Mr. Albino East Africa: ‘Sitosahau siku walipotaka kuvunja mlango na kukoswa kuuawa’
Iliyochapishwa
Ikiwa leo tarehe 13/06 ni siku ambayo dunia inaadhimisha siku ya Walemavu wa ngozi duniani (albino), Emmanuel Shedrack anakumbuka alivyonusulika kuuawa kwasababu ya ulemavu wake wa ngozi (ualbino) kutokana na imani potofu na za kishirikina katika jamii.
Anaamini kupitia mashindano ya ulimwende na utanashati jamii itapata ujumbe kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi wanaweza na ni binadamu wa kawaida tu. Emmanuel Shedrack amezungunza na Mwandishi wa BBC Frank Mavura...