Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mbunge apoteza wadhifa wa serikali Tanzania kwa kusitasita akila kiapo
Francis Ndulane, aliyekuwa ameteuliwa kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Madini, alijaribu mara kadhaa kutamka maneno
Moja kwa moja
Esther Namuhisa, Dinah Gahamanyi and Ambia Hirsi
Mbunge apoteza kazi Tanzania kwa kusita akila kiapo
Mbunge wa Tanzania aliyeteuliwa katika wadhifa serikalini amepoteza nafasi hiyo baada ya kusitasita wakati kula kiapo.
Francis Ndulane, aliyekuwa ameteuliwa kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Madini, alijaribu mara kadhaa kutamka maneno kabla ya kuambiwa akae chini..
Video ya hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa na Rais John Magufuli imesambazwa katika mtandao wa kijamii Twitter.
Akizungumzia suala hilo Bwana Magufuli alisema aliangalia wasifu wa wateuliwa wote lakini akaongeza kuwa nafasi ya Bwana Ndulane itabadilishwa.
"Nitampatia hii nafasi mtu atakayeweza kula kiapo vizuri," rais alisema.
Alimwambia Bwana Ndulane atasalia na wadhifa wake wa ubunge lakini "tutalazimika kupata mbadala".
Bwana Ndulane hajatoa tamko lolote kwanini alitatizika wakati wa kula kiapo.
Tazama upasuaji wa kuongeza kimo unavyofanywa
Upasuaji wa kurefusha miguu unajumuisha mambo mengi sana ikiwa ni pamoja na mifupa kuvunjwa kuunganishwa. Upasuaji wa aina hiyo ulikuwa ukifanyiwa watu waliopata ajali, lakini sasa mamia ya watu wanafanyiwa upasuaji huo katika maeneo tofauti duniani.
Gharama ya upasuaji huo uko juu sana na licha ya hatari inayotokana na changamoto yake baadhi ya watu wako tayari kufanyiwa.
Matokeo ya kura zilizohesabiwa Ghana yaonesha rais wa zamani John Dramani Mahama anaongoza
Matokeo ya uchaguzi yaliyokwisha kutangazwa na Tume ya uchaguzi ya Ghana yanaonesha kuwa rais wa zamani John Dramani Mahama wa chama cha NDC anaongoza.
Hadi sasa tume hiyo imekwishatangaza matokeo kutoka majimbo saba kati ya majimbo 16nchini humo.
Takwimu zinaonesha kuwaJohn Dramani Mahama alipata kura 1,997,450.
Huku rais anayewania muhula mwingine Nana Akufo-Addo wa NPP akipata kura 1,500,310.
Hadi kufikia Jumatano asubuhi, matokeo ya majimbo saba ya uchaguzi yalikuwa yametangazwa kama ifuatavyo:
- Upper West: NPP: 121,230 - NDC: 238,972
- North East: NPP: 122,742 - NDC: 112,306
- East Bono: NPP: 292, 604 - NDC: 203,329
- Oti: NPP: 103,865 - NDC: 181,021
- Voltage: NPP: 100,481 - NDC: 606,508
- Ahafo: NPP: 145,584 - NDC: 116,485
- Central: NPP: 613,804 - NDC: 538,829
Covid-19 yaongoza orodha ya taarifa zilizotafutwa zaidi kwenye Google 2020
Katika mwaka ambao umegubikwa na athari za janga la corona, sio jambo la kushangaza kwamba ugonjwa huo ulitafutwa sana katika mtandao wa Google nchini Kenya, Afrika Kusini na Nigeria, kwa mujibu wa uchunguzi wa kampuni hiyo, kutokana na jinsi maswali yalivyoulizwa kuhusu ugonjwa huo.
Afrika Kusini ambayo iliathiriwa zaidi na janga la corona barani Afrika, watu walitafuta taarifa kuhusu amri ya kutotoka nje na habari kuhusu sigara na pombe ambazo zilipigwa marufuku kuuzwa.
Nchini Kenya, baadhi ya mambo yaliyotafutwa katika mtandao kuhusu janga la corona ni pamoja na: jinsi ya kutengeneza vyeyuzina namna ya kuimarisha kinga ya mwili.
Taarifa za kupotosha kuhusu mtandao wa 5G kusambaza virusi vya corona zilikuwa miongoni mwa masuala yaliitafutwa na watu nchini Afrika Kusini .
Pia watu walipendelea taarifa kuhusu uchaguzi wa Marekani na katika nchi hizo tatu zaidi wakitaka kupata maelezo zaidi kumhusu rais Joe Biden na makamu wa rais mtarajiwa Kamala Harris.
Wanigeria, sawa na watumiaji wengine wa mtandao wa Google nchini Kenya na Afrika Kusini, walitafuta taarifa kuhusu watu mashuhuri nchini humo.
Taarifa kuhusu Ligi ya Primia zilikuwa maarufu sana nchini Kenya.
Nchini Nigeria, wembo wa Fem, ulioimbwa na nyota wa miondoko ya kiafrika Davido ulitafutwa zaidi.
Rais Magufuli apunguza adhabu za wafungwa katika maadhimisho ya miaka 59 ya uhuru
Katika maadhimisho ya miaka 59 ya uhuru nchini Tanzania, Rais Magufuli ametangaza kupunguza adhabu za wafungwa za kunyongwa na kutaka wafungwe maisha.
"sheria inaniambia niue wafungwa 256, sasa mimi au huyo aliyeua mtu mmoja nani atakuwa mwenye dhambi"
Rais ametaka wafungwa hao 256 wapewe kazi badala ya kunyongwa.
Aliongeza kusema kuwa kuna wafungwa wengine zaidi ya 3000 ambao hawana kesi za mauaji, wao watapunguziwa adhabu zao za kifungo na wengine wenye makosa madogomadogo wataachiwa huru.
Rais Magufuli awaapisha mawaziri Tanzania,ataka wawajibike
Rais John Magufuli amewaapisha leo mawaziri 21, na manaibu waziri 23. Novemba 13 aliteuwa waziri wengine wawili hivyo idadi ya mawaziri walioapishwa kuwa mawaziri kuwa 23.
Rais Magufuli anasema kazi ya kuwachagua ilikuwa ngumu kutoka idadi ya zaidi 300.
"Wote walikuwa wanafaa kupewa uwaziri au unaibu uwaziri. Ilikuwa kazi nzito kufanya uamuzi, Kuna vitu vingi ambavyo tumeviangalia katika uteuzi tulioufanya."
Hata hivyo aliongeza kusema waliochaguliwa sio kwamba ni wazuri sana kuliko wengine, hivyo waende kufanya kazi kwa kuwa watanzania wanataka kuona kazi na wakishindwa yeyote anaweza kuwekwa kwa mbadala.
Aliongeza kusema kuwa "ni nafuu kufanya maamuzi yakawa mabaya kuliko kutofanya chochote, fanyeni maaamuzi yatakayosaidia maslahi ya wananchi. Suala la ushirikiano ndio jambo la muhimu ili kazi iweze kutekelezeka".
Rais Magufuli alisisitiza kuwa jambo muhimu ni kusimamia kazi kwa weledi.
"Sitaki mitindo ile ya kisasa ya kupiga selfie kwa kila unachofanya, unapaswa kufanya kazi na ajenda nyingine ni za siri . Teknolojia mpya ni nzuri lakini ni muhimu kwa kuzingatia maadili ya kazi zenu.
Ndani ya serikali ni vyema kufanya kazi kwa uadilifu , kuna makundi mengi katika mitandao ya kijamii . Ndani ya serikali ni vyema kuzingatia siri na maadilli tulio nayo."
Mchezo wa PSG na Instambul kuchezwa tena leo kuanzia dakika ya 14
Mchezo kati ya Paris St-Germain dhidi ya Istanbul Basaksehir utachezwa siku ya Jumatano baada ya kutelekezwa siku ya Jumanne wakati afisa wa mechi hiyo akishutumiwa kutoa maneno ya kibaguzi .
Instanbul imedai mwamuzi wa nne Sebastian Coltescu alitumia lugha ya kibaguzi kwa kocha wao msaidizi Pierre Webo.
Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa, Webo alioneshwa kadi nyekundu baada ya kurushiana maneno na muamuzi wa nne
Wachezaji wa Instambul walitoka nje ya uwanja wakikemea kitendo hicho, huku PSG wakifuatia
Tukio hilo lilitokea dakika 14 tu tangu kuanza kwa mchezo wa kundi H, mchezo ambao walikuwa hawajafungana.
Mchezo huo utaanza Jumanne kuanzia dakika ya 14 ya mchezo,mchezo utaanza saa 2:55 saa za Afrika Mashariki
Maafisa wengine watausimamia mchezo huo, huku Mholanzi Danny Makkelie akiteuliwa kuwa mwamuzi.
Wachina waruhusiwa kuingiza chanjo Uganda
Uganda imewaruhusu raia wa China wanaoishi nchini humo kuagiza chanjo ya kujikinga na Covid 19 kutoka nchini kwao.
Vyombo vya habari nchini Uganda vimesema, raia wa China wanaoishi nchini Uganda wanaweza kuagiza chanjo ya Covid-19 ili kukabiliana na janga hili.
Kwa mujibu wa mtandao wa Nile Post umeandika ,serikali ya Uganda imeruhusu kuagizwa kwa dozi 4,000 zinazofahamika kama VeroCell ambazo zitatumiwa katika jamii ya Wachina peke yake wanaoishi katika eneo la Nakaseke.
Wachina hao wamesema kuwa waliiomba serikali ya Uganda kuwasaidia kuagiza chanjo kutoka China.
Wapinzani walalamikia kushambuliwa Ghana
Kiongozi wa upinzani nchini Ghana, John Mahama, ameelezea wasiwasi wake juu ya matumizi ya jeshi, ambapo wamekuwa wakiwatishia wafuasi wake na kulalamikia mashambulizi yaliyotokea katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.
Serikali imekanusha madai hao ya kufanya mashambulizi.
Matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Jumatatu bado yanahesabiwa.
Huku zaidi ya watu milioni 17 walipiga kura kumchagua rais mpya pamoja na wabunge wapya nchini humo.
Ingawa vyama viwili vikuu vinadai kuwa vimeshinda uchaguzi licha ya kwamba matokeo hayajatangazwa rasmi.
Mpaka sasa rais Nana Akufo Addo, anaonekana kuongoza katika kinyang'anyiro hicho.
Tume ya uchaguzi Ghana’ ilihaidi kutangaza matokeo saa 24 baada ya kura kumalizika kupigwa, lakini wamesema wamehitaji muda zaidi ili kuwa na majibu ya uhakika zaidi.
Waziri mkuu wa Ethiopia afanya ziara yake ya kwanza tangu mzozo wa Tigray uanze
Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ameanza ziara yake leo nchini Kenya.
Ziara hii itakuwa ya kwanza tangu waziri mkuu huyo atangaze kufanya operesheni ya kijeshi kaskazini mwa nchi yake.
Kiongozi huyo atakaribishwa na menyeji wake rais Uhuru Kenyatta katika eneo la Moyale, mji ambao upo mpakani mwa Kenya na Ethiopia.
Viongozi hao wawili wanatarajia kuanza na ukaguzi wa miradi ya ujenzi.
Ukiwemo mradi wa mpaka wa Moyale unaofahamika kama 'One Stop Border Post (OSBP) ' na bandari mpya ya Lamu.
Mataifa hayo mawili ambayo yamekuwa katika uhusiano mzuri, viongozi wao wamekuwa wakikutana mara kadhaa lakini ujio huu wa Abiy umeonekana kuwa na mtazamo chanja zaidi.
Mgogoro unaondelea kati ya serikali ya shirikisho nchini Ethiopia umeweza kugonga vichwa vya habari duniani tangu mwanzoni mwa mwezi Novemba.
Mamia wameuawa na maelfu wamekimbia makazi yao kutokana na mapigano ya Tigray.
Ingawa kumekuwa na migogoro katika wakazi wa mpakani wa Kenya, suala ambalo si geni.
Wiki chache zilizopita,jeshi la Ethiopia liliwakamata wakenya wapatao 10 na kuwapeleka magharibi mwa Ethiopia.
Mgogoro huo utakuwa miongoni mwa ajenda zitakazozungumziwa na viongozi hao katika mkutano wao wa Jumatano na Alhamisi.
Habari...Heri ya sikukuu ya uhuru Tanzania..Karibu katika matangazo ya moja kwa moja, leo hii ikiwa tarehe 9 Desemba 2020.