Mzozo wa Urusi: Wanajeshi wa Urusi wakaribia kuuteka mji wa Severodonetsk - fahamu kinachoendelea

Chanzo cha picha, Getty Images
Jeshi la Urusi limepiga hatua na kuingia ndani ya mji wa Severodenetsk , huku mapigano makali yakiendelea katika mji huo , amesema mkuu wa utawala wa Lugansk , Serhiy Gaidai siku ya Jumatatu.
Kulingana na ripoti hiyo ya jioni kutoka kwa vikosi vya Ukraine vilivyopo katika makabiliano , vita pia vinaendelea katika barabara kuu inayounganisha Severodonetsk na Lysichank na Bakhmut Pamoja na eneo lote linalodhibitiwa na Waukraine.
Akizunumza katika runinga, Gaidai aliwaomba raia kusalia katika mji huo ndani ya nyumba zao . Kulingana na yeye uhamishaji wa raia kutoka katika jimbo la Luhank utasitishwa kwa kuwa kuna hatari kubwa kwa sasa.
Mapema siku ya Jumatatu, Gidai aliripoti kwamba vikosi vya Urusi vilikuwa vimeingia maeneo ya kaskazini mashariki na kusini mashariki - viungani mwa mji wa Severodonetsk na vilikuwa vinajaribu kuingia katikati mwa mji huo.
Makabiloiano makali yamekuwa yakiendelea nje ya mji huo pamoja na mji wa Jirani wa Lisichansk siku nzima.
"Ili kuimarisha kambi zao za wanajeshi , adui alihamisha risasi na vifaa kutoka Urusi hadi maeneo fulani," ripoti ya asubuhi ya Mkuu wa Kikosi cha Wanajeshi wa Ukraine inasema.
Severodonetsk na Lysichansk, ziko kusini-magharibi mwa eneo hilo, lenye idadi kubwa ya watu . Haya ni makazi makubwa ya mwisho kwenye eneo la mkoa wa Luhansk ambayo yanabaki chini ya udhibiti wa Kyiv, na hamu ya kuyateka sio tu ya kimkakati, lakini pia umuhimu kwa Urusi.
Shambulio la uvamizi wa Severodonetsk lilifanikiwa baada ya wiki kadhaa za mapigano makali, huku jeshi la Urusi kufanikiwa kuvunja ngome za jeshi la Ukraine katika jiji la Popasna, lililopo kilomita 30 kutoka jimbo la Luhansk

Vyanzo vya Kirusi vinaripoti kurudi kwa vikosi vya UKraine kutoka Severodonetsk kuelekea Lysichansk, lakini hakuna uthibitisho wa habari hii. Mapema Mei 28, mkuu wa Chechnya, Ramzan Kadyrov, alidai kwamba Severodonetsk ilikuwa chini ya udhibiti kamili wa Urusi. Hatahivyo Gaidai anasema kuwa wanajeshi wa Ukraine wanaendelea kuushikilia mji huo.
Tarehe 29 mwezi Mei , vikosi vya Urusi viliendeleza mashambulizi dhidi ya mji wa Severodonetsk , ijapokuwa hatuwezi kuthibitisha ufanisi wowote , wachambuzi kutoka taasisi ya mafunzo ya vita ISW waliandika. Kwa kuongezea , vikosi vya Urusi vilikuwa vikajaribu kuelekea Severodonetsk kutoka Bobrovo na Ustinovka."

Chanzo cha picha, Getty Images
Wataalamu wa jeshi la Marekani wanaamini kwamba kasi ya ufanisi uliopigwa na majeshi ya Urusi huenda ukapungua . Haiwezekani kwamba vikosi vya Urusi vitaweza kutekeleza mashambulizi mengi zaidi kwasababu kuna uwezekano mkubwa vitaondoka katika mji wa Izyum na magharibi mwa Liman ili kupatia nguvu vikosi vilivyopo katika mji wa Severodonetsk katika siku zijazo, iliandika ISW.
Wakati huohuo , Vikosi vya Urusi havijasitisha majaribio yao ya kuiteka barabara ya Lisichansk-Bakhmut ili kuweza kukata usambazaji wa vifaa unaotekelezwa na jeshi la Ukraine . Ni hatari kutumia barabara ya Lisichansk-Bakhmut , tunatumia mbinu mbadala zilizo salama ili kufanya uhamishaji Pamoja na usafirishaji wa bidhaa za kibinadamu , alisema Serhiy Gaidai, Mkuu wa utawala wa Lugansk.
Unaweza pia kusoma
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Mapema, alisema kwamba jeshi la Ukraine lilitekeleza mashambulizi madogo na kulisukuma kundi la vikosi vya Urusi nje ya kijiji cha kaskazini mwa Toshkovka huko Popasna, hali ambayo inaweza kuathiri operesheni ya vikosi vya Urusi katika eneo hilo.












