Jaji wa pili ajiondoa kesi ya kiongozi wa upinzani Tanzania, Mbowe

Jaji Kiongozi Mustapha Siyani amejiondoa kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi Tanzania inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na mwenzake watatu

Moja kwa moja

Ambia Hirsi

  1. Ufaransa yazindua magari ya umeme nchini Tanzania

    magari ya umeme
    Maelezo ya picha, magari ya kutumia umeme

    Waziri wa Biashara na uchumi nchini Ufaransa Franck Riester amezindua magari ya umeme yaliyoundwa na kampuni ya E-Motion Africa.

    Kampuni ya E-Motion Africa iliundwa mnamo 2019 kwa lengo la kutoa suluhisho la asili na rahisi kwa changamoto ya usafiri unaotoa gesi ya kaboni nchini Tanzania na inapendekeza kubadilisha injini ya dizeli ya magari ya uchukuzi kuwa magari ya umeme, unayotumia na nguvu ya betri.

    Kwa mujibu The Citizen nchini Tanzania, Waziri Riester amenukuliwa akisema “Gari lisilotoa gesi chafu ndio gari la siku zijazo”.

    Pia alisema Ufaransa imejitolea kukuza ushirikiano na kushirikiana kiteknolojia na Tanzania.

    Mradi huo ulianzishwa na kampuni ya safari ya Ufaransa Mount Kilimanjaro Safari Club (MKSC) ambayo imekuwa ikifanya kazi kwa miaka 20 kaskazini mwa nchi katika mbuga za kitaifa.

  2. Ndege yamwagia mtu majitaka akiwa kwenye bustani yake

    Ndege ilidondosha maji taka ya kibinadamu kote kwa mtu wakati alikuwa katika bustani

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mwanamume mmoja na mfanyakazi wake walimwagiliwa maji taka kutoka kwa ndege, jopo la uchunguzi lafahamishwa nchini Uingereza.

    Akizungumza katika baraza la Royal Borough ya Windsor na shurika la ndege la Maidenhead, kansela Karen Davies alisema "amegutushwa" kusikia kisa hicho.

    Alielezea jinsi "yeye’’ na bustani lote "lilivyofunikwa" kwa uchafu huo.

    Kisa hicho kilitokea mjini Windsor kati kati ya -Julai.

    Vyoo vya ndege huhifadhi maji taka katika sehemu maalum, lakini yaliyomo kawaida hutupwa mara tu ndege inapotua.

    Diwani wa Clewer Mashariki aliambia kikao hicho kuwa alifahamishwa kuhusu kisa hicho cha "kuogofya" na mkazi wa eneo bunge lake, kulingana na Huduma ya Kuripoti Demokrasia ya Mitaa.

    Diwani wa parokia ya Whitfield, Geoff Paxton, ambaye amefanya kazi katika viwanja vya ndege kwa miaka 40, alitaja tukio hilo kuwa "nadra sana" na ambalo halijawahi kutokea kwa muda mrefu.

    BBC imewasiliana na Mamlaka ya Usafiri wa Angani ili kupata tamko lake.

  3. Wanajeshi wa zamani wa Ujerumani wakamatwa juu ya vita vya Yemen

    Prosecutors say the accused wanted to fight in Yemen, which has been gripped by civil war for years

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Wanajeshi wawili wa zamani wa Ujerumani wamekamatwa kwa tuhuma za kujaribu kuunda kikosi cha mamluki wa kigaidi kupigana katika vita vya Yemen, waendesha mashtaka wanasema.

    Arend-Adolf G na Achim wanakabiliwa na mashtaka ya ugaidi baada ya msako wa polisi kusini mwa Ujerumani Jumatano.

    Wanadaiwa kupanda na kuwasajili hadi wanaume 150 katika jeshi la kibinafsi lilijumuisha maafisa wa zamani wa polisi na wanajeshi.

    Walitaka kutoa huduma zao kwa serikali yaSaudi Arabia kwa uparesheni haramunchini Yemen, waendesha mashtaka walisema.

    Yemen imekumba wna vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya serikali inayoungwa mkono na Saudi Arabia- na kutambuliwa kimataifa na wanamgambo wa Kihouthi tangu mwaka 2014.

    Saudi Arabia iliijiunga na vita vya Yemen mwaka 2015 muda mfupi baada ya mjii mkuu, Sanaa, kutekwa na wapiganaji wa Kihouthis, ambao wanaungwa mkono na Iran.

    Wanajeshi hao wa zamani inasemekana walitaka Saudi Arabia kufadhili oparesheni zao za kibinafsi ya Yemen, waendehsa mashtaka wa Ujerumani.

    Wanaume hao walijaribu kuwasiliana na mashirika ya serikali ya Saudi Arabia lakini hawakupata jibu na juhudi zao hazikufanikiwa.

  4. Benzema akabiliwa na kesi ya udhalilishaji wa kingono ya Ufaransa

    On the pitch Karim Benzema, 33, has scored for Real Madrid and France in the past 10 days

    Chanzo cha picha, Reuters

    Mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema ameshtakiwa nchini Ufaransa kwa kuhusika na jaribio la kumlaghai mwanasoka mwenzake Mathieu Valbuena kuhusiana na viddeo ya ngono iliyopatikana katika simu yake.

    Amepuuza mashtaka dhidi yake na kukosa kufika mahakamani mjini Versailles.

    Kesi hiyo ni ya kutoka Juni 2015, wakati wanasoka hao walikua katika kambi ya mazoezi huko Ufaransa.

    Sakata hiyo iliyokumba soka ya Ufaransa ilifanya wachezaji wote wawili kupoteza nafasi zao.

    Karim Benzema, 33, hata hiyo amerejea katika timu ya Ufaransa na kufungia bao Real Madrid mjini Kyiv Jumanne katika michuano ya Ligi ya Mabingwa.

    Amefunguliwa mashataka pamoja na wanaume wengine wanne kwa kujaribu kumtapeli Bw. Valbuena, ambaye aliambia mahakama kuwa soka ni maisha yake.

    "Nilijua video hiyo ingelivujishwa maisha yangu yataathiriwa katika timu Ufaransa," alisema kulingana na waandishi wa habari.

    Kesi juu ya video hiyo ya ngono ilianza mwaka 2015 wakati Valbuena, ambaye sasa ana miaka 37, kumuomba mtu huko Marseille, Axel Angot, kupakua yaliyomo kwenye simu yake ya rununu kwa kifaa kipya.

  5. Habari za hivi punde, Masharti ya kutotoka nje usiku nchini Kenya yaondolewa

    Rais Uhuru Kenyatta
    Maelezo ya picha, Rais Uhuru Kenyatta

    Rais Uhuru Kenyatta ameondoa masharti ya kutotoka nje kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri nchini Kenya.

    Akizungumza katika sherehe za kuadhimisha siku kuu ya mashujaa, Uhuru amesema kwamba hatua hiyo inafuatia kupungua kwa visa vya maambukizi nchini Kenya.

    Amesema kwamba kufikia sasa ni watu milioni 5 waliopata chanjo ya ugonjwa wa corona na kuongezea kwamba serikali yake inaelekea kuafikia lengo lake la kuwapatia chanjo hiyo watu milioni 10 kufikia Disemba mwaka huu.

    Hatahivyo rais Uhuru Kenyatta amewataka Wakenya kuchukua jukumu la kujilinda na kuwalinda wapendwa wao.

    Hatua hiyo inajiri wakati ambapo Wakenya wamekuwa wakiitaka serikali kuondoa masharti hayo kwa lengo la kuendelea na biashara zao za kawaida.

    Uhuru alisema kwamba baraza la viongozi wa kidini, wafanyakazi wa afya na maafisa wa usalama walifanya kazi nzuri katika kuhakikisha kwamba masharti ya kukabiliana na ugonjwa huo yanaheshimiwa.

    Masharti hayo ya kutotoka usiku yalikuwa yamekandamiza biashara na uchumi wa Wakenya wengi ambao wamekuwa wakijipatia pato lao nyakati za usiku

    Kuhusu mzozo wa mpaka kati ya kenya na Somalia, rais Uhuru aliapa kwamba Kenya haitakubali kutoa hata kipande kidogo cha ardhi yake kwa majirani zake.

    Alisema kwamba serikali yake imeliimarisha jeshi la kenya tayari kulinda mipaka ya taifa hili kwa hali na mali.

  6. Mzozo waendelea Libya miaka 10 baada ya kuuawa kwa Gaddafi

    Kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Ni miaka 10 tangu kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi, kuuawa na waasi katika makabiliano ya risasi.

    Katika machafuko ambayo yameikumba nchi hiyo tangu kifo chake, Libya imefanya chaguzi mbili za wabunge, ya pili akiwa ni ya mwaka 2014 ambao ulisababisha mgawanyiko katika nchi hiyo, kati ya Benghazi Mashariki na Tripoli Magharibi.

    Libya inatarajiwa kufanya chaguzi zaidi mwezi Disemba, ijapokuwa wengi wanaamini chaguzi hizo hazitafanyika.

    Raia wa Libya hawaadhimishi kifo cha Kanali Gaddafi. Mauaji yake ya ghasia mikononi mwa waasi waliomshika alipokua akijaribu kutoroka ni ishara ya kile kilichotarajia kutokea.

    Vita vilivyochochewa na pande mbili zinazohasimiana ndani na nje ya Libya viligawanya Libya na watu wake zaidi.

    Ingawa baadhi ya Walibya wengi ambao wanaendelea kujitahidi kwa utulivu na uhuru ambao walitarajia kupata miaka 10 iliyopita na kuuawa kwa kiongozi huyo, kuna wengine ambao wanchukulia hali ya sasa kama wakati wa usalama na amani chini ya utawala wa Gaddafi.

  7. Habari za hivi punde, Newcastle yamfuta kazi mkufunzi wake Steve Bruce

    Steve Bruce

    Chanzo cha picha, PA Media

    Maelezo ya picha, Steve Bruce

    Mkufunzi wa Newcastle Steve Bruce ameondoka katika klabu ya Newcastle kwa makubaliano ya pande zote mbilisiku 13 tu baada ya Saudia kuinunua klabu hiyo kwa £305m.

    Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 60 alichukua uongozi wa klabu hiyo katika mechi yake ya 1000 akiwa mkufunzi ambapo timu yake ilishindwa 3-2 na klabu ya Tottenham – ikiwa mechi yake ya pekee kama mkufunzi wa klabu hiyo chini ya wamiliki wapya.

    Bruce alisema kwamba kumekuwa na pandashukana kwamba alikuwa akitumaini kwamba wamiliki hao wapya wangepeleka mbele klabu hiyo.

    Graeme Jones atachuku mamlaka ya klabu hiyo kwa muda .

    Klabu hiyo imeshindwa kushinda hata mechi moja tangu ligi ya Premia ilipoanza msimu huuna imekuwa ya pili kutoka mwisho baada ya kucheza mechi nane.

    Bruce aliteuliwa kuiongoza klabu hiyo mwezi Julai 2019 na kumaliza katika nafasi ya 13na 12 katika misimu yake miwili.

    ‘’Nashukuru kila anayehusiana na klabu ya Newcastle kwa kunipatia fursa ya kuifunza klabu hiyo’ , alisema Bruce.

  8. Jaji wa pili ajiondoa kesi ya kiongozi wa upinzani Tanzania, Mbowe

    aa

    Chanzo cha picha, Mwananchi

    Jaji Kiongozi Mustapha Siyani amejiondoa kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi Tanzania inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na mwenzake watatu.

    Huyo ni jaji wa pili kujiondoa katika kesi hiyo inayomkabili kiongozi huyo mkubwa wa upinzani nchini humo, baada ya mapema mwezi uliopita Jaji Elinaza Luvanda naye kujitoa baada ya mshtakiwa namba Nne, Mbowe kwa niaba ya wenzake kusema hawana imani nae.

    Uamuzi wa kujiondoa Jaji Siyani kusikiliza kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 16/2021, kunahusishwa na kuteuliwa kwake na Rais Samia Suluhu kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, uteuzi uliotangazwa Oktoba 8, 2021.

    Katika uamuzi wake leo oktoba 20, 2021 Mahakamani hapo, Jaji Siyani amesema sababu ya kujitoa kusikiliza kesi hiyo kunatokana na majukumu aliyoyanayo ambayo ameona yanaweza kumfanya ashindwe kuendesha kesi kwa haraka.

    Wakati huo huo Mahakama hiyo Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imetupilia mbali pingamizi la kwanza lililowekwa kuhusu maelezo ya mshtakiwa wa pili Adamu Hassan Kasekwa yaliandikwa nje ya muda.

    Mahakama hiyo imekataa hoja ya pili kuwa Adamu Kasekwa aliteswa kwani hakutatolewa ushahidi huo. Hivyo maelezo yalitolewa na mshtakiwa wa pili kwa ridhaa yake.

    Kama ilivyoripotiwa na mtandao wa gazeti la Mwananchi nchini Tanzania, uamuzi huo umetolewa katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

    Akisoma uamuzi huo Jaji Mustapha Siyani ameeleza kuwa anakubaliana na Jamhuri kuwa mazingira yaliyokuwepo yana mantiki kuwa walikuwa wakiendelea na upelelezi.

    Freeman Mbowe na wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka sita yakiwemo ya kula njama na kufadhili fedha kwa ajili ya vitendo vya kigaidi.

  9. Wanajeshi wa Ethiopia wapelekwa vitani Tigray - mashahidi

    Troops advancing to the front line are said to be accompanied by government-allied militias

    Chanzo cha picha, AFP

    Wanajeshi wa serikali ya Ethiopia wanatumwa kuelekea mstari wa mbele wa mzozo na waasi wa Tigraya, mashahidi kaskazini mwa Ethiopia wameambia BBC.

    Mwandishi wa kituo cha redio cha Marekan NPR katika mji wa Kombolcha, alisema wanajeshi hao walikuwa wameandamana na wanamgambo washirika wa serikali wakiwa na silaha zilizoboreshwa zikiwemo mapanga, mashoka na majembe.

    Walisema wanahofia kuuawa na Watigray ikiwa watashindwa kusitisha hatua hiyo.

    BBC haijafanikiwa kuthibitisha madai hayo.

    Mji wa Kombolcha umefurika wakazi wanaotorokamaeneo ya Tigray yanayoshikiliwa, baadhi ya maeneo hayo kulingana na Umoja wa Mataifa yanakabiliwa hali ya njaa baada ya serikali kuyafungia.

    Msemaji Watigray amesema kuwa waasi wanaendelea kukabiliana na maadui, lakini bado wako mbali na Kombolcha.

  10. Msanii wa Ghana Shatta Wale ajisalimisha kwa polisi

    Shata Wale

    Chanzo cha picha, TWITTER/@SHATTAWALEGH

    Msanii maarufu wa Ghana ambaye alisema amekimbilia mafichoni kwa kuhofia usalama wake amejisalimisha, polisi inasema.

    Watu wengine wawili pia wamekamatwa kwa "kueneza taarifa za uwongo" juu ya shambulio la bunduki dhidi ya Shatta Wale.

    "Amekamatwa ili kusaidia polisi katika uchunguzi wa madai yake ya kuhusika katika uundaji na usambazaji wa habari inayokusudiwa kusababisha hofu na taharuki, "polisi walisema juu ya kukamatwa kwa mwanamuziki huyo.

    Polisi walitanga kukamatwa kwake Jumanne sa kadhaa baada ya msanii huyo kuweka ujumbe mtandaoni akisema "maisha yake yako hatari"

  11. Wamiliki wa Pornhub wawafidia waathiriwa wa video ya Girls Do Porn

    Pornhub

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Kampuni mama ya Pornhub imesuluhisha kesi iliyowasilishwa mahakamani dhidi yao na wanawake 50 ambao wanasema ni waathiriwa wa oparesheni ya ulanguzi wa kingono.

    Wanawake hao walisema kwamba Girls Do Porn, inayoangazia maudhui ya watu wazima, iliwalaizimisha kufanya ngono huku wakirekodiwa na kuhadaiwa jinsi kanda hiyo ya video itakavyotumiwa.

    Wanawake 50 waliishtaki Pornhub, wakidai kuwa kampuni hiyo ilikuwa na ufahamu kuhusu madai hayo lakini waliendelea mbele na njama yao.

    Masharti ya makubaliano hayo hayakutolewa kwa umma.

    Katika taarifa, Pornhub kampuni mama ya MindGeek ilisema ilisema hairuhusu kabisa kuchapishwa kwa bidhaa haramu kwenye majukwaa yake.

    "Pande hizo zilifikia azimio la pamoja kusuluhisha mzozo huo na masharti hayo ni ya siri, "Brian Holm, wakili aliyewakilisha wanawake alisema katika taarifa ya barua pepe.

  12. Korea Kaskazini yanadai kujaribu kombora jipya la manowari

    KCNA released a photo apparently showing North Korea's missile being launched from a submarine

    Chanzo cha picha, KCNA VIA REUTERS

    Korea Kaskazini imethibitisha kuwa ilifanikiwa kufania majaribio kombora jipya la balistiki siku ya Jumanne.

    Kituo cha habari cha kitaifa KCNA kimesema kuwa kombora hilo "lina uwezo mkubwa wa udhibiti wa kiteknolojia", ambao utafanya kuwa vigumu kuifikia.

    Korea Kaskazini imefanya msururu wa majaribio ya silaha zake katika wiki za hivi karibuni, ikizindua kile ilisema kuwa silaha za hypersonic na zile za masafa marefu.

    Umoja wa Mataifa inazuia kufanyia majaribio makombora ya balistiki na silaha za nyuklia.

    Ilisema kombora hilo lilifyatuliwa kutoka kwa manowari ile ile ambayo ilizindua kombora la zamani katika jaribio la 2016.

    Kombora hili lilikuwa moja wapo ya silaha mpya zilizojumuishwa kwenye maonyesho ya ulinzi huko Pyongyang wiki iliyopita.

    Ripoti hazikumtaja kiongozi Kim Jong-un, zikidokeza kwamba hakuhudhuria hafla ya jaribio hilo.

  13. Misri yawaapisha majaji takriban 100 wanawake katika hatua ya kwanza kama hiyo

    TH

    Chanzo cha picha, EPA

    Misri imewateua kwa mara ya kwanza wanawake 98 kama majaji katika moja ya vyombo vikuu vya idara ya mahakama nchini humo - Baraza la kuu la serikali .

    Majaji waliapishwa mbele ya jaji mkuu wa baraza hilo katika hafla iliyofanyika katika mji mkuu Cairo Jumanne.

    Inakuja miezi kadhaa baada ya Rais Abdul Fattah al-Sisi kuwataka wanawake wajiunge na vyombo vikuu viwili vya mahakama - baraza na Mashtaka ya Umma.

    Tangu kuanzishwa kwake mnamo 1946, Baraza la serikali limekuwa likiwateua wanachama wa kiume pekee na hadi sasa limekataa kabisa maombi ya wanawake

    Katika miaka iliyopita, wanawake walipinga maamuzi ya baraza, hilo wakisema kuwa wanabaguliwa.

  14. Afrika yahitaji dola bilioni 50 kwa mwaka kupambana na mabadiliko ya tabia nchi

    m

    Chanzo cha picha, AFP

    Ripoti mpya inasema Afrika inahitaji kuwekeza $50bn (£36bn) kwa mwaka ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

    Umoja wa Afrika na taasisi ya hali ya hewa duniani imeonya kuwa watu maskini wapatao milioni 120 wanakabiliana na mafuriko, ukame, kuhama makazi yao na joto lililopita kiasi ifikapo mwishoni mwa muongo kama hakuna jitihada zitafanyika.

    Vilevile wameonya juu ya barafu zote zilizopo barani Afrika kuwa ziko njiani kutoweka ifikapo miaka ya 2040.

    Afrika imepata joto haraka kuliko wastani wa ulimwengu ingawa imewajibika kwa 4% tu ya uzalishaji wa hewa chafu duniani.

  15. Habari...Karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya ukurasa wetu wa BBC Swahili leo ikiwa Jumatano 20/10/2021, Karibu.