Marekani yaiweka Tanzania katika orodha ya nchi hatari kusafiri

Marekani imeweka Tanzania katika orodha yake nchi hatari kusafiri, ikitoa ushauri kwa raia wake dhidi ya kusafiri katika mataifa hayo.

Moja kwa moja

  1. Na kufikia hapo tunakamilisha matangazo haya ya moja kwa moja kwa leo. Hadi hapo kesho kweheri.

  2. Nusu ya maambukizi ya Omicron yaripotiwa barani Afrika-WHO

    Maabukizi ya virusi yamefikia karibu 1,000 ulimwenguni kote na hakuna vifo vilivyoripotiwa

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Nchi kumi za Kiafrika zinachangia 46% ya kesi za Omicron zilizoripotiwa ulimwenguni, kulingana na Shirika la Afya Duniani.

    Inasema nchi nyingi kati ya hizi ziko kusini mwa Afrika, ambapo wanasayansi wanakuwa waangalifu zaidi kwa kesi zingine na wanachunguza sampuli ili kuangalia mabadiliko ya virusi.

    Linasema nchi nyingi kati ya hizi ziko kusini mwa Afrika, ambapo wanasayansi wanakuwa waangalifu zaidi kwa visa vingine na wanachunguza sampuli ili kuangalia mabadiliko ya virusi.

    Viwango vya kulazwa hospitalini na visa vya maambukizi makali yanasalia chini nchini Afrika Kusini, data ya ndani inaonyesha. Lakini utafiti bado unaendelea, WHO inasema.

    Hakuna vifo vya coronavirus vilivyohusishwa na kirusi kipya cha Omicron na marufuku ya usafiri haitazuia kusambaa kwake , shirika hili la kitaifa la duniani liliongeza.

    Kupata chanjo mikononi mwa watu kutazuia virusi hivyo kubadilika zaidi, inasema WHO, lakini barani Afrika, ni Mauritius, Morocco, Tunisia, Ushelisheli, Cape Verde na Botswana pekee ndio wamefikia lengo la kimataifa la kuchanja asilimia 4 ya watu wao kufikia mwisho wa mwaka huu.

    Nchi nyingi za Kiafrika bado hazijatoa dawa kwa sababu za vifaa, wakati mashaka ya umma kuhusu kupata chanjo hiyo bado ni kikwazo.

  3. Somalia inajiandaa kwa wanajeshi wa AU kuondoka

    th

    Chanzo cha picha, Reuters

    Somalia imeunda kamati ya uongozi ya makamanda kutoka vyombo mbalimbali vya usalama ili kujadili kukaribia kutwaa majukumu ya usalama wa taifa kutoka vikosi vya kulinda amani vya Afrika (Amisom).

    Amisom iliundwa mwaka 2007 kusaidia serikali inayotambulika kimataifa mjini Mogadishu kurejesha udhibiti wa nchi na kupambana na al-Shabab. Nchi zinazochangia wanajeshi katika ujumbe huo ni pamoja na Kenya, Uganda, Burundi na Ethiopia.

    Majukumu ya ujumbe wa AU yanatazamiwa kumalizika rasmi ifikapo tarehe 31 Disemba, lakini Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaweza kuliongezea muda .

    Kuna hofu kwamba vikosi vya usalama vya nchi hiyo haviko tayari kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara na mabaya yanayofanywa na kundi la wanamgambo wa al-Shabab.

    Viongozi wa serikali wakiwemo mawaziri na makamanda wa usalama walihudhuria mkutano huo uliolenga kutathmini maendeleo ya usalama.

    Kulingana na wizara, mkutano huo unalenga kutekeleza "maono ya umoja wa kitaifa ya kimkakati na kisiasa" ili kuhakikisha uhamishaji wa majukumu yote ya usalama kutoka kwa Amisom hadi kwa Vikosi vya Usalama vya Somalia.

    Serikali imekuwa ikifanya mikutano na maafisa wa AU na Umoja wa Mataifa kuhusu suala hilo.

    Mwezi Oktoba, Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika lilipendekeza mpango wa kuanzisha ujumbe wa mseto wa UN-AU nchini Somalia kuchukua nafasi ya Amisom, lakini hili lilikataliwa na serikali ya Somalia.

  4. Boris na Carrie Johnson watangaza kuzaliwa kwa mtoto wao wa kike

    Conservatives wametozwa faini ya £17,800 kwa "kukosa kuripoti kwa usahihi mchango" ambao ulilipia ukarabati wa gorofa ya wanandoa hao Downing Street.

    Chanzo cha picha, Reuters

    Boris na Carrie Johnson wametangaza kuzaliwa kwa binti, mtoto wao wa pili tangu awe waziri mkuu.

    Bi Johnson alijifungua mtoto huyo katika hospitali ya London mapema Alhamisi, na Bw Johnson alikuwa huko muda wote.

    Msemaji wa wanandoa hao alisema "mama na binti wanaendelea vizuri sana" na alishukuru timu ya NHS kwa utunzaji na msaada wao.

    Wawili hao waliofunga ndoa Mei mwaka huu, pia wana mtoto wa kiume, Wilfred, ambaye alizaliwa Aprili 2020.

    Kuzaliwa kwa Wilfred kulikuja wiki chache baada ya Bw Johnson kuruhusiwa kutoka kwa wagonjwa mahututi kufuatia matibabu ya virusi vya corona.

    Kiongozi wa chama cha Labour Sir Keir Starmer alituma pongezi zake kwa kuzaliwa kwa binti wa wanandoa hao, na kuongeza: "Tunaitakia familia yako afya na furaha."

    Habari hizo zinakuja katika wiki yenye misukosuko kwa waziri mkuu, huku kukiwa na msukosuko wa umma na wa kisiasa juu ya vizuizi vipya vya Covid.

  5. Wanajeshi wa Uganda wahukumiwa kifungo kwa kuwaua waandamanaji

    Vikosi vya usalama vya Uganda vimeshutumiwa kukiuka haki za binadamu

    Chanzo cha picha, AFP

    Mahakama ya kijeshi nchini Uganda imewatia hatiani wanajeshi wawili kwa mauaji ya watu watatu wakati wa maandamano mwaka jana.

    Maandamano hayo yalianza kufuatia kukamatwa kwa mgombea urais wa wakati huo Robert Kyagulanyi, ambaye pia anajulikana kama Bobi Wine, katika mkutano wa kampeni.

    Mwanajeshi wa kwanza alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kumuua Grace Waiona katika duka la kutengeneza magari - akidaiwa kuwa muandamanaji.

    Pia alimpiga risasi Hussein Ssenoga - mfanyakazi mwenzake ambaye alikataa kusaidia katika kukamatwa.

    Askari wa pili alikuwa mwanachama wa Kitengo cha Ulinzi cha Mitaa. Alihukumiwa kifungo cha miaka 35 jela kwa kumuua Ibrahim Kirevu - mwanaume ambaye alitakiwa kumsindikiza kwenye kituo cha polisi.

    Hizi ni hukumu za kwanza kuhusiana na mauaji yaliyotekelezwa na vikosi vya usalama wakati wa maandamano ya mwaka jana.

  6. Mwimbaji maarufu wa muziki wa pop nchini Kenya ajitokeza kama mpenzi wa jinsia moja

    Mwanachama wa bendi ya afro-pop nchini Kenya Sauti Sol amejitokeza kama mpenzi wa jinsia moja.

    Tamko la hadharani la Chimano lilikuja alipokuwa akielezea wazo la wimbo wake mpya, Friday Feeling, ambapo aliwashirikisha wanajamii wa LGBT.

    "Hakuna kujificha tena," aliambia vyombo vya habari vya ndani.

    Alisema kwa sasa anaishi ukweli wake na atatumia muziki wake kupinga taasubi za kiume zenye sumu, chuki na unafiki.

    Chimano hajawahi kujitokeza hadharani kama mpenzi wa jinsia moja ingawa hapo awali aliwahi kuonekana na wapenzi wa kiume.

    Tamko hilo la hadharani linaweza kuwa kupiga jeki juhudi za kupigania haki za watu wa jamii ya LGBT nchini Kenya, ambapo mapenzi ya jinsia moja yameharamishwa na yanaweza kuadhibiwa kwa hadi miaka 14 jela.

    Ruka Instagram ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa Instagram ujumbe

  7. Burudani mbalimbali katika maadhimisho ya sherehe za uhuru Tanzania

    m
    m
    n
    n
    n
    n
    n
  8. Umoja wa Mataifa yalaani mauaji ya walinda amani wa Togo nchini Mali

    mm

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mkuu wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Mali, Minusma, amelaani mauaji ya wanajeshi saba katika shambulio dhidi ya msafara wao.

    El-Ghassim Wane aliliita "shambulio la woga".

    Msafara wa Umoja wa Mataifa ulipigwa na kilipuzi katika eneo la Bandiagara katikati mwa Mali.

    Wanajeshi waliouawa walikuwa Togo.

    Togo ni nchi ya pili kwa mchango mkubwa wa wanajeshi Minusma kutoka kambi ya kanda ya Afrika Magharibi Ecowas.

    Nchi imerekodi hasara kadhaa za askari katika miaka ya hivi karibuni katika mfumo wa misheni hii.

    Minusma anasema shambulio la hivi punde lililohusisha vilipuzi ni ukumbusho wa dharura wa haja ya kuongeza juhudi za kuleta utulivu katikati mwa Mali.

  9. Polisi yalaani vikali video ya maafisa wapya inayoenea mtandaoni

    m

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Polisi nchini Kenya wamelaani hatua ya kundi la maafisa wapya waliohitimu kurekodi video wakiwatishia raia.

    Vijana hao waliohitimu walisikika katika video iliyoshirikiwa wakijigamba kuwa wao ni "watu wabaya tuliovalia kofia nyekundu " na "raia…tunatoka nje, hatuji kucheza".

    Huduma ya Polisi ya Kitaifa ilitaja matamshi yao "ya kutowajibika, yasiyokubalika na ya kutojali", katika taarifa iliyotolewa Jumatano jioni.

    Walioandikishwa ni wanachama wa Kitengo cha Huduma kwa Jumla (GSU), kitengo cha polisi cha Kenya ambao huvaa kofia nyekundu.

    Huduma ya polisi ilisema tabia iliyooneshwa kwenye video "haikubaliki na haiakisi maadili ya polisi" Taarifa hiyo imetumwa kwenye Twitter:

  10. Vita vya Ethiopia: UN yasitisha kutoa msaada wa chakula katika miji miwili

    m

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Shirika la Chakula Duniani (WFP) limesitisha usambazaji wa chakula cha msaada katika miji miwili ya kaskazini mwa Ethiopia baada ya watu wenye silaha kupora maghala yake.

    Waporaji kutoka kwa vikosi vya waasi wa Tigrayan waliwashikilia wafanyakazi wa misaada wakiwa wamewaelekezea bunduki katika mji wa Kombolcha, Umoja wa Mataifa umesema.

    Waliiba kiasi kikubwa cha chakula muhimu - kikiwepo chakula cha baadhi ya watoto wenye utapiamlo.

    Kaskazini mwa Ethiopia kunakabiliwa na njaa kubwa huku kukiwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea kati ya Tigrayan na vikosi vya serikali.

    Zaidi ya mwaka mmoja wa mapigano, watu zaidi ya milioni tisa wanahitaji chakula muhimu, Umoja wa Mataifa umesema.

    Msemaji wa Umoja wa Mataifa, wa WFP, alisema wafanyakazi wake huko wamekabiliwa na "vitisho vikali" wakati wa siku za uporaji.

    Aliongeza: "Unyanyasaji huo wa wafanyakazi wa kibinadamu unaofanywa na vikosi vya kijeshi haukubaliki.

    Unadhoofisha uwezo wa Umoja wa Mataifa na washirika wetu wote wa kibinadamu kutoa msaada wakati unahitajika zaidi."

    Msemaji huyo pia alishutumu wanajeshi wa serikali kwa kuamrisha malori matatu ya kibinadamu ya WFP na kuyatumia kwa malengo yao binafsi.

    • Mgogoro wa Tigray-Ethiopia: Baa la njaa lililosababishwa na binadamu
  11. Maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania bara katika picha

    m
    m
    m
    m
    m
  12. Rais Samia awasili uwanja wa Uhuru

      • Author, Alfred Lasteck
      • Nafasi, BBC News, Dar es Salaam
    n

    Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameshawasili katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam zinapofanyika sherehe za miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika.

    Samia amepigiwa mizinga 21 ya heshima na kisha kuanza kukagua gwaride la majeshi mbalimbali.

    Sherehe hizi zimehudhuriwa na Marais wa nchi mbalimbali wakiwemo Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na Rais wa Rwanda, Paul Kagame ,rais wa Comoro, Msumbiji na DRC.

    n

    Maadhimisho haya ya miaka 60 ya Uhuru ni ya kwanza kwa Rais Samia ambaye alichukua Hatamu Mwezi Machi mwaka huu

  13. Maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania bara

    Maelezo ya video, Tanzania yaadhimisha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania bara
  14. Tanzania yasheherekea miaka 60 ya uhuru

      • Author, Eagan Salla
      • Nafasi, BBC Swahili, Dar es Salaam
    Maafisa wa serikali Tanzania katika uwanja wa taifa Dar es Salaam kusherehekea miaka 60 ya uhuru
    Maelezo ya picha, Maafisa wa serikali Tanzania katika uwanja wa taifa Dar es Salaam kusherehekea miaka 60 ya uhuru

    Rais Samia leo analiongoza taifa lake katika kuadhimisha miaka 60 ya uhuru.

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ndiye atayekuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo inayofanyika katika uwanja wa taifa mjini Dar es Salaam.

    Wageni wakuu wanaohudhuria sherehe hiyo ni pamoja na Rais Paul Kagame wa Rwanda, Filipe Nyusi wa Msumbiji, Mwenyekiti wa AU , Rais wa DRC Felix Tshisekedi na Rais wa zamani wa Malawi Joyce Banda. Wengine ni wawakilishi waliotumwa na mataifa yao .

    Mkesha wa kuamkia sherehe hiyo ya kitaifa , Rais Samia alihutubia taifa ambapo alitaja mafanikio mbalimbali yaliyopatikana tangu Tanzania ilipopata uhuru na kueleza matumaini yake kwa zaidi, miaka ijayo.

    Akilinganisha mahali nchi ilipo kwa sasa, alisema Tanzania ina mafanikio katika miundombinu, kwa mifano ya maendeleo katika usafiri wa anga na reli, na kuhainisha mabadiliko makubwa katika huduma za kijamii kama elimu na afya.

    Wananchi walivyojaa katika uwanja wa Dar es Salaam kwa sherehe za miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania
    Maelezo ya picha, Wananchi walivyojaa katika uwanja wa Dar es Salaam kwa sherehe za miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania

    Baadhi ya mafanikio ya Tanzania kwa kipindi cha miaka 60

    • Kuulinda uhuru na mipaka yetu
    • Amani
    • Kuimiraisha uchumi - uchumi wa kati
    • Kuboresha huduma za kujamii
    • Kuimarisha demokrasia -Hatujapoteza hata sentimita moja ya ardhi yetu Ni fahari kuwa na jeshi imara na lenye weledi na nidhamu ya hali ya juu Licha ya kuwa na kuwa na makabila 120 bara na pwani tumeunganishwa na kuwa taifa moja na yeyote anaweza ishi popote na kufanya kazi Kiswahili hakikuzungumzwa wakato wa uhuru ila baada ya uhuru tunajjivunia mendeleo yake siku ya lugha ya kiswahili 7 July kila mwaka ( Unesco)
    • Mafanikio tuliyopata ni matokeo ya demokrasia imara na haki ya kuchagua viongozi wanaowataka wakati tunapata uhuru tulikuwa na wabunge 80 sasa tuna wabunge zaidi ya 350
    • Vyombo vya habari vimeendelea kuwa huru ukilinganisha na wakati wa chombo kimoja cha habari wakati tunapata uhuru
  15. Pele alazwa hospitalini kwa mara nyingine

    n

    Gwiji wa soka wa nchini Brazil ,Pele amelazwa hospitalini kwa ajili ya matibabu ya uvimbe kwenye utumbo uliobainika hapo awali, madaktari wake walisema Jumatano.

    Bingwa huyo wa dunia mwenye umri wa miaka 81 alilazwa katika Hospitali ya Albert Einstein mjini Sao Paulo.

    "Mgonjwa anaendelea vizuri na anatarajiwa kuruhsiwa katika siku zijazo." ingawa taarifa hazikusema ni lini Pele alilazwa hospitalini.

    Pele alifanyiwa upasuaji wa uvimbe huo Septemba 4, na kukaa mwezi mmoja hospitalini kabla ya kuruhusiwa kuendelea na matibabu.

  16. Rais wa Burkina Faso avunja serikali

    M

    Rais wa Burkina Faso amemfukuza kazi Waziri Mkuu wake Christophe Joseph Marie Dabiré na kuvunja serikali.

    "Kazi ya Waziri Mkuu imesitishwa, serikali inavunjwa," agizo la rais lilisema.

    Aidha bado hakuna dalili ya ni lini kiongozi mkuu wa serikali atateuliwa.

    Nchi hiyo ya Afrika Magharibi yenye wakazi milioni 20.5, Burkina Faso imekumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya wanajihadi tangu mwaka 2015 ambayo yamewaacha mamilioni ya wakimbizi wa ndani.

    Kaboré ameahidi kuleta "usalama na utulivu" nchini humo katika muhula wake wa pili na wa mwisho lakini hadi sasa hajafanikiwa katika kazi hiyo na kusababisha hasira kuongezeka kutoka kwa wananchi.

  17. Marekani yaiweka Tanzania katika orodha ya nchi hatari kusafiri

    m

    Marekani imeweka Tanzania katika orodha yake ya nchi hatari kusafiri, ikitoa ushauri kwa raia wake kutosafiri katika taifa hilo.

    Kituo cha kudhibiti magonjwa nchini Marekani (CDC) imeweka Tanzania katika orodha ya nchi hatari kusafiri.

    Kituo hicho kimesema ni vyema kutosafiri katika taifa hilo na kama kuna ulazima basi mtu amepata chanjo kamili dhidi ya corona.

    th

    Aidha wamesema, "hali ya sasa nchini Tanzania, hata wasafiri walio na chanjo kamili wanaweza kuwa katika hatari ya kupata na kueneza virusi vipya vya corona" CDC imesema.

    Siku ya Jumapili, taarifa zilienea mitandaoni kuwa msafiri kutoka Tanzania alipimwa na kukutwa na aina mpya ya virusi vya corona- Omicron huko New Delhi, India, na kusababisha mamlaka 'kuanza uchunguzi'.

    Licha ya tahadhari za mara kwa mara kutoka kwa Wizara ya Afya ya Tanzania, uzingatiaji wa umma kwa hatua za kuzuia Covid-19 bado ukochini, Ubalozi wa Marekani umesema.

    • Omicron: Je, utajuaje kwamba umeambukizwa virusi vya Omicron
    • Virusi vya corona: Kituo cha afya CDC Marekani chatahadharisha raia wanaokwenda Afrika Mashariki
  18. Habari...karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya BBC Swahili leo ikiwa 09/12/2021