Shimo la ajabu la Chile lawashangaza wengi

Iliyochapishwa

Maafisa nchini Chile wanachunguza shimo la ajabu linaloendea kuongezeka kina lililojitokeza wikendi katika eneo la mgodi kaskazini mwa nchi hiyo.

Picha za droni zinaonyesha shimo kubwa kwenye ardhi ya mgodi wa machimbo ya madini unaoendeshwa na kampuni ya Canada - Lundin Mining.

Taasisi ya kitaifa ya huduma za Giolojia na machimbo, Sernageomin, imewatuma wataalamu kwenye eneo hilo, ambalo lipo takriban maili 413 (665km) kaskazini mwa mji mkuu, Santiago.