Rodney Kiggundu: ‘Watu wananiambia umetupa ushauri mbaya’

Iliyochapishwa

Kutana na kijana kutoka nchini Uganda anayevuma kutokana na Video yake inayohamasisha watu kufurahia maisha kwa kutumia pesa zao

Jina lake halisi ni Rodney Kiggundu lakini kwa jina maarufu anajulikana kama EAT THAT MONEY GUY kijana mfanyabiashara wa masuala ya Teknolojia ambaye msemo wake wa EAT THAT MONEY umempa umaarufu kwa kutumiwa na maelfu ya watu katika mtandao wa TikTok pekee ikiwemo watu maarufu na wasanii wa muziki kutokana nchi mbali mbali za Afrika Mashariki

Anasema amekuwa akifuatwa na watu wanaotumia vibaya fedha zao kwa starehe wakimsema kuwa amewashauri vibaya kupitia video hiyo.

Mwandishi wa BBC @frankmavura amefanya mahojiano kwa nia ya mtandao na kijana Rodney