Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Rais Samia:Haiwezekani polisi wafanye mauaji halafu wajichunguze wenyewe
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekemea matukio ya mauaji ambayo yamekua yakiripotiwa katika siku za hivi karibuni nchini Tanzania, amesema kuwa kamati maaulum itachunguza chanzo cha mauaji hayo.
Hivi karibuni Tanzania imerekodi idadi ya mauaji katika mikoa kadhaa ikiwemo Mtwara, Mbeya, Mwanza, Moshi na Dodoma.
"Nimemuelekeza Waziri Mkuu, aunde kamati nyingine iende ikafanye uchunguzi wa mauaji yaliyofanywa na Jeshi la Polisi alafu watuletee taarifaa, lakini wakati huo huo, nataka Jeshi lako lijitafakari waone kinachotokea ni misingi ya jeshi la polisi''. Alisema Rais Samia