Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Halima Mdee na wenzake kusalia na ubunge wao?
Mahakama Kuu Dar es Salaam imetupilia mbali maombi ya Halima Mdee na wenzake kutokana na kuwepo kwa kasoro kuhusu jina la mjibu maombi wa kwanza.
Wajibu maombi walikuwa Bodi ya Wadhamini wa Chadema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
Chadema kupitia jopo la mawakili wake linaloongozwa na Peter Kibatala waliweka pingamizi wakiiomba Mahakama hiyo isiyasikilize maombi hayo, wakidai kuwa yana kasoro za kisheria huku wakibainisha hoja sita.
Mzozo wa nafasi za kibunge kwa wabunge hao zilianza mara tu baada ya uchaguzi wa mkuu wa mwaka 2020, ambapo Chadema ilipinga matokeao na ‘kususa’ kupeleka majina ya wabunge wa viti maaalumu kwa kile ilichoeleza kutoridhishwa na mchakato mzima wa uchaguzi, uliompa ushindi hayati John Magufuli.
Hata hivyo, wabunge hao, walitangazwa na aliyekuwa spika wa bungee, Job Ndugai kama wabunge wa viti maaalumu wa Chadema, lakini chadema ilikana kuwatambua, ikisema hakijawasilisha jina lolote la wabunge hao.
Wakafukuzwa na Kamati kuu ya chama, wakakata rufaa baraza kuu, ambalo nalo liliungwa mkono kufukuzwa kwao kabla ya kwenda Mahakamani na mahakama kutupitilia mbali maombi yao.
Mwandishi wetu Scolar Kisanga amezungumza na mwanasheria, Fulgence Massawe, kuhusu nini hasa maana ya uamuzi wa Mahakama?