Mzozo wa Ukraine: Fahamu uwezo wa silaha ya lazer inayodaiwa kutumiwa na Urusi vitani UKraine

Chanzo cha picha, Getty Images
Urusi inadai kwamba imekuwa ikitumia silaha za lazer zinazotumia mionzi vitani Ukraine , ijapokuwa Marekani inasema kwamba hakuna ushhaidi huku Ukraine ikidai ni Propanga za Urusi.
Je silaha za lazer ni silaha za aina gani?
Yury Borisov, naibu waziri mkuu anayesimamia maendeleo ya kijeshi aliambia runinga ya Urusi kwamba aina ya silaha ya Lazer kwa jina Zadira ilikuwaimepelekwa nchiuni Ukraine na kwamba iliichoma ndege moja ya Ukraine isio na rubaniu kwa sekunde tano pekee ikiwa umbali wa kilomita tano.
Hii ilikuwa ni pamoja na mfumo wa leza uliotangulia uitwao Peresvet - uliopewa jina la mtawa wa Orthodox - ambao ungeweza kutumika kuangaza satelaiti zinazozunguka juu ya dunia na kuzizuia kukusanya taarifa.
"Ikiwa Peresvet hupofusha, basi kizazi kipya cha silaha za laser kitasababisha uharibifu wa kitu kinacholengwa - joto huchoma," Bw Borisov alisema.
Hata hivyo, afisa wa Idara ya Ulinzi ya Marekani alisema hajaona "chochote cha kuthibitisha ripoti za lasers kutumika" nchini Ukraine.
Wakati huo huo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alikejeli madai ya Urusi, akiyalinganisha na kile kinachoitwa "silaha za ajabu" ambazo Wanazi wa Ujerumani ywalidai kuunda wakati wa Vita vya Pili vya Dunia.
"Kadiri ilivyokuwa wazi kwamba hawakuwa na nafasi katika vita, ndivyo propaganda zilivyokuwa nyingi kuhusu silaha ya ajabu ambayo ingekuwa na nguvu sana ya kuhakikisha mabadiliko," alisema katika anwani ya video.
"Na hivyo tunaona kwamba katika mwezi wa tatu wa vita kamili, Urusi inajaribu kupata 'silaha yake ya ajabu' ... hii yote inaonyesha ishara za kushindwa kwao ."
Kile ambacho silaha zinaweza kufanya na zisizoweza kufanya
Ni machache yanayojulikana kuhusu mpango wa leza ya Zadira, lakini mwaka wa 2017 vyombo vya habari vya Urusi vilisema shirika la nyuklia la serikali Rosatom limesaidia kuitengeneza kama sehemu ya mpango wa kuunda silaha kwa kuzingatia kanuni mpya za umbo lake, shirika la habari la Reuters liliripoti.
Lakini kuna angalau nchi moja ambayo imeunda silaha ya laser. Mwezi uliopita Israel ilitoa video inayoonyesha mfumo wa leza ukitungua roketi na ndege zisizo na rubani.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe

Waziri Mkuu Naftali Bennett alisema inaweza kuangusha ndege zisizo na rubani, kombora na roketi kwa $3.50 tu (£2.80) kwa shambulio. "Inaweza kuonekana kama hadithi za kisayansi, lakini ni silaha ya kweli," alisema.
Lakini mtaalamu wa ulinzi wa makombora Dk Uzi Rubin kutoka Taasisi ya Mikakati na Usalama ya Jerusalem (JISS) alisema teknolojia ya silaha za leza haitabadilisha usawa wa nguvu kwenye uwanja wa vita nchini Ukraine.
"Zelensky yuko sahihi - sio silaha ya ajabu," aliiambia BBC. "Iliwachukua sekunde kadhaa kuangisha ndege aina ya UAV isikuwa na rubani . Kuna njia bora zaidi za kufanya hivyo, kutumia silaha ya Stinger au kombora lolote la kushambulia ndege ingekuwa nafuu, haraka ba kusafiru masafa marefu zaidi ."
Lasers hufanya kazi kwa kutuma mwali wa mwanga wa infrared ambao huchoma lengo lake hadi kuharibika kabisa.
Dk Rubin alisema nguvu za hata silaha za kisasa za laser bado ni dhaifu sana kuleta mabadiliko makubwa kwenye uwanja wa vita, na silaha kama hizo zina "kiwango cha chini cha mauaji".
"Siyo kama katika filamu ya Star Wars ambapo wanaelekeza bunduki ya leza kwa watu wabaya na kubofya kitufe haraka na mtu mbaya analipuka. Kwa kweli, ni kama tanuri ya microwave tu. Ukitaka kutengeneza kikombe cha maji inachukua muda kuchemka. ichemshe ni sawa. Unahitaji kulenga eneo na kusubiri hadi hadi ipate joto ili kulichom au kuliharibua," alisema.
Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Laser inaweza tu kulenga shabaha moja kwa wakati mmoja, Dk Rubin alisema, wakati mifumo ya ulinzi ya kombora inaweza kulenga shabaha nyingi zinazoingia kwa wakati mmoja.
Zaidi ya hayo, leza hazibadilishwi na hali mbaya ya hewa kwa sababu hazifanyi kazi kwenye mvua au theluji na haziwezi kupenya mawingu.
Hata hivyo "Iron Beam" ya Israel ina mantiki, alisema, lakini hasa kama njia ya kuokoa pesa. Silaha za kutengua makombora za Israel - Iron Dome zameundwa kulinda miji mikubwa dhidi ya makombora yanayoingia, badala ya ndege zisizo na rubani.
"Vita vya makombora ni vita vya rasilimali. Ni nafuu kutengeneza roketi kuliko kujilinda dhidi yao. Kwa hiyo chochote unachoweza kufanya ili kupunguza gharama za kulinda ni muhimu," alisema.
"Silaha za nishati zinaweza kuwa muhimu katika kupunguza gharama - lakini hazitafanya mapinduzi."
Zaidi ya hayo, Urusi inaweza kutumia leza kwenye uwanja wa vita kuwapofusha wanajeshi wa Ukraine, meja jenerali mstaafu wa jeshi la Australia Mick Ryan aliliambia gazeti la Washington Post, ingawa hii ni marufuku chini ya itifaki ya 1995 iliyoongezwa kwenye mkataba wa Umoja wa Mataifa ambayo inakataza silaha kusababisha majeraha kupita kiasi au kuwa na athari kiholela.
Urusi, Marekani, Uingereza na wengine wametia saini sheria hiyo.








