambuliaji huyo wa Argentina na wachezaji wenzake Juan Bernat, Nathan Bitumazala na Sergio Rico walithibitishwa kuwa na Covid siku moja kabla ya mechi ya PSG ya Kombe la Ufaransa dhidi ya Vannes ya daraja la nne.
Wachezaji hao wanasemekana kuwa wamejitenga.
Bosi wa PSG, Mauricio Pochettino aliongeza kuwa Messi alibaki Argentina ambako alikuwa mapumziko ya majira ya baridi na hatasafiri hadi atakapopimwa tena na kukutwa hana virusi.
Wakati wa mkutano na wanahabari kabla ya mechi Jumapili, Pochettino alisema hawezi kusema tarehe ambayo Messi atarudi.
Mchezo wa kwanza wa ligi wa PSG 2022 baada ya mapumziko yao ya msimu wa baridi ni dhidi ya Lyon ni Jumapili, Januari 9.
Wakati Neymar atakosa mechi hiyo huku akiendelea kupata nafuu kutokana na jeraha la mguu nchini Brazil.
PSG wanasema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 anatarajiwa kurejea mazoezini baada ya wiki tatu.
Mhifadhi maarufu wa mazingira Kenya afariki

Chanzo cha picha, Getty Images
Richard Leakey, mhifadhi na mwindaji maarufu wa wanyama nchini Kenya amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 77.
Kazi kubwa aliyoifanya ni kuitangaza Afrika kuwa na watu wenye ukarimu.
Pia aliongoza kampeni za kukomesha ujangili nchini Kenya, alipata umaarufu kwa kuchoma akiba ya pembe za ndovu zilizowindwa nchini humo.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alisema Leakey "ameitumikia nchi yetu kwa upendeleo wa aina yake".
Leakey alitumikia nyadhifa mbalimbali zikiwemo za serikali ya Kenya , Makumbusho ya Kitaifa ya Kenya, Huduma ya Wanyamapori ya Kenya na kama mkuu wa utumishi wa umma.
"Kando na taaluma yake ya kipekee katika utumishi wa umma, Dkt Leakey anakumbukwa kwa jukumu lake kuu katika mashirika ya kiraia nchini Kenya ambapo alianzisha na kusimamia vyema taasisi kadhaa," Bw Kenyatta alisema.
Heri ya Mwaka Mpya 2022...Karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja katika kurasa yetu ya BBC Swahili!
