Tazama: Ndege za Urusi 'zikihangaisha' ndege zisizo na rubani za Marekani Syria - Jeshi la Anga la Marekani

Maelezo ya video, Tazama: Video iliyotolewa na Jeshi la Anga la Marekani inaonyesha ndege za Urusi 'zikihangaisha' ndege zisizo na rubani za Marekani
Iliyochapishwa

Jeshi la Wanahewa la Marekani limetoa kanda za video zinazoonyesha ndege za Urusi "zikisumbua" ndege zisizo na rubani za Marekani juu ya anga ya Syria.

Luteni Jenerali wa Jeshi la Wanahewa Alexus Grynkewich alisema kuwa, wakati wa tukio hilo, Marekani ilikuwa ikiendesha misheni dhidi ya shabaha za kundi la Islamic State.