Tanzania yahimizwa kuwekeza katika kilimo cha alizeti

Maelezo ya video, Tanzania yahimizwa kuwekeza katika ukuzaji wa mafuta ya Alizeti
Iliyochapishwa

Wakati nchi nyingi duniani zikiendelea kukumbwa na uhaba wa mafuta ya kupikia kutokana na changamoto mbalambali janga la Corona na Vita vya Urusi na Ukraine vikitajwa kama moja ya sababu, Tanzania ni moja ya nchi zinazoathirika kutokana na hali hiyo.

Serikali ya Tanzania imeanza kuwekeza kwenye zao la alizeti ili kuimarisha uzalishaji wa ndani.

Mkoa wa Dodoma unategemewa zaidi katika uzalishaji wa mafuta ya alizeti. Humphrey Mgonja akiwa Dodoma ameandaa taarifa hii.