‘Baada ya kuokolewa kutoka kwa ndege tulihofia boti ingezama'-Manusura wa ajali ya Bukoba

Maelezo ya video, Manusura na mashahidi wazungumza kuhusu ajali ya ndege ya Bukoba
Iliyochapishwa

Manusura na mashahidi wa ajali ya ndege ya huko Bukoba nchini Tanzania wamesimulia kilichotokea kabla na pindi baada ya ajali hiyo wakati ndege ya Precison Air ilipotua katika Ziwa Victoria .

Ajali hiyo ilisababisha vifo vya watu 19 huku wengine 26 wakiokolewa .

Baadhi ya manusura wamesema walihofia kwamba boti waliokuwa wamehamishiwa baada ya kuokolewa kutoka kwa ndege hiyo ingezama kwa sababu ya idadi kubwa ya watu waliokuwa wameiabiri .