Wakati ndege isio na rubani ya Ukraine iliposhambulia meli ya Urusi katika bahari nyeusi

Maelezo ya video, Tazama: Wakati ndege isio ya rubani ya Ukraine ilipokaribia meli ya Urusi
Iliyochapishwa

Huu ni wakati ambapo ndege isiyo na rubani ya baharini inaelekea moja kwa moja kuishambulia meli ya Urusi karibu na bandari ya Novorossiysk, ambapo milipuko imesikika usiku kucha.

Picha zilizotoka katika idara ya usalama ya Ukraine zinaonyesha ndege hiyo isiyo na rubani ikivuka Bahari Nyeusi na kuikaribia meli ya Urusi.

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema imezima shambulio la Ukraine kwenye kambi yake ya jeshi la wanamaji huko kwa kutumia ndege mbili zisizo na rubani.

Ingawa wizara haikutoa maoni yoyote kuhusu uharibifu wowote, vyanzo vya kijasusi vya Ukraine vimeviambia vyombo mbalimbali vya habari kuwa Olenegorsky Gornyak, "meli ya Urusi iliyoundwa kubeba vifaa na wafanyakazi ilishambuliwa.