Karine Jean-Pierre: Mfahamu msemaji mpya wa kwanza mweusi na mpenzi wa jinsia moja wa Ikulu ya Marekani

Karine

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Rais Biden amemteua Karine Jean-Pierre kama msemaji wake mkuu mpya - ikiwa ni mara ya kwanza mtu mweusi, au mtu ambaye amejitangaza kushiriki mapenzi ya jinsia moja kushika nafasi hiyo.

Bi Jean-Pierre, 44, amehudumu kama msaidizi wa nafasi hiyo tangu Bw Biden achaguliwe. Karine atachukua nafasi ya Jen Psaki, 43 anayeondoka mwishoni mwa wiki ijayo.

Wasemaji wa Ikulu hufanya muhtasari wa habari kila siku na wanahabari wa Ikulu, kumaanisha jukumu hilo ni kuwa kubwa. Bi Psaki anakwenda kufanya kazi katika kituo cha habari cha MSNBC kinachoegemea mrengo wa kushoto.

Kwenye Twitter, alimwita mrithi wake ''mwanamke wa ajabu'' na ''msingi wa maadili''.

''Siwezi kungoja kumuona aking'aa kwani analeta mtindo wake, uzuri na neema kwenye jukwaa,'' alisema.

Karine

Chanzo cha picha, Getty Images

Uchambuzi na Zurcher, mwanahabari wa Marekani Kaskazini

Msemaji wa Ikulu ya White House ni uso wa utawala wa rais kwa vyombo vya habari vya kitaifa, ndani ya nchi na ulimwengu kwa ujumla. Mtu huyo anaweza kuwa mtu anayetambulika mara moja wakati wa migogoro ya kitaifa au kashfa ya kisiasa.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Marekani, uso wa utawala wa Marekani utakuwa wa mwanamke mweusi, na wa mtu ambaye ni mpenzi wa jinsia moja aliyejiweka wazi.

Kupewa nafasi hiyo ni kuonyesha utawala wa Biden ambao umeweka msisitizo katika kuwaweka mbele wanawake weusi - ambao mara nyingi wanachukuliwa kuwa sehemu muhimu, lakini isiyoonekana kisiasa katika muungano wa Chama cha Kidemokrasia - kwenye nafasi za madaraka.

Anaungana na Makamu wa Rais Kamala Harris, Jaji anayekuja wa Mahakama ya Juu Ketanji Brown Jackson, mwenyekiti wa Baraza la Sera za Ndani Susan Rice, Balozi wa Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield, na maafisa wengine wachache na majaji katika majukumu makubwa na maarufu.

Ingawa wasemaji wa Ikulu hawatungi sera, wanasaidia kuunda mtazamo wa umma wa utawala. Jean-Pierre ana changamoto kubwa mbele yake.

Jean-Pierre ametokea wapi?

Karine

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bi Jean-Pierre aliwahi kuwa mchambuzi katika kituo cha Habari cha MSNBC

Bi Jean-Pierre, ambaye hapo awali alikuwa mchambuzi katika kituo cha Habari cha MSNBC, analeta uzoefu wa zaidi ya miongo miwili katika siasa za Kidemokrasia kwenye jukumu hilo.Alizaliwa katika kisiwa cha Caribbean cha Ufaransa cha Martinique na kukulia Queens, New York, alikuwa mkurugenzi mkuu wa kisiasa katika utawala wa Obama.

Wakati wa uchaguzi wa urais wa 2016, alikuwa msemaji wa kitaifa wa MoveOn, kikundi kikuu cha utetezi wa kiliberali.

Kabla ya kujiunga na timu ya wanahabari wa White House, alihudumu kama mkuu wa wafanyakazi wa Kamala Harris, baada ya kuchaguliwa kama makamu wa rais mteule wa Bw Biden.Uteuzi wa Bi Jean-Pierre unakuja kabla ya uchaguzi muhimu wa katikati mwa muhula mwezi huu wa Novemba ambao utaamua jinsi urais mwingine wa Bw Biden utakavyokuwa.