Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Maalim Seif: Hali yangu inazidi kuimarika
Maalim Seif amesema kuwa hali yake inazidi kuimarika
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
Aliyekuwa waziri wa fedha Kenya Simeon Nyachae aaga dunia
Aliyekuwa waziri wa fedha nchini Kenya Simeon Nyachae amefariki akiwa na umri wa miaka 88.
Mfanyabiashara huyo , mwanasiasa, katibu wa zamani na aliyekuwa mkuu wa wafanyakazi wa umma alifariki katika hospitali ya Nairobi siku ya Jumatatu ambapo alikuwa akifanyiwa matibabu ya ugonjwa usiojulikana.
Mwili wake kwa sasa umelazwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Lee Funeral mjini Nairobi.
Baada ya kuzaliwa 1932 katika kijiji cha Nyosia, Nyaribare huko Kisii, magharibi mwa Kenya kutoka kwa baba aliyekuwa chifu wa ukoloni Musa Nyandusi , Nyachae alipata mafunzo yake kama msimamizi wa masuala ya umma katika chuo kimoja nchini Uingereza.
Aliajiriwa kama Afisa mkuu wa Wilaya huko kangundo, Machakos na kupanda ngazi hadi kuwa mkuu wa Wilayawakati Kenya ilipojipatia Uhuru wake 1963 kabla ya kuhudumu kama mkuu wa Mkoa kati ya mwaka 1965 na 1979.
Baadaye alihudumu kama katibu mkuu na mkuu wa wafanyakazi wa umma chini ya aliyekuwa rais Jomo Kenyatta na Daniel arap Moi.
Israel itatoa chanjo 5,000 za corona kwa Wapalestina
Israeli inasema kuwa imepata kutoa chanjo 5,000 za corona kwa wahudumu wa afya wa Kipalestina.
Israeli ina mfumo bora wa utoaji chanjo duniani, lakini Wapalestina wanaoishi katika maeneo kama Gaza na Ukingo wa magharibi wa mto Jordan (West Bank) , bado hawajapata chanjo kabisa.
Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanasema Israeli inawajibu wa kutoa chanjo kwa jamii zinazoishi katika maeneo yaliyoathiriwa.
Israeli inasema hii sio sehemu ya makubaliano na haijapokea ombi lolote kutoka kwa Wapalestina.
Watu wapatao 640,000 wameambukizwa virusi vya corona nchini Israeli na 4,700 wengine kufa kutokana na virusi hivyo , kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Hopkins.
Watu wapatao 160,000 walipatwa na maambukizi katika West Bank na Gaza na wengine 1,833 wamekufa.
Baraza la Kiislamu la Uingereza lamchagua kiongozi wake wa kwanza mwanamke
Zara Mohammed amesema ni "heshima " kuteuliwa kama Katibu mkuu baada ya kushinda kwa kura nyingi katika uchaguzi wa makundi yaliyo chini ya mwavuli wa Muungano wa makundi ya shirikisho kubwa zaidi la Waislamu nchini Uingereza (MCB).
Anachukua nafasi ya Harun Khan, ambaye alikamilisha muhula wake wa miaka minne kama mkuu wa MCB.
Bi Zara mwenye umri wa miaka 29-kutoka Glasgow, amesema ana matumaini kuwa wanawake zaidi na vijana wataiga mfano wake kupata nyadhifa za uongozi.
Alisema: "Ninadhani wakati mwingine wanawake husita kuchukua nyadhifa za uongozi hata kama wana ujuzi zaidi wa kufanya hivyo
Meya wa London Sadiq Khan alitweet kuwa uteuzi wa Bi Mohammed ni "wakufurahisa sana " , na akimtakia mafanikio katika kazi yake mpya.
Chama cha Bobi Wine chawasilisha mashitaka mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi
Mawakili wa kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine wamewasilisha kesi katika mahakama ya juu zaidi wakitaka Rais Museveni azuiwe kushiriki uchaguzi ujao.
Wakili wa Bobi Wine Medard Ssegona alipokuwa akiwasilisha kesi hiyo alisema kuwa hawataki kumona Bw Yoweri Kaguta Museveni akishiriki tena uchaguzi ambapo alimshutumu kupanga ghasia;
Awali Makamu mwenyekiti wa chama cha NUP, John Batst Nambesh ambaye pia ni naibu mwenyekiti mkoa wa mashariki alidai wana ushaidi wa kutosha kuonesha udaganyifu uliofanyika katika uchaguzi uliopita.
Wagombea wengine wa Urais pia wamejitokeza kupinga wazi matokeo ya Uchaguzi ikiwa ni pamoja na Bw Patric Amuriat wa chama cha FDC, Jenerali Mugisha Muntu wa chama cha ANT, Norbert Mao wa chama DP na mgombea wa kujitegemea Jenerali Henery Tumukunde.
Uganda yaonya juu ya madai ya 'kufungwa kwa shughuli' za nchi
Waziri wa Uganda wa teknolojia ya mawsiliano ICT Judith Nabakooba ametoa tahadhari ya kuwafunga watu wanaoeneza taarifa za uongo kuhusu "kufungwa kwa shughuli " nchini humo wiki hii.
Waziri Nabakooba alitweet kuwa mamlaka zinatambua kuhusu mpango wa kusabababisha ghasia kuanzia tarehe 3 hadi 7 Februari.
"Ninatoa wito kwa yeyote yule anayejihusisha na mpango huu mbaya kuachana nao. Nchi hii iko salama na usalama utakaoharakisha kumkatamata kila mtu anayepanga kusababisha ghasia ," alitweet
Upinzani wamewasilisha ombi la mashitaka mahakaman kupinga matokeo ya uchaguzi ya mwezi uliopita ambapo Rais Yoweri Museveni alitangazwa kuwa mshindi .
Kiongozi wa upinzani Robert Kyagulanyi al maarufu Bobi Winealipinga matokeo ya uchaguzi akidai kuwa kulikua na wizi wa kura.
Tume ya uchaguzi na Bw Museveni wamekanusha madai hayo.
Magufuli azitaka mahakama kutumia lugha ya kiswahili
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Munira Hussein
- Nafasi, BBC Africa, Swahili
Rais wa Tanzania John Magufuli amehamasisha matumizi ya kiswahili katika shughuli za mahakama nchini humo.
Akizungumza katika maadhamisho ya wiki ya wiki ya sheria Tanzania Magufuli amesema kuwa matumizi ya kiswahili mahakamani yatawasaidia sana Watanzania wa kawaida. "Lugha ya Kiswahili inatumika SADC, EAC sioni sababu kwanini mahakama hamtaki kutumia Kiswahili, kushindwa kutumia lugha hii siyo tu tunawanyima haki wananchi bali tunawaongezea gharama kupitia ukalimani wa kutafsiri hukumu na mienendo ya kesi," anasema Rais Magufuli.
Nchini Tanzania, kiswahili na kingereza Hutumika katika shughuli rasmi za mahakama. Lakini hukumu za kesi zote hutolewa kwa lugha ya kiingereza jambo ambalo limeleta shida kwa Wananchi wa kawaida kuelewa hukumu hizo.
Hata hivyo mwezi uliopita Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, mkuu wa mahakama Tanzania alisema kuwa mahakama itaanza kutoa muhtasari wa hukumu kwa lugha ya Kiswahili kuanzia Februari mwaka huu ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kuanza kuendesha shughuli zote za Mahakama kwa lugha hiyo.
Sudan Kusini yarudisha nyuma majira ya muda wake
Sudan Kusini imerudisha nyuma muda wake kwa saa moja nyuma.
Waziri wa ajira , Bi.Mary Hillary Wani amethibitisha muda mpya utaanza kufuatwa kuanzia saa sita za usiku.
Hata hivyo muda wa kazi haujabadilika ni kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni.
Tarifa kutoka mjini Juba zinasema kuwa Rais salva Kiir ataungana na mawaziri katika tukio hilo la kurudisha nyuma mshale wa saa kwa saa moja kama ishara ya kuthibitisha tukio hilo.
Raia wa nchi hiyo wamepewa wito wa kufadhimisha ishara hiyo pia.
Vyombo vya habari vya Sudan Kusini vimekua vikishirikisha umma taarifa hiyo:
Nigeria kuisaidia Msumbiji kukabiliana na ugaidi
Nigeria imejitolea kuisaidia Msumbiji katika mapambano dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu katika jimbo lenye utajiri wa mafuta llililopo kaskazini mwa Msumbiji, mji wa Cabo Delgado.
Zaidi ya watu 2,000 wameuawa na wengine zaidi ya 500,000 wamekimbia ghasia, kwa mujibu wa kamati ya Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu.
Waziri wa mambo ya nje wa Nigeria , Geoffrey Onyeama, alitembelea Msumbiji mwishoni mwa juma na kukutana na Waziri Mkuu Carlos Agostinho do Rosário.
Bw Onyeama alisema kuwa Nigeria iko tayari kushirikisha uzoefu wake wa kupambana wanamgambo wa Kiislamu na kutoa usaidizi kwa Msumbiji.
Ziara hiyo ilikuwa ni sehemu ya ziara ya kidiplomasia aliyoifanyika katika nchi za kusini mwa Afrika kuhamasisha uungaji mkono nia ya Nigeria kuwa mwenyekiti wa baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika.
Tanzania, Afrika Kusini na Burkinafaso pia zinawania kiti hicho,
Uchaguzi utafanyika wakati wa kikao cha AU kilichopangwa kufanyika wiki hii.
Rais Ramaphosa asema uenyekiti wake AU ulikuwa ni 'ubatizo wa moto'
Rais wa Afrika Kusini ,Cyril Ramaphosa ameelezea wadhifa wake kama Mwenyekiti wa Muungano wa Afrika(AU) kuwa sawa na "kubatizwa kwa moto".
Muhula wake wa mwaka mmoja kama mwenyekiti wa Umoja wa Afrika utamalizika baada ya wiki hii na kiti hicho kitachukuliwa na Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo Félix Tshisekedi.
Bw Ramaphosa amesema kazi yake kubwa katika kipindi cha mwaka mzima uliopita ilikuwa ni kuliongoza bara wakati wa kipindi cha janga la dunia la corona.
Ametaja mafanikio mengine katika upande wa kuimarisha Amani, kuwawezesha wanawake kufungua biashara katika bara la Afrika.
"Katika kipindi hicho, eneo huru la biashara (AfCFTA) liliweza kuzinduliwa na kutangazwa kwa ari mpya ya biashara baina ya mataifa ya Afrika na ushirikiano wa kiuchumi," aliandika.
Chama cha Bobi Wine kuwasilisha kesi mahakamani dhidi ya matokeo ya uchaguzi
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Isack Mumena
- Nafasi, BBC Swahili Kampala
Hatimaye chama cha upinzani cha NUP kinawasilisha leo Jumatatu kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa rais mwaka 2021, yaliyomupatia rais Museveni Ushindi wa asilimia 58.38% huku mpinzani wake mkuu Robert Kyagulanyi akipata asilimia 35.08%.
Idara ya mahakama ilikanusha nusha ripoti zilizokuwa zikisambazwa katika mitandao ya kijamii kwamba mahakama ya juu imekaataa kupokea keshi hiyo.
Makamu mwenyekiti wa chama cha NUP, John Batst Nambesh ambaye pia ni naibu mwenyekiti mkoa wa mashariki amesema wana ushaidi wa kutosha kuonesha udaganyifu uliofanyika katika uchaguzi uliopita.
Wagombea wengine wa Urais pia wamejitokeza kupinga wazi matokeo ya Uchaguzi ikiwa ni pamoja na Bw Patric Amuriat wa chama cha FDC, Jenerali Mugisha Muntu wa chama cha ANT, Norbert Mao wa chama DP na mgombea wa kujitegemea Jenerali Henery Tumukunde.
Jumla ya wagombea 11 walishiriki katika uchaguzi wa urais wa mwezi Januari ambapo Rais Museveni alitangazwa mshindi na kupata fursa ya kuendelea kuliongoza taifa la Uganda kwa muhula wa sita.
Maalim Seif asema 'anaendelea vizuri', baada ya kupatwa na mambukizi ya corona
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif ametoa shukrani kwa watanzania wote waliomtakia Kheri na kumuombea apone haraka.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Maalim aliandika ; "Hali yangu inazidi kuimarika na nawashukuru madaktari na wahudumu wa afya kwa jitihada zao. Naungana na wito uliotolewa na Chama changu cha Act Wazalendo juu ya kuendelea kuchukua tahadhari".
Jumapili, chama cha upinzani cha ACT Wazalendo nchini Tanzania kilitoa taarifa kuwa mwenyekiti wa chama chake, Maalim Seif Sharif Hamad na mkewe Bi Awena, wamethibitika kupata maambukizi ya Covid 19.
Kwa mujibu wa chama iliyotumwa kwenye mitandao yake ya kijamii, ACT Wazalendo imesema kuwa wasaidizi kadhaa wa Makamu huyo wa Rais wa Zanzibar pia wamepatika na virusi vya corona baada ya kufanyiwa vipimo.
Karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya kurasa ya BBC Swahili, leo tarehe 01/02/2021