Katibu wa Chadema :Pumzi bado tunayo

Iliyochapishwa

Katibu wa chama cha upinzani Tanzania Chadema , John Mnyika amesema kuwa uamuzi wa kesi dhidi ya mwenyekiti wao Freeman Mbowe, haina maana kuwa wamekata tamaa, watapamana na kuleta utetezi katika kesi hiyo.

Jana, Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imesema Mbowe na wenzake watatu Mohamed Ling'wenya, Halfan Bwire na Adam Kasekwa wana kesi ya kujibu kuhusiana na tuhuma mbalimbali zikiwemo za kupanga njama za kufanya vitendo vya kigaidi.