Afcon: Siri ya Cape Verde kufuzu kwa michuano ya Afcon ni ipi
Iliyochapishwa
Imesalia chini ya mwezi mmoja kabla ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kung’oa nanga nchini Cameroon – na kwa mara nyingine Cape Verde itashiriki mashindano hayo. Hii itakuwa mara ya tatu katika michuano mitano iliyopita kwa taifa hilo dogo la visiwa lenye watu takriban nusu milioni kufika fainali.
Lakini je,siri yao ni nini?