Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Fahamu uhusiano wa matumizi ya vipodozi vyenye kemikali na matatizo ya uzazi
Matumizi ya muda mrefu ya viambato vyenye sumu katika vipodozi yanaweza kusababisha matatizo katika mfumo wa uzazi ikiwemo kuharibika kwa mimba au kusababisha kutokuwa na uwezo wa mtu kushika mimba na hata matatizo ya mfumo katika mishipa ya fahamu kwa mtoto anayezaliwa.
Shirika la Viwango nchini Tanzania Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa hivi karibuni juu ya viambato ambavyo vinaruhusiwa kutumika kwa masharti ya kiasi maalumu , imebainika kwamba matumizi ya muda mrefu ya baadhi ya viambato yana athari katika mwili wa binadamu. Baadhi ya watumiaji wenyewe wa vipodozi hivi pamoja na Mtaalamu wa Masuala ya uzazi Daktari Manuwar Kaguta wa hospitali ya Aghakan Dar es Salaam wamezungumza zaidi na BBC...