Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kulipia samaki kutumia ngono:'Niliuza mwili wangu kwa wavuvi kupata samaki'
Kaunti ya Kisumu, Magharibi mwa Kenya, inajivunia juhudi zake za kubadilisha , tabia iliyokithiri miaka ya hapo awali iliyohusisha baadhi ya wanawake wanaofanya biashara ya kuuza Samaki kuuza miili yao kwa wavuvi ili kupata samaki wa kuuza badala ya kutumia pesa kama malipo ya kawaida .
Elizabeth Atieno, ambaye alishiriki tabia hii inayofahamika kama ‘jaboya’ anasimullia mabadiliko makubwa ambayo yamefanyika baada ya wanawake wafanyabiashara wa samaki katika ufuo wa ziwa Victoria nchini Kenya kupata uhamasisho na kupunguza kutegemea wanaume kupata samaki ili kuendelea na biashara .