Ubaguzi wa rangi huenda ukaathiri wanawake wengi zaidi wanaoharibikiwa na mimba Uingereza

Iliyochapishwa

Ubaguzi wa rangi unaonekana upo kwenye mfumo wa huduma za afya Marekani na Uingereza. Huenda ukaathiri wanawake wengi zaidi wanaoharibikiwa na mimba. Hii ni kwa mujibu wa madaktari nchini humo.

Chuo cha Royal cha wataalamu wa ujauzito na magonjwa ya kinamama nchini Uingereza kimekanusha kuwa kuna ubaguzi huo, na hivyo utafiti unahitajika kufanyika zaidi kwani wanawake wenye asili ya Afrika wako hatarini zaidi Mimba zao kuharibika kwa asilimia 40 kuliko wanawake wazungu.