Mzozo wa Israel na Palestina: Video inayonekana kuonyesha vifaru vya Israel ndani ya Gaza
Iliyochapishwa
Video iliyotolewa na Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) inaonekana kuonyesha makumi ya vifaru vya Israel na magari ya kijeshi huko Gaza.
Jeshi la Israel limesema linapanua oparesheni zake za ardhini na kwamba mara moja "ndege 100 za kivita" zilitumika kushambulia kwa mabomu Ukanda wa Gaza.
IDF haikubainisha ni wapi katika eneo la Gaza kanda hiyo ilirekodiwa na BBC haijaweza kuthibitisha kikamilifu video hiyo au wakati ilirekodiwa.



