Seif Kisauji: 'Familia yangu iliponiona katika TikTok iliona naidhalilisha'

Maelezo ya video, Seif Kisauji: 'Familia yangu iliponiona katika TikTok iliona naidhalilisha'
Iliyochapishwa

Kutana na Seif Kisauji almaarufu kama ‘Babu wa TikTok’ ambaye amekuwa akichapisha video mbalimbali zinazomuonesha akicheza nyimbo huku akiwaasa vijana kupitia mada mbalimbali anazozitoa kila uchao kwa njia ya uchekeshaji.

Akiwa na miaka 57 amefanikiwa kuwa ni Kati ya watu wazima waliopo kwenye mtandao unaopendwa sana na Vijana huku akiwavuta na wazee wengine kujiunga nae katika matamasha pindi akitumbuiza ili wafurahie maisha.

Mwandishi wa BBC @frankmavura amefanya mahojiano haya maalumu na Babu wa TikTok