Zuhura Yunus :Mtangazaji wa BBC kuondoka baada ya kuitumikia kwa takriban miaka 14

Iliyochapishwa

Mtangazaji mashuhuri wa BBC Zuhura Yunus anaondoka kutoka Shirik ala habarai la BBC baada ya kulitumikia kwa takriban miaka 14.

Zuhura alitangaza kipindi chake cha mwisho cha Dira ya Dunia Ijumaa usiku majira ya saa tatu Afrika mashariki.

Hata hivyo amebakiza siku kadhaa za likizo kabla ya kuondoka rasmi.

Mtangazaji huyo aliyejiunga na BBC Swahili mwaka 2008 amesema anataka kuutumia muda wake sasa kuendelea na uandishi na mambo mengine nje ya BBC.