Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mzozo wa Ukraine: Kamera ya CCTV yaonesha watu wakitoroka kufuatia shambulio la Urusi Kremenchuk
Picha za CCTV kutoka kwenye kidimbwi cha maji katika mji wa Kremenchuk nchini Ukraine zimenasa raia waliokuwa wakikimbia kujificha na kuanguka chini huku makombora ya Urusi yakishambulia eneo jirani na kusababisha vifo vya takriban watu 18.
BBC imechambua kanda hiyo - na inaonekana kombora moja lilipiga karibu na ituo cha biashara, huku lingine likipiga kaskazini wa kiwanda cha karibu.
Urusi inadai kushambulia kituo cha kuhifadhi silaha kilichosababisha moto na kuteketeza jengo la karibu la maduka.
Maafisa wa Ukraine wamekanusha kuwa kulikuwa na ghala la silaha karibu.