Je, mmea huu unaweza kulisha ulimwengu?

Maelezo ya video, Je, mmea huu unaweza kulisha ulimwengu?
Iliyochapishwa

Mabadiliko ya tabia nchi , ambayo huleta ukame mkali wa mara kwa mara na mafuriko, yanafanya kuwa vigumu kukuza chakula cha kutosha - kulingana na Umoja wa Mataifa, uzalishaji wa chakula duniani lazima uongezeke kwa 70% ifikapo mwaka 2050.

Mwani una uwezo wa kusaidia kulisha idadi ya watu inayoongezeka duniani, na pia ni nzuri kwa afya yako na mazingira.

BBC ilizungumza na Kirk Haworth, mpishi na mmiliki wa mkahawa wa mimea, Plates London, ambaye alisifu uwezo wa mwani na mwanaikolojia wa baharini Profesa Ana Queirós ambaye alizungumzia kuhusu umuhimu wa mmea huo kiuchumi na kimazingira.