Tazama rubani alivyonusurika baada ya treni kuigonga ndege yake
Iliyochapishwa
Polisi huko Los Angeles, Marekani wamemuokoa rubani aliyekwama kwenye ndege yake iliyoanguka sekunde chache kabla ya hajagongwa na treni. Mkazi wa eneo hilo alinasa tukio hilo hatari kwenye simu yake. Rubani huyo anaendelea kupata nafuu hospitalini na hakuna aliyejeruhiwa kwenye treni hiyo.