Mfungwa alivyofaulu kuandika vitabu 81 akiwa gerezani
Iliyochapishwa
Licha ya kufungwa kwa miaka 10 gerezani, kijana Vedastus Goa alifanikiwa kuandika vitabu 81 huku akiwa mfungwa.
Swali ambalo huenda unajiuliza ni kwamba alipata wapi vitabu na hata kalamu za kufanikisha kazi hii ambayo bila shaka ni kubwa?
Kijana huyu aliachiliwa mwanzoni mwa mwaka jana kwa msamaha wa Rais huku akiapa kuendelea na kipaji chake cha uandishi.
Mwandishi wa BBC David Nkya alikutana naye jijini Mwanza Kaskazini mwa Tanzania na hapa Goa anaanza kwa kuelezea sababu haswa iliyomfanya akafungwa.
Picha na Eagan Salla