Vijana wanaoongeza ukubwa wa midomo ili kuwa sawa na picha wanazoziona mtandaoni

Iliyochapishwa

BBC imebaini kuwa baadhi ya wanavipodozi wanatoa huduma ya kuongeza ukubwa wa midomo kwa nia ya kuipendezesha kwa vijana wadogo. Ni kinyume cha sheria kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 18 kupokea huduma ya vipodozi vya kuongeza midomo nchini Uingereza, lakini Liv aliweza kufanyiwa upasuaji huo akiwa na umri wa miaka 16. Anasema alihisi kufanya hivyo baada ya kuona picha za watu kwenye mitandao ya kijamii