Agnes Ndunguru: ‘Nimeokoa maisha ya wanawake na watoto wengi Tanzania’
Iliyochapishwa
Katika mfululizo wa makala kuhusu vijana walio chini ya miaka 30 tunaangazia vijana waliofanya vizuri na wanaoendelea kufanya vizuri katika Teknolojia, Siasa na Kijamii kwa nchi za Afrika Mashariki na leo tunae @midwifeaggie ambaye ni mkunga kijana anayeokoa maisha ya mama waja wazito na watoto.
Ameamua kuishi ndoto yake kuhakikisha hakuna vifo vitakavyosababishwa na matatizo ya ujauzito au wakati kujifungua nchini Tanzania.
Takribani miaka saba ya kufanya kazi Agnes Ndunguru amehudumia zaidi ya wajawazito elfu sita na kuwasaidia kujifungua vyema wengine zaidi ya elfu mbili nchini humo.
Mwandishi wa BBC @frankmavura amemtembelea na kuandaa taarifa ifuatayo