Vita vya Ukraine: Barabara ya Bucha iliyojaa mabaki ya mizinga na maiti zilizoteketea

Chanzo cha picha, BBC/Lee Durant
Barabara ya suburban mjini Bucha iligeuka kuwa uwanja wa maafa baada ya jaribio la vikosi vya Urusi kuteka mji mkuu wa Kyiv na kumtimua madarakani Rais Volodymyr Zelensk kutibuka.
Tukio hilo lilitokea siku mbili au tatu baada ya vikosi vya kwanza vya Urusi kuvuka mpaka na kuingia nchini Ukraine mnamo Februari 24, wakati vikosi vya Ukraine vilipoharibu magari ya kivita ya Urusi yaliyokuwa yakipita katika mitaa ya Bucha kuelekea mjini Mkuu wa Kyiv.
Msafara huo wa Urusi uliovamiwa na vikosi vya Ukraine ni moja ya mashambulio makali dhidi ya wanajeshi wa Urusi.
BBC ilifanikiwa kufika mji wa Bucha siku ya Ijumaa wakaati kundi la mwisho la jeshi la Urusi lilikuwa likiondoka katikamji huo, kama sehemu ya kile ambacho Kremlin imedai ni uamuzi wa kimkakati ili kuelekeza oparesheni yao mashariki mwa Ukraine.
Moscow inasema, bila uthibitisho kwamba malengo yake ya vita katikati mwa Ukraine yamefikiwa, na kamwe hayakujumuisha kuteka mji wa Kyiv.
Ukweli ni kwamba ulinzi mkali uliwekwa na Majeshi ya Ukraine uliwazuia nje ya mji mkuu, na ushahidi ni pamoja na uharibifu wa msafara wa magari ya kivita ya Urusi ambayo mabaki yake yamesalia kwenye barabara hiyo ya miji.

Chanzo cha picha, BBC/Kathy Long
Wiki mbili au tatu za vita wavamizi wa Urusi waliishiwa na kasi. Kwenye barabara huko Bucha unaweza kuona ni kwa nini.
Wanajeshi wenye ujuzi kutoka vikosi vya anga vya Urusi waliingia mjini kwa magari ya kivita mepesi ambayo hata yanaweza kubebwa na ndege.
Walikuja kutoka uwanja wa ndege wa Hostomel, umbali wa maili chache, ambao ulishambuliwa na kutekwa na askari wa miamvuli wa Urusi waliotua kwa helikopta siku ya kwanza ya uvamizi. Hata wakati huo, kulikuwa na upinzani mkali kutoka kwa vikosi vya Ukrane.
Walipotoka mji wa Bucha kuelekea Kyiv, waliviziwa na kushambuliwa vikali na vikosi vya Ukraine.
Barabara ni nyembamba na imenyooka, mahali pazuri pa kuvizia. Walioshuhudia walisema raia wa Ukraine walishambulia msafara huo kwa kutumia ndege zisizo na rubani za Bayraktar zilizonunuliwa kutoka Uturuki. Wakazi wanasema walinzi wa kujitoleaji wa wa eneo la Ukraine pia walikuwa katika eneo hilo.
Kadri walivyopambana ndivyo yakiongoza na yale ya nyuma yalitolewa na kuwafunga wengine. Mabaki hayajaguswa. Mikanda ya makombora ya mizinga 30 bado imelala kando ya barabara, pamoja na vipande vingi vya zana hatari na zilizoharibiwa ziliachwa nyuma.
Wnajeshi kadhaa wadogo walikimbia, wakiomba watu wa eneo hilo wasiwawawasilishe kwa ulinzi wa eneo la Ukraine. kazi wa karibu miaka 70 ambaye alijiita mjomba Hrysha, alisema: "Niliwahurumia. Walikuwa wadogo sana, kati ya mika 18 hadi 20."
Inaonekana kama Warusi, walipokuwa wakijiandaa kutoka Bucha, hawakuwa na huruma hata kidogo. Takriban watu 20 waliouawa miili yao ilikuwa imetapakaa barabarani wakati wanajeshi wa Ukraine walipokiingia katika mji huo. Baadhi yao walikuwa wamefungwa mikono nyuma ya migongo yao. Meya huyo alisema wamezika watu 280 kwenye makaburi ya pamoja.
Raia kidogo waliosalia katika mji huo walisema walijaribu kujitenga na wavamizi hao wa Kirusi. Waliwasha moto wa kuni nje yanvyumba zao za zamano Khrushchev, wakipikia nje baa ya kuishiwa na gesi, umeme na maji .
Wahudumu wa kujitolea wanaleta vifaa kutoka Lviv magharibi mwa Ukraine, na kutoka nchi zilizo mbali na vita, angalau kijiografia.
"Huu ndio mkate wa kwanza ambao tumeupata ndani ya siku 38," alisema mwanamke anayeitwa Maria, akitazama mfuko wa plastiki uliokuwa na maandazi ya kiasi. Binti yake Larysa alinionyesha huku akikuzunguka jengo la ghorofa lililojengwa na Usovieti.
Baadhi ya watu ambao walikuwa wameondoka kwenda maeneo salama, au nje ya nchi, walikuwa wamefunga milango ya usalama. Warusi waliyafungua kwa kung'oa nguzo za zege na nguzo za mlango.

Chanzo cha picha, BBC/Kathy Long

Vita vya Ukraine: Maelezo zaidi














