Tanzania: Bei mpya ya mafuta ilivyo mwiba kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri

Iliyochapishwa

Baadhi ya wamiliki wa vyombo vya moto vya usafiri wameonesha kuathiriwa na upandaji wa bei za mafuta uliotangazwa na EWURA hapo jana.

BBC imeingia mitaani na kuongea na baadhi ya wamiliki wa vyombo vya moto ambao wengi wao wanatamani kuona kama bei ya mafuta itapanda basi nazo gharama za usafirishaji zipandishwe.

Bei mpya ya petroli kwa mafuta yanayopokelewa kupitia Bandari ya Dar es salaam itakuwa Sh2,861 kutoka Sh 2,540 ikiwa ni ongezeko la Sh321.

Bei ya nishati hiyo inapanda wakati wananchi wakilalamika kuongezeka kwa bei za bidhaa mbalimbali za vyakula hasa wakati huu wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

'Kama bei ya mafuta imepanda basi bei ya usafirishaji abiria nayo ipandishwe'