DJ Sinyorita: DJ huyu machachari wa Tanzania yuko mbioni kuacha kazi hii
Iliyochapishwa
Katika Nyota wa Afrika Mashariki wiki hii tumezungumza na Mwanaisha Akida almaarufu kama @djsinyorita ambaye ni mshindi wa tuzo ya Afrimma ya DJ Bora Afrika na kuzidi kuwa ni kati ya maDJ wanaofahamika sana akiwa na wafuasi zaidi ya Milioni 2 katika mtandao wa Instagram na kuendelea kujizolea mashabiki toka nchini Tanzania, Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla.
Je DJ huyu machachari yuko mbioni kuacha kazi hii ya u-DJ ambayo anasema kwa sasa ndio inayomuweka mjini?
Mahusiano yake je? Hayayumbishwi na kazi zake hifi ambazo mara nyingi hufanyika usiku?
Hayo na mengine mengi ameyaweka bayana katika mahojiano aliyoyafanya na mwandishi wa BBC @frankmavura
@djsinyorita