Patrick Kimaro : 'Ni maandalizi ya siku yangu ya kufa'
Iliyochapishwa
Kwa kawaida kila mtu anafahamu kuwa atakufa lakini kuzungumzia au kujiandaa kwa ajili ya kifo ni suala sio la kawaida kabisa
.
Hata kama mtu ni mgonjwa mahututi sana, familia au mgonjwa hawezi kuanza kutaka kaburi kuanza kuandaliwa.
Lakini , ukijaaliwa kufika, katika kijiji cha Mbosho, wilayani Machame, katika mkoa wa Kilimanjaro, ambapo ndipo anapoishi Patrick Kimaro, mwenye umri wa miaka 59, ukiingia tu katika nyumba yake, mkono wa kulia utakutana na kaburi, aliloliandaa kwa ajili yake.