Ubaguzi wa rangi: Kundi moja la Watoto wa Kiafrika laagizwa na sauti ya kamera kusifu maneno fulani machafu ya kichina

Maelezo ya video, ‘’Mimi ni zimwi jeusi lenye akili ndogo‘’:Watoto waagizwa kurejelea hayo bila kujua maana
Iliyochapishwa

Kundi moja la Watoto wa Kiafrika limeagizwa na sauti ya kamera kusifu maneno fulani ya kichina.

Watoto hao wanarejelea maneno hayo kwa tabasamu, lakini hawaelewi kwamba wanachoagizwa kusema ni maneno yenye maana ya ‘’mimi ni zimwi jeusi lenye akili ndogo’.

Kanda hiyo imezua hisia kali nchini China na kwengineko. Lakini hakuna aliyejibu maswali muhimu: kwanini kanda hiyo ilirekodiwa ? na ni nani aliyeirekodi?

Maswali hayo yalimshinikiza Ripota wa BBC wa kitengo cha Afrika Eye Runako Celina na Henry Mhango kufunga safari kuelekea katika sekta ya video inayowanyanyasa watoto wadogo barani.