Mwanaume aokolewa asiburutwe chini ya treni yenye kasi India

Maelezo ya video, Watch: Moment man saved from being pulled under moving train at Indian station
Iliyochapishwa

Mwanamume mmoja aliokolewa ili asivutwe chini ya treni iliyokuwa mbioni kwenye kituo katika Wilaya ya Purnea, mashariki mwa India.

Mwanaume huyo aliokolewa na mwanajeshi wa Kikosi cha Ulinzi cha Reli cha India (RPF) baada ya kujikwaa na kuanguka alipokuwa akijaribu kupanda treni.

Vyombo vya habari vya ndani viliripoti kuwa tukio hilo ambalo lilinaswa na kamera ya CCTV, lilifanyika katika kituo cha treni cha Purnea Junction, katika jimbo la mashariki la Bihar