Kenya: Mahakama Kuu yaamua kazi za nyumbani ni kazi
Iliyochapishwa
Suluhu ya talaka ya Mary Wambui imekuwa mfano nchini Kenya, baada ya Jaji mwandamizi kukiri kwamba kazi za nyumbani ni kazi katika uamuzi wa kesi ya ndoa.
Huu ni utekelezaji wa kwanza wa Sheria ya Mali ya Ndoa ya mwaka 2013.
Hili ni tamko la kihistoria kwa wanawake kote barani Afrika na sasa linaweza kutumiwa na majaji wengine katika kuamua kesi ambapo akina mama wa nyumbani wanahusika na hivyo kuwapa fidia ya pesa inayohitajika.