Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Siku ya Wanawake Duniani:Gertrude Mongella azungumzia hatua walizopiga wanawake hadi sasa
Siku ya Wanawake duniani huadhimishwa tarehe 8 mwezi Machi kila mwaka ambapo huwapa fursa wanawake kutathmini ni wapi walipotoka, wapi walipo na wapi wanatarajia kufika.
Mwandishi wa BBC Aboubakar Famau amepata fursa ya kufanya mahojiano na Mama Gertrude Mongella mwanasiasa mkongwe aliyewahi kushika nyadhfa mbalimbali za uongozi nchini Tanzania kama vile Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Mbunge wa Bunge la Afrika, Waziri wa Wizara ya Mali asili na Utalii, Katibu Mkuu msaidizi wa Umoja wa mataifa (UN) na kubwa zaidi Mwanaharakati aliyeongoza mkutano wa Beijing mwaka 1995 uliopigania haki za Wanawake Duniani kote.