Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Ifahamu misingi ya Muungano pekee ulio hai barani Afrika
Tanzania hii leo inaadhimisha miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Maadhimisho hayo yanafanyika kitaifa huko jijini Dodoma, ambapo mbali na viongozi wengine watakaohudhuria kilele cha sherehe hizo, mgeni rasmi atakuwa rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Wakati maadhimisho haya yakifanyika, Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema, katika kipindi cha mwaka mmoja, changamoto zaidi ya kumi za muunganamo zimepatiwa ufumbuzi.
Mwandishi wa BBC Caro Robi amezungumza na mwanasiasa mzoefu wa Zanzibar, Ismail Jussa na Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo ambaye anaaza kuelezea misingi ya Muungano huo pekee ulio hai barani Afrika.