'Nilificha ugonjwa wangu kwanza ili nisipatikane na matatizo nirudishwe nyumbani'
Iliyochapishwa
“Ni kheri umuone daktari mapema uanze matibabu ya saratani, kuliko kujificha, kwani kutakugharimu sana baadaye” Huu ni ujumbe ambao Douglas Kipkoech mwenye umri wa miaka 32 alisisitiza sana kwani alificha hali yake ya kukauka kwa ngozi na hatimaye akapatikana na saratani ya ngozi kwa jina Cutaneous T-cell lymphoma (CTCL) ambayo ni miongoni mwa saratani zilizo nadra sana.
Wanahabari wetu Paula Odek na Judith Wambare walimtembelea Douglas na familia yake mjini Eldoret nchini Kenya na kutuandalia taarifa hii kabla ya Douglas kufariki Dunia miezi miwili iliyopita. Taarifa hii ni kwa ruhusa ya mke wake Mercy Mugure.